Ni gharama kubwa kuwa na Mwanasheria mzuri asiye na uzalendo

Ni gharama kubwa kuwa na Mwanasheria mzuri asiye na uzalendo

Ila twende na ukweli LISSU anakosea sana kujifanya yupo mstari wa mbele wa kuangalia HASARA NA SI FAIDA kwa ajili ya vizazi vijavyo.......na hii ni rahisi sana kwa LISSU kutumiwa na hawa VIBARAKA wenye maslahi yao kwenye hili kutuletea matatizo nchini kwa kuhamsha TAHARUKI kama wafanyavyo sasa
 
Nchi imeibiwa vya kuibiwa. Madini yetu yamesombwa vya kusombwa kwenda kujenga ulaya. Rais amesimama kidete kutetea rasilimali zetu halafu anaibuka kibaraka mmoja hivi anawatetea wezi. Nina mashaka na uzalendo wake. Nina mashaka na usalama wa afya ya ubongo wake
Umeongea jambo muhimu sana mkuu.

Hata enzi za ukoloni walikuwepo vibaraka waliohakikisha hatupati uhuru ili wafaidike na choroko na dengu walizokuwa wanalipwa.

Tundu Lisu anapaswa kupingwa kwa nguvu zote. Mtu mjivuni na mjuaji ilihali hawezi hata kujichoma sindano akiumwa... Nikimuangalia Lisu ninashuhudia madhara ya rushwa
 
Nchi imeibiwa vya kuibiwa. Madini yetu yamesombwa vya kusombwa kwenda kujenga ulaya. Rais amesimama kidete kutetea rasilimali zetu halafu anaibuka kibaraka mmoja hivi anawatetea wezi. Nina mashaka na uzalendo wake. Nina mashaka na usalama wa afya ya ubongo wake
Acheni ujinga wenu nyie, nyie ndio majizi mliotufikisha hapa, Lisu na Upinzani walipiga kelele sana sana juu ya huu ujinga wenu, mkataka kumfunga, mmesahau yote haya leo?? Nyie ni wezi na msio n aibu. Kwa mwana CCM mwenye akili angekaa kimya tu maana dhambi hii inawala hadi mwisho. Hizi kelele sijui mnazitoa wapi leo
 
Nchi imeibiwa vya kuibiwa. Madini yetu yamesombwa vya kusombwa kwenda kujenga ulaya. Rais amesimama kidete kutetea rasilimali zetu halafu anaibuka kibaraka mmoja hivi anawatetea wezi. Nina mashaka na uzalendo wake. Nina mashaka na usalama wa afya ya ubongo wake

Hapa ndipo ccm na serikali yake walipotufikisha,wanajivunia upumbavu wetu,haiwezekani walioliingiza Taifa kwenye kadhia hii wapo na wengine tunawalinda na kuwatunza kwa kodi zetu wao pamoja na vizazi vyao,halafu tumgeukie Tundu Lissu ambaye hajawahi kukanyaga hata korido za chumba lilimoketi baraza la mawaziri lililopitisha mikataba hii inayotunyonya!

Magufuli ni sehemu ya serikali tangu awamu ya tatu,alikuwemo barazani wakati mikataba hii mibovu inaandaliwa,wagonga meza wa ccm walikuwemo bungeni wakati bunge linamfukuza Mh.Zitto aliyekuwa amebeba agenda ya Buzwagi kupitia Chadema,iweje leo muwasahau waliotufikisha hapa na kuwageukia wahanga walioteswa na dola walipojaribu kuipinga mikataba hii ya kifisadi?

Wanaopaswa kuwajibika hapa ni viongozi wote wa awamu ya 3&4 na mawaziri wao wote,hao ndiyo waliyolinajisi Taifa kwa kuingia mikataba ya hovyohovyo!Mikataba hii ni Kazi ya mikono ya ccm na serikali yake,Tundu Lissu hajawahi kuwa sehemu ya serikali iliyopitisha mikataba hii mibovu,kumuhusisha nayo ni dalili ya wazi inayoashiria kuwa unapaswa "utumwe mirembe".
 
Tatizo unaleta Dini kwenye siasa,hivyo hatuwez kuelewana ikiwa utashindwa kuvitofautisha hivi vitu viwil,unamuweka Mungu asipohusika,nakushaur ondoa wazo la Dini ndiyo utaelewa kisemwacho tofaut na hapo utatoka patupu mkuu
Hakuna kitu chochote chini ya jua kinacho fanyika bila kumhusisha Mwenye Enzi Mungu! Ndiyo maana watu wa siasa na wafanya biashara wakubwa wazungu kwa wahindi, hukimbilia kwa Beyond human thinking powers in order to succeed! COMMON SENSE IS NOT COMMON kwa kweli! Bye bye!
 
Nchi imeibiwa vya kuibiwa.

Unaongea haya ukiwa na ushahidi au ni hisia na imani kwamba tunaibiwa? Kama ushahidi upo, na kama Serikali ina ushahidi wa nchi kuibiwa, kwa nini hakuna kesi mahakamani?

Kwa nini tunatumia kangaroo courts kuhukumu na si mahakama?

Madini yetu yamesombwa vya kusombwa kwenda kujenga ulaya.

Moja, hii yote ni kwa mujibu wa mkataba. Kama mkataba unawaruhusu kusomba hayo madini kosa lao ni lipi hasa?

Pili, unaposema yamesombwa ni kama vile wanaenda wanaokota madini na kuondoka nayo. Tuwe wakweli kwamba wameweka mitaji yao kuweza kuyapata hayo madini. Mitaji hiyo sisi hatuna na ndiyo maana tumewaruhusu wao kuja.

Rais amesimama kidete kutetea rasilimali zetu halafu anaibuka kibaraka mmoja hivi anawatetea wezi.

Rais kusimama kidete hakuna manufaa yoyote kama hawezi kushinda kesi. Rais kusimama kidete hakuna manufaa yoyote kama nchi itaingia hasara kwa (1) kukosa wawekezaji (2) kulipishwa faini mahakamani (3) kushindwa kutumia hayo madini/mchanga kupata fedha/mapato.

Pia, tujadili kwa hoja na si kupeana majina kwamba Lisu ni kibaraka. Tusiendeshwe kwa ushabiki na mihemeko. Jibu hoja za Lissu. Si kumwita kibaraka.

Nina mashaka na uzalendo wake. Nina mashaka na usalama wa afya ya ubongo wake

Uzalendo si kukubali kila linalofanywa na Serikali. Uzalendo pia ni kuikosoa Serikali pale inapofanya makosa. Kambona aliitwa majina yote lakini leo hii Ujamaa upo wapi?

Tujifunze kujadiliana kwa hoja na ustaarabu na si kuonyesha ujinga wetu kwa mihemeko.
 
Ila twende na ukweli LISSU anakosea sana kujifanya yupo mstari wa mbele wa kuangalia HASARA NA SI FAIDA kwa ajili ya vizazi vijavyo.......na hii ni rahisi sana kwa LISSU kutumiwa na hawa VIBARAKA wenye maslahi yao kwenye hili kutuletea matatizo nchini kwa kuhamsha TAHARUKI kama wafanyavyo sasa
Lissu aliiona hasara miaka 17 iliyopita wakati wewe hujazaliwa.
 
Nchi kuwa na Mwanasheria mashuhuri asiye na uzalendo ni hasara kubwa sana

Huyu ni hatari kwa taifa maana huwa mchumia tumbo na mbinafsi, aweza asionekane kuwasaidia hawa wezi lakini akawaibia siri zetu na kuwapa mbinu mbalimbali za kutusumbua.

Ni aibu kubwa kwa TLS kuongozwa na bwana huyu, ambae badala ya kusaidia nchi namna ya kufanya ili nchi ilipwe na hawa wezi, yeye anakuwa upande wao na kumtisha rais kwamba atashitakiwa.

Mtu wa namna gani huyu, Tundu Lisu uzalendo wako uko wapi. Ni nini umuhimu wa sheria yako kwa nchi yetu?
You are a good lawyer who doesn't care when the isue is for public interest.

Kwa hili kama hauko upande wetu, kutetea maslahi ya nchi yetu ni bora ukae kimya utuachie tu pale tutakapoishia.

Mungu wetu ni wakili wa haki namba 1 atatutetea na tutashinda kwa imani.

Ni hasara kubwa kwa wazazi waliozaa kiumbe kama wewe bora hiyo mimba ingetoka tu.
 
Mnafiki huyo, naona kavuta mpunga wa kuwatetea. Ila safari hii watakufa wanafiki wengi, maana wanavuta mipunga na serikali lazima ishinde.
 
Nchi imeibiwa vya kuibiwa. Madini yetu yamesombwa vya kusombwa kwenda kujenga ulaya. Rais amesimama kidete kutetea rasilimali zetu halafu anaibuka kibaraka mmoja hivi anawatetea wezi. Nina mashaka na uzalendo wake. Nina mashaka na usalama wa afya ya ubongo wake
Kuwatetea wezi umeona wapi? Unadhani wewe peke yako ndiye unayepata taarifa? Tunajua alichosema Lissu, acha kupotosha umma
 
Nchi imeibiwa vya kuibiwa. Madini yetu yamesombwa vya kusombwa kwenda kujenga ulaya. Rais amesimama kidete kutetea rasilimali zetu halafu anaibuka kibaraka mmoja hivi anawatetea wezi. Nina mashaka na uzalendo wake. Nina mashaka na usalama wa afya ya ubongo wake
sasa kama imeibiwa hiyo miCCM iko wapi imelala wao si ndio wenye dola. lakini ivi kuna mwizi asiyekuwa CCM?
 
Nchi imeibiwa vya kuibiwa. Madini yetu yamesombwa vya kusombwa kwenda kujenga ulaya. Rais amesimama kidete kutetea rasilimali zetu halafu anaibuka kibaraka mmoja hivi anawatetea wezi. Nina mashaka na uzalendo wake. Nina mashaka na usalama wa afya ya ubongo wake
NYIE NDO WASHAURI WA RAISI?
 
Nchi kuwa na Mwanasheria mashuhuri asiye na uzalendo ni hasara kubwa sana

Huyu ni hatari kwa taifa maana huwa mchumia tumbo na mbinafsi, aweza asionekane kuwasaidia hawa wezi lakini akawaibia siri zetu na kuwapa mbinu mbalimbali za kutusumbua.

Ni aibu kubwa kwa TLS kuongozwa na bwana huyu, ambae badala ya kusaidia nchi namna ya kufanya ili nchi ilipwe na hawa wezi, yeye anakuwa upande wao na kumtisha rais kwamba atashitakiwa.

Mtu wa namna gani huyu, Tundu Lisu uzalendo wako uko wapi. Ni nini umuhimu wa sheria yako kwa nchi yetu?
You are a good lawyer who doesn't care when the isue is for public interest.

Kwa hili kama hauko upande wetu, kutetea maslahi ya nchi yetu ni bora ukae kimya utuachie tu pale tutakapoishia.

Mungu wetu ni wakili wa haki namba 1 atatutetea na tutashinda kwa imani.
Uzalendo ni pamoja na kuwasikiliza wengine, tangu miaka nenda rudi WAPINZANI wanaililia mikataba hii ijadiliwe Bungeni na hasa kitaifa ili na sisi wa darasa la saba tuione tena itafasiriwe kwa kiswahili, lakini CCM walikataa kata kata.

Kwa namna yoyote ile unavyotaka kujinasua kwenye mtego ni lazima uwe makini mno kujinasua vinginevyo ukikurupuka vibaya unaweza ukajimalizia hapo hapo.

Sasa process za kujitegua kwenye mtengo ndiyo zile za kuwashirikisha wabunge werevu wa sheria, wanasheria nguli nchini kabla ya kumpa adhabu kibaka wetu tuliyemkamata ili tumbane kote kote hasa kwenye sheria za mikataba ambako wengi hatujui. (tu weupe pee)

Wengi tunaikubali move ya Rais wetu, lakini je hakuna kingine ambacho kingefanywa ili impact yake isiwe kikwazo kipya kwetu.

Hata mimi nyumbani kwangu kuna wezi wanaendelea kuniibia kuku wangu kila mara, pamoja na kuwa wameniibia kwa miaka mingi lakini hawachoki ndiyo kwanza wanazidi kuwaiba zaidi.

Sasa nimeapa siku nikimkamata mwizi wangu live sitajali kwamba huyo ni siku yake ya kwanza kaniibia ama ni jirani yangu hapana, ni RUNGU la kichwa, awe hai ama mfu hilo sintajali kwa kweli maana nimeumia kwa miaka mingi mno.

Hoja, Je huu utakuwa ndiyo uamuzi pekee niliopanga kuuchukua? hakuna alternative solution naweza nikaitumia badala ya hii ya Rungu la Kichwa kwa huyu mwizi wangu?
 
Ila twende na ukweli LISSU anakosea sana kujifanya yupo mstari wa mbele wa kuangalia HASARA NA SI FAIDA kwa ajili ya vizazi vijavyo.......na hii ni rahisi sana kwa LISSU kutumiwa na hawa VIBARAKA wenye maslahi yao kwenye hili kutuletea matatizo nchini kwa kuhamsha TAHARUKI kama wafanyavyo sasa
Kipindi analazwa ndani na mkapa kwa kupigania maslahi ya hiyo mkataba inaonekana ilikuwa bado mtoto mdogo
 
Lisu anapinga namna mkubwa anavyoenenda, anatoa ushauri nini kianze kwanza au kingeanza kwanza. Si lazima wote kuzungumza neno linalofanana....muhimu ni kutakiana mwisho mwema.

kasema nini kianze?
 
Mnafiki huyo, naona kavuta mpunga wa kuwatetea. Ila safari hii watakufa wanafiki wengi, maana wanavuta mipunga na serikali lazima ishinde.
Lissu kipindi anaswekwa ndani na mkapa inaonekana ilikuwa unasema vidudu huko
 
Back
Top Bottom