Uchaguzi 2020 Ni Dkt. Magufuli pekee 2020

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Napenda kuungana na mamilioni ya Watanzania kumpongeza Dkt. John Pombe Magufuli kuchukua fomu ya kugombea urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ninamtakia kila la heri airejeshe tayari kwa ushindi Octoba 28, 2020.

Nasema ushindi kwa maana kati ya wote tuliosikia wanagombea hakuna anayefikia hata robo ya uzalendo, uadilifu, uchapa kazi, ufuatiliaji na ucha Mungu alio nao Dkt. Magufuli ambao umetuvusha miaka mitano mpaka sasa tupo kwenye uchumi wa kati.

Dk. Magufuli ndio tumaini na tegemeo la pekee la Mtanzania mnyonge na maskini kwani amewawezesha kusoma bure shule ya Msingi hadi sekondari, amewajengea hospitali, vituo vya afya, Zahanati kila kona ya nchi na kuwaweka Madaktari, Madawa na vifaa tiba.

Ni Dkt. Magufuli huyu huyu ametupatia heshima Watanzania kwa kuhakikisha tunanunua ndege zetu wenyewe; tunajenga reli ya kisasa ya umeme ya SGR; tunajenga Bwawa kubwa la umeme utakaozalisha megawatts 2115; amejenga Miundombinu ya kisasa ya Madaraja, barabara, viwanja vya ndege na amehakikisha rasilimali zetu zinatunufaisha sisi Watanzania kuliko kipindi chochote kile.

Alipoona Wakulima wanaonewa aliingilia kati bei za mazao; Amehakikisha huduma kwenye ofisi za umma zinaimarika na leo hii hakuna tena matabaka wala uonevu wa Wenye nguvu kwa Wanyonge. Tumpate wapi tena kama Dk. Magufuli?

Tulianza na Mungu, tutamaliza na Mungu. Tumpe tena Rais Magufuli miaka mitano akakamilishe miradi ya ujenzi mIkubwa aliyoianza; Kama aliweza kutufikisha uchumi wa kati kwa muda wa miaka 5 tu, hadi 2025 nchi yetu ya Tanzania itakuwa kama Ulaya mpya. Itakuwa ni miaka 5 ya fursa, maendeleo, raha zaidi na utajiri kwani misingi imara na mizuri imeshawekwa.

- Emmanuel J. Shilatu
DO MIHAMBWE

FB_IMG_1596731266427.jpeg
 
Ni Magufuli pekee ambaye kura hazitotosha. Atatumia jumuiya za chama kurudi madarakani. Jumuiya hizo ni Tume na polisi
 
Wateule wanahangaika Sana. Endelea kujipa moyo tu. Magufuli atachaguliwa na nani?
Timu Kikwete, timu Nape, timu Kinana, timu Membe, timu Makamba zote hizi ziko against huyu jamaa. Atapitaje ??
 
Jamani tuacheni msitusemee utadhani sisi hatuishi tanzania.kila mtu kwa nafasi yake atamchagua kiongoz anayemtaka sio kuanza kunielezea mazuri ya mtu fulan utadhan me siishi hapa Tanzania,
 
Wateule wanahangaika Sana. Endelea kujipa moyo tu. Magufuli atachaguliwa na nani?
Timu Kikwete, timu Nape, timu Kinana, timu Membe, timu Makamba zote hizi ziko against huyu jamaa. Atapitaje ??
Nyie ma.fa.la wa ufipa subirini tuwanyooshe
 
Wanabodi, mabibi na mabwana, salamu nyingi ziwafikie popote mlipo.

Mimi ninajua pasi na shaka kuwa mnajua hatahivyo sio vibaya kuwakumbusha kile mnachokijua kuwa ni Magufuli yuleyule.

Nchi zote duniani zina maadui. Maadui hawa wamegawanyika katika makundi mawili, maadui wa nje na wale wa ndani. Ogopa sana maadui wa ndani kwani maadui wa nje hawawezi kufanikiwa mpaka wapate ushirikiano wa maadui wa ndani.

Ninataka niwakumbushe kuwa ni Magufuli yuleyule aliyesimama kidete kuitetea Tanzania dhidi ya maadui wa nje na ndani. Alipotangaza azma yake ya kuhakikisha tatizo la umeme linabaki kuwa historia katika nchi yetu kwa kujenga bwawa la Nyerere (stiglers gorge), maadui wa nje na ndani wakainua mapembe kwa kigezo cha uharibifu wa mazingira. Ni Magufuli yuleyule aliyesimama ije mvua lije just, mradi utatekelezwa. Na kweli mradi inaendelea.

Ni Magufuli yuleyule aliyekataza makinikia yasisafirishwe nje ya nchi. Kelele zikapigwa sana. Wengine tukaifahamu MIGA. Tuliambiwa tutanyooshwa. Ni Magufuli yuleyule aliyesimama imara na kusema afe kipa afe beki, makinikia hayatoki. Leo hii tunafaidi rasilimali zetu.

Ni Magufuli yuleyule aliyesimamia kidete ujenzi wa ukuta wa merelani, leo tanzanite kubwa zaidi inapatikana Tanzania. Hivi ndivyo ilivyopaswa kuwa lakini Kenya na India walikuwa wanaongoza kwa kuuza bidhaa hiyo huku tanzanite kubwa zaidi ikiwa huko Thailand.

Wakati nchi kadhaa za Afrika zikichukua hatua Kama zilizochukuliwa na nchi za magharibi katika kupambana na janga la virusi vya korona, ni Magufuli yuleyule aliyeliongoza taifa kumlilia Mungu atuepushe na janga hilo. Maadui wa ndani na nje walitabiri maafa makubwa lakini Mungu alisikia maombi yetu.

Katikati ya kupingwa, kusemwa vibaya na kutukanwa, ni Magufuli yuleyule aliyetufikisha uchumi wa kati.

Orodha ni ndefu ila muhimu ni kujua kuwa Kama alituvusha salama miaka mitano iliyopita basi ni Magufuli yuleyule atakaye tufikisha kanani kwenye hii miaka mitano mingine.

#ni Magufuli yuleyule
 
Tunashukuru kwa mazuri hayo lakini this time tunataka mabadiriko 1 term is enough for him..... Mazuri machache kuliko mabaya
 
Umeandika kuwa tumpe miaka mingine mitano ili akakamilishe miradi mikubwa aliyoianza? Ok aliwahi kusema kuwa haoni mtu mwingine wa kuja kukamilisha miradi hiyo. Unaelewa hiyo kauli? Tunampeleka ikulu mtu anayeenda kufanyaje?
 
Back
Top Bottom