Ni dhambi kuilaumu serikali bila kushauri nini kifanyike

Hukumsikia rais akisema yeye ni rais anayejiamini. Hashaurki. Ukimshauri ni kama unamwingilia katika kazi zake na akishauriwa ndiyo kwanzaanakataa kufuata. Alisema mwenyewe kuwa alichukua fomu peke yake bila kuambiwa na mtu na hivyo asiambiwe atende nini.
 
Ni kweli tupu ulichoandika yaani nchi imekuwa kama ya wananchi wajawazito kutwa kulalama badala ya kutoa mapendekezo
 
Napenda kuwashauri Wale woote ambao wanatumia mda mrefu sana kuilamu Serikali kwa kila inachofanya, na wanafanya hivyo bila kushauri nini kifanyike ili kurekebisha kile wanachokilalamikia.
Inasikitisha watu wazima wanatumia muda mwingi kuishutumu Serikali bi hata kushauri, huko kunaitwa ni kulalamika na siyo kukosoa. Mkosoaji wa Serikali hukosoa sera, na anafanya hivyo kwa kuleta Sera mbadala, nakusema Sera iliyopo ina mapungufu moja mbili tatu, na kwa kutumia Sera hii itaweza kuziba mapengo moja mbili tatu. Sasa humu mitandaoni utawakuta watu wanalalamika tu, Rais mbabe, Demokrasia inaminywa, Makonda vyeti feki, Rais hana huruma kuna njaa, fedha ya rambirambi imeliwa, n.k. Lakini ukiwataka walalamikaji wa mambo haya wathibitishe pasipo shaka wote huishia mitini na wengine huanza kutukana. Nijuavyo mimi kwa mjibu wa vitabu vitakatifu, tabia hii ya kulaumu bila kutoa mapendekezo ilianzishwa na Lucifa (Shetani), ambaye alimpinga Mungu bila hata kutoa sababu ya kueleweka, ba kwa bahati mbaya aliungwa mkono na malaika wengine wenye mawazo finyu na yenye chuki kama Lucifa. Hivyo hatushangai hata kwenye Serikali hii ya Tano wakati Rais ambaye amepewa dhamana na Wananchi walio wengi kwamba anafaa kuwaongoza, kwa makusudi tena bila aibu mtu anajitokeza kumponda JPM pamoja na Serikali yake, na wakati huo huo bila kutoa mapendekezo kwenye hicho anachodai kuwa siyo sahihi. Hii ni tabia ya Kishetani.
Dhambi kubwa zaidi ni kuingia madarakani na mtu usijue la kufanya.
 
Itakapokuja 2020 atajua ushauri wetu ukoje hata akipiga magoti, achilia mbali push ups za kufa mtu. Hii nchi si ameifanya ya kwake peke yake ngoja muda wake ufike uone kama haya maneno yako sahihi au ni ujinga tu!
Pokea likes zangu mkuu. Tukutane 2020.
 
Napenda kuwashauri Wale woote ambao wanatumia mda mrefu sana kuilamu Serikali kwa kila inachofanya, na wanafanya hivyo bila kushauri nini kifanyike ili kurekebisha kile wanachokilalamikia.
Inasikitisha watu wazima wanatumia muda mwingi kuishutumu Serikali bi hata kushauri, huko kunaitwa ni kulalamika na siyo kukosoa. Mkosoaji wa Serikali hukosoa sera, na anafanya hivyo kwa kuleta Sera mbadala, nakusema Sera iliyopo ina mapungufu moja mbili tatu, na kwa kutumia Sera hii itaweza kuziba mapengo moja mbili tatu. Sasa humu mitandaoni utawakuta watu wanalalamika tu, Rais mbabe, Demokrasia inaminywa, Makonda vyeti feki, Rais hana huruma kuna njaa, fedha ya rambirambi imeliwa, n.k. Lakini ukiwataka walalamikaji wa mambo haya wathibitishe pasipo shaka wote huishia mitini na wengine huanza kutukana. Nijuavyo mimi kwa mjibu wa vitabu vitakatifu, tabia hii ya kulaumu bila kutoa mapendekezo ilianzishwa na Lucifa (Shetani), ambaye alimpinga Mungu bila hata kutoa sababu ya kueleweka, ba kwa bahati mbaya aliungwa mkono na malaika wengine wenye mawazo finyu na yenye chuki kama Lucifa. Hivyo hatushangai hata kwenye Serikali hii ya Tano wakati Rais ambaye amepewa dhamana na Wananchi walio wengi kwamba anafaa kuwaongoza, kwa makusudi tena bila aibu mtu anajitokeza kumponda JPM pamoja na Serikali yake, na wakati huo huo bila kutoa mapendekezo kwenye hicho anachodai kuwa siyo sahihi. Hii ni tabia ya Kishetani.
Dhambi kubwa zaidi ni Serikali kutokujua nini cha kufanya.
 
Back
Top Bottom