Ni gharama kubwa kuwa na Mwanasheria mzuri asiye na uzalendo

Ni gharama kubwa kuwa na Mwanasheria mzuri asiye na uzalendo

Nchi kuwa na Mwanasheria mashuhuri asiye na uzalendo ni hasara kubwa sana

Huyu ni hatari kwa taifa maana huwa mchumia tumbo na mbinafsi, aweza asionekane kuwasaidia hawa wezi lakini akawaibia siri zetu na kuwapa mbinu mbalimbali za kutusumbua.

Ni aibu kubwa kwa TLS kuongozwa na bwana huyu, ambae badala ya kusaidia nchi namna ya kufanya ili nchi ilipwe na hawa wezi, yeye anakuwa upande wao na kumtisha rais kwamba atashitakiwa.

Mtu wa namna gani huyu, Tundu Lisu uzalendo wako uko wapi. Ni nini umuhimu wa sheria yako kwa nchi yetu?
You are a good lawyer who doesn't care when the isue is for public interest.

Kwa hili kama hauko upande wetu, kutetea maslahi ya nchi yetu ni bora ukae kimya utuachie tu pale tutakapoishia.

Mungu wetu ni wakili wa haki namba 1 atatutetea na tutashinda kwa imani.
Mlishinda?
 
Indeed!
 
Sinda69 Jiongeze kidogo
Humu jamvini kuna uzi wa Mwanasheria Mkuu mpya kabla ya kuteuliwa akizungumzia suala la mikataba ya madini na uwezekano wa sisi kushtakiwa
Alichokisema ni sawa sawa kabisa na maoni ya Lissu.
Tofauti ni mmoja kamiminiwa risasi lukuki na mwingine kaukwaa UanasheriaMkuu
Shida ya hawa watu hawataki kuusikia na kuufuata ushauri unaotolewa na upande wa upinzani.Wao upinzani ni uadui.Tunasafari ndefu sana.
 
Kwa akili ndogo tu ndo ngumu, otherwise sema majibu uliyonayo kwa maswali niliyokuuliza YANAKUSUTA NAFSI!

ha ha mkuu, kwa lipi? Lissu? Lissu huyu huyu au? who is he? umebaki kudhani unasutwa nafsi
 
angalia lugha aliyotumia, politely, friendly, yet educative and logical

angalia yule mpuuzi mwingine anavyoongea sasa
Sifa kubwa ya Lissu huwa yupo bold na anaongea ukweli ambao una irritate lkn ndio ukweli, ni sio mtu anayesubiri kuteuliwa. Chungu lakini ndio dawa, mkizoea sugarcoat comments tutazalisha taifa la wapumbavu na waoga.
 
Hatujui next minute itakuaje ndiyo maana wakristo tuliambiwa kesheni mkiomba, siyo aibu wala dhambi kusema nina weledi kwakua mafundisho yake yanasema "Katika viumbe vyote vilivyoumbwa, mwanadamu kaumbika kuliko vyote"
Kwanini? Kwa sababu amepewa uelewa, maarifa na akili. Ukizitumia au ukisema unazo, siyo dhambi.

Isis wanaua watu wasio na hatia.
Usa wanaua watu wasio na hatia.
Watu wanaokosa chakula kwa mwaka idadi inaongezeka.
Majanga ya asili yanazidi kuikumba dunia.

Kweli Mungu aache kushughulika na hivyo vitu aje kushughulika na hili la kujitakia?

Kwenye biblia kuna mstari unasema "Laana isiyo na sababu haimpati mtu" na pia ni agizo la Mungu la kusema "Jisaidie na mimi nitakusaidia"

Tunaingia kwenye shimo kwa uzembe wetu kisha tumpe mzigo wa kutulinda? Inaingia hata akilini?

NB. Huna sababu ya "Mijitu kama nyinyi" ili kuonyesha upo serious na hoja yako
Umemjibu kwa akili sana.
 
Lisu anapinga namna mkubwa anavyoenenda, anatoa ushauri nini kianze kwanza au kingeanza kwanza. Si lazima wote kuzungumza neno linalofanana....muhimu ni kutakiana mwisho mwema.
Nawachukia wale wanaodhulumu haki na hata sifa za watu. Kama Mhe. Tundu Lissu sio mzalendo kwa taifa hili-( Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) basi hakuna mtu mzalendo katika taifa hili na maana ya neno mzalendo itakuwa imebadilika. Mzalendo ni mtu mwenye mapenzi ya kweli kwa nchi yake, sioni na sishawishiki kuwa Mheshimiwa Tundu Lissu hana sifa hii.
 
Back
Top Bottom