Ni dhambi kuilaumu serikali bila kushauri nini kifanyike

Mfano mdogo tu ni wa Bashite. Watanzania tulio wengi tumepiga kelele sana kuhusu vyeti vya huyu hasa ukitilia maanani kuna Watanzania walio wengi ambao wamefukuzwa kazi na baadhi kufunguliwa mashtaka.

Ukaja uvamizi uliofanywa na Bashite pale Clouds. Pamoja na kuwepo ushahidi chungu nzima kwa mshangao wa Watanzania wengi aliyepoteza kazi ni Nape kwa kutaka kulinda sheria za nchi lakini mvunja sheria bado yupo!

Maswala kama ya Lugumi Watanzania tukapiga kelele uchunguzi wa kina ufanywe na ripoti husika iwekwe hadharani lakini ikapotezewa na malaika mkuu hata kuitaja Lugumi tu alikuwa anaogopa.

Ikaja issue ya Wabunge wa CCM kupokea rushwa ya milioni kumi kila mmoja sawa na 2.7 billion. Tukapiga kelele uchunguzi ufanywe lakini Majaliwa na Tulia wakalipotezea!

Kwenye issue ya pesa za wahanga Watanzania tukachanga mapesa chungu nzima na nchi rafiki wakasaidia sana pia tukijua fika zile pesa ni za wahanga, lakini zile pesa zaidi ya bilioni 16 zikaporwa na kelele za Watanzania kuhusu pesa zile hazikufua dafu.

Kwenye issue ya kutumia pesa ambazo hazikuidhinishwa na Bunge tumepiga kelele sana bila mafanikio na malaika mkuu bado analidharau Bunge kwa kutumia pesa zaidi ya trilioni moja kununulia ndege na bilioni 50 kujenga kiwanja cha ndege chato kiwanja ambacho hakina watumiaji.

Na kuna mifano mingine chungu nzima ya Watanzania kushauri nini kifanywe lakini dikteta uchwara hasikii la mtoa adhana wala la mchimba kaburi.

Hivi unadhani ni kwanini Kinana kashindwa kuvumilia mpaka kuyasema haya!? Tafakari kwa kina.

Napenda kuwashauri Wale woote ambao wanatumia mda mrefu sana kuilamu Serikali kwa kila inachofanya, na wanafanya hivyo bila kushauri nini kifanyike ili kurekebisha kile wanachokilalamikia.
Inasikitisha watu wazima wanatumia muda mwingi kuishutumu Serikali bi hata kushauri, huko kunaitwa ni kulalamika na siyo kukosoa. Mkosoaji wa Serikali hukosoa sera, na anafanya hivyo kwa kuleta Sera mbadala, nakusema Sera iliyopo ina mapungufu moja mbili tatu, na kwa kutumia Sera hii itaweza kuziba mapengo moja mbili tatu. Sasa humu mitandaoni utawakuta watu wanalalamika tu, Rais mbabe, Demokrasia inaminywa, Makonda vyeti feki, Rais hana huruma kuna njaa, fedha ya rambirambi imeliwa, n.k. Lakini ukiwataka walalamikaji wa mambo haya wathibitishe pasipo shaka wote huishia mitini na wengine huanza kutukana. Nijuavyo mimi kwa mjibu wa vitabu vitakatifu, tabia hii ya kulaumu bila kutoa mapendekezo ilianzishwa na Lucifa (Shetani), ambaye alimpinga Mungu bila hata kutoa sababu ya kueleweka, ba kwa bahati mbaya aliungwa mkono na malaika wengine wenye mawazo finyu na yenye chuki kama Lucifa. Hivyo hatushangai hata kwenye Serikali hii ya Tano wakati Rais ambaye amepewa dhamana na Wananchi walio wengi kwamba anafaa kuwaongoza, kwa makusudi tena bila aibu mtu anajitokeza kumponda JPM pamoja na Serikali yake, na wakati huo huo bila kutoa mapendekezo kwenye hicho anachodai kuwa siyo sahihi. Hii ni tabia ya Kishetani.
 
Inasikitisha watu wazima wanatumia muda mwingi kuishutumu Serikali bi hata kushauri, huko kunaitwa ni kulalamika na siyo kukosoa. Mkosoaji wa Serikali hukosoa sera, na anafanya hivyo kwa kuleta Sera mbadala, nakusema Sera iliyopo ina mapungufu moja mbili tatu, na kwa kutumia Sera hii itaweza kuziba mapengo moja mbili tatu.
Kwa kukosoa tu au hata kulalamika ya kwamba hiki hakiko sawa au hili haliendi vizuri-ni haki ya kila mwananchi. Serikali sikivu huanzia hapo. Kuna issues ambazo mtu anaweza akawa na utatuzi akashauri kuna mambo mengine ni ya kitalaam na ndio maana serikali mahiri zinakuwa na wataalaamu wa mambo mbali mbali au zinauwezo wakutafuta washauri mbali mbali. Kuna mengi watu "wakawaida" wanaweza wakakuambia hayaendi vizuri au yanawaumiza na wasijue dawa yake ni nini. Hivyo si sawa kusema kila alalmikae au akosoae aje na dawa. Matatizo mengi pia huhitaji utafiti na watu wengi wa kawaida hawana mbinu za kitafiti.
Lingine tunachagua viongozi watuongoze pamoja na kutatua matatizo yetu, hawa ni wajibu wao kutafuta majibu kwa matatizo yetu. Kwa ufupi sio lazima kila mlalamikaji/mkosoaji aje na njia mbadala ya utatuzi. Na hii haijali unaongelea serikali gani.
Ukiacha hayo niliyoeleza, pia kuna serikali sio sikivu na nyingine zinajichanganya umesha sikia mimi sipangiwi cha kufanya sasa kwa mtu kama huyo utafanyaje?
KUJUA NA KUKUBALI KUNA TATIZO NI MWANZO WA KUTAFUTA UTATUZI HIVYO WATU WAKOSOE NA WENYE UWEZO WA KUTOA UTATUZI WAFANYE HIVYO NA WALE WALIOAJIRIWA/WALOCHAGULIWA ILI WAJE NA SERA STAHIKI WAFANYE KAZI YAO.
 
Nani alikwambia kuwa Bwana mkubwa anashaurika?

Si tulimsikia wenyewe majuzi pale Ubungo akisema kuwa fomu ya kugombea Urais alikwenda kuchukua yeye mwenyewe kule Dodoma na hakushauriwa na mtu yeyote na wala yeye hapangiwi la kufanya?

Kwa tafsiri nyingine ni kuwa yeye 'hatambui' kuwa alipelekwa Ikulu na kura za wananchi Bali 'anaamini' kuwa Ikulu alijipeleka yeye mwenyewe na huo utukufu ni his own property!!
 
Tumeshauri humu makada wasipewe ukurugenzi lakini tukasemwa wachochezi. H/mashauri nyingi miradi imesimama kisa migogoro ya mslahi ya kisiasa. Tumesema swala bandari ushuru upunguzwe ili meli nyingi zilete mizigo. Tulisema tangu kipindi cha Mkapa sera nzuri yenye kufaidisha wazawa iwepo kulinda migodi yetu but kalamagi na wenzio waliona bora wasaini mikataba ya Buzwagi huko ulaya ili wtz tusijue mzungu kaja kivipi. Leo tunaona jinsi hawa wawekezaji wanavyoitafuna Nchi yetu.Tushauri kipi sisi ambao tunaonekana hatuna faida ndani ya Nchi hii. Labda tuiombee serikali japo iwe na huruma kwa maskini tunaoteseka na ukoloni huu wa njia ya uwekezaji.
 
Napenda kuwashauri Wale woote ambao wanatumia mda mrefu sana kuilamu Serikali kwa kila inachofanya, na wanafanya hivyo bila kushauri nini kifanyike ili kurekebisha kile wanachokilalamikia.
Inasikitisha watu wazima wanatumia muda mwingi kuishutumu Serikali bi hata kushauri, huko kunaitwa ni kulalamika na siyo kukosoa. Mkosoaji wa Serikali hukosoa sera, na anafanya hivyo kwa kuleta Sera mbadala, nakusema Sera iliyopo ina mapungufu moja mbili tatu, na kwa kutumia Sera hii itaweza kuziba mapengo moja mbili tatu. Sasa humu mitandaoni utawakuta watu wanalalamika tu, Rais mbabe, Demokrasia inaminywa, Makonda vyeti feki, Rais hana huruma kuna njaa, fedha ya rambirambi imeliwa, n.k. Lakini ukiwataka walalamikaji wa mambo haya wathibitishe pasipo shaka wote huishia mitini na wengine huanza kutukana. Nijuavyo mimi kwa mjibu wa vitabu vitakatifu, tabia hii ya kulaumu bila kutoa mapendekezo ilianzishwa na Lucifa (Shetani), ambaye alimpinga Mungu bila hata kutoa sababu ya kueleweka, ba kwa bahati mbaya aliungwa mkono na malaika wengine wenye mawazo finyu na yenye chuki kama Lucifa. Hivyo hatushangai hata kwenye Serikali hii ya Tano wakati Rais ambaye amepewa dhamana na Wananchi walio wengi kwamba anafaa kuwaongoza, kwa makusudi tena bila aibu mtu anajitokeza kumponda JPM pamoja na Serikali yake, na wakati huo huo bila kutoa mapendekezo kwenye hicho anachodai kuwa siyo sahihi. Hii ni tabia ya Kishetani.

Nadhani ili ushauriwe inabidi ujenge mazingira ya kushaurika. Bahati mbaya sana Rais wetu mpendwa sijui kitu gani kimemkumba toka day one hakuonyesha wa kushaurika.
Nililiona hili pindi tu alivyotangazwa mshindi wa kiti cha urais, kwa maneno aliyoyasema pale lumumba ambayo yote yalikuwa ya umimi na tukampigia makofi kama ilivyo ada.
Ukishatanguliza umimi unaziba nafasi ya watu kukushauri, hivyo utaishia kuona kila akwambiaye ukweli anakulaumu.
Rais anasema maendeleo hayana chama, namshauri amtumie Tundu Lissu, huyu ndiye msemakweli na si yeye kama anavyojinasibu, na ni hazina kubwa sana ya taifa katika masuala yanayohusu haki na sheria ambazo nyingi hukandamiza masikini, this guy ametufungua macho sana sisi masikini this time.
 
Serikali hii inaongoza kwa kupata ushauri lakini pia inaongoza kwa kupuuza ushauri. 'mifano iko mingi, ila mtu shupavu wa shingo atazidi kusema toa mifano. Sijui anataka kuikariri hiyo mifano akajibie paper wapi?
 
Itakuaje sisi tuwashauri wakati wanao washauri waliowaajiri na ikifika mwisho wa mwezi wanachukua mamilioni?
Sisi kazi yetu ni criticise, wao wakae na washauri wao wajue nini la kufanya
tena wenye sifa na wanao lipwa kwa kodi zetu
 
We mleta mada toa upumbav humu ndan tuache wenyewe tulalamike tutapike nyongo sio kutuletea ngonjera kama wewe ni nyumba ndogo ya baba bashite hebu jarib mumshauri huyu jamaa hivi unaakili au nawe ni walewale? Kama mshauriwa katoa rai hadharan kuwa yeye ndie anaeamua na hapangiwi na mtu wewe utafanya nini? Mbona Mafuru mtaalam wa uchumi na fedha tena amefanya kazi kwenye mashirika makubwa na ya kimataifa ya fedha alipomshauri huyo mzee kuhusu madhara ya kuficha au kuzuia pesa BOT kutaleta mzunguko finyu wa fedha aliishia kutumbuliwa tena akaambiwa anatetea wezi sasa nani atakaetoa ushaur kwa huyu jamaa hebu tazama hata first lady ktk taifa hili anashindwa hata kujitokeza hadharani unategemea kuna ushaur utapokelewa huko?
 
Napenda kuwashauri Wale woote ambao wanatumia mda mrefu sana kuilamu Serikali kwa kila inachofanya, na wanafanya hivyo bila kushauri nini kifanyike ili kurekebisha kile wanachokilalamikia.
Inasikitisha watu wazima wanatumia muda mwingi kuishutumu Serikali bi hata kushauri, huko kunaitwa ni kulalamika na siyo kukosoa. Mkosoaji wa Serikali hukosoa sera, na anafanya hivyo kwa kuleta Sera mbadala, nakusema Sera iliyopo ina mapungufu moja mbili tatu, na kwa kutumia Sera hii itaweza kuziba mapengo moja mbili tatu. Sasa humu mitandaoni utawakuta watu wanalalamika tu, Rais mbabe, Demokrasia inaminywa, Makonda vyeti feki, Rais hana huruma kuna njaa, fedha ya rambirambi imeliwa, n.k. Lakini ukiwataka walalamikaji wa mambo haya wathibitishe pasipo shaka wote huishia mitini na wengine huanza kutukana. Nijuavyo mimi kwa mjibu wa vitabu vitakatifu, tabia hii ya kulaumu bila kutoa mapendekezo ilianzishwa na Lucifa (Shetani), ambaye alimpinga Mungu bila hata kutoa sababu ya kueleweka, ba kwa bahati mbaya aliungwa mkono na malaika wengine wenye mawazo finyu na yenye chuki kama Lucifa. Hivyo hatushangai hata kwenye Serikali hii ya Tano wakati Rais ambaye amepewa dhamana na Wananchi walio wengi kwamba anafaa kuwaongoza, kwa makusudi tena bila aibu mtu anajitokeza kumponda JPM pamoja na Serikali yake, na wakati huo huo bila kutoa mapendekezo kwenye hicho anachodai kuwa siyo sahihi. Hii ni tabia ya Kishetani.

Hapendi kushauriwa....Na ukimuambia cha kufanya ndio unaharibu kabisa....
 
Wataalamu wa uchumi walishaamua kumuachia Mzee Haambiliki gurudumu hasa baada ya kuanza kuwatumbua badala ya kuwasikiliza. Kama alivyofanya kwa Mafuru.
 
Naona imekupendeza kuniita mnafiki, siyo mbaya wala sishangai, hoja hapa toa mifano ya ushauri iliokataliwa, eleza aliyeshauri na wapi na lini na alisema nini juu ya kitu gani? Na majibu ya upande wa serikali yalitolewa na nani ma wapi ili tuweze kufuatilia. Siyo kuibuka na matusi na kejeli dhidi ya Watanzania wenzako, sote tunaheshima sawa mbele ya Katiba.
Unabahati unaongea kwenye media hk kwetu kwa ujinga ulio post nina uhakika ungekuwa umefanyiwa lolote huenda saiz yangekuwa mengine be careful sn km unacho usidhan everybody anacho
 
Kilwangu huyuu jamaa namuona km sio mtanzania au anatafta Kiki ili JF ifungiwe yakuongea yapo mengi mm nimefungwa mdomo kilicho mtokea Nape kila mtu ameshuhudia
 
Umerogwa mtoa mada.upuuzi tuh umeandika.
 
Naona imekupendeza kuniita mnafiki, siyo mbaya wala sishangai, hoja hapa toa mifano ya ushauri iliokataliwa, eleza aliyeshauri na wapi na lini na alisema nini juu ya kitu gani? Na majibu ya upande wa serikali yalitolewa na nani ma wapi ili tuweze kufuatilia. Siyo kuibuka na matusi na kejeli dhidi ya Watanzania wenzako, sote tunaheshima sawa mbele ya Katiba.
Kwa uelewa wako kupitia majibu na hoja zako, sidhan kama nina haja ya kuichosha akili yangu kutoa ufafanuzi juu ya hayo unayo hitaji, maana hata ukipewa ufafanuzi si rahisi kuuelewa, maana kama wewe ni mtanzania na nimfuatiliaji mzuri wa mwenendo wa serikali ya tanzania wala usinge thubutu kuuliza maswali yenye hoja ambazo naziona ni za kitoto namna hiyo maana kila linalo jiri liko wazi, watoa ushauri walio ishauri serikali ni wengi na ushauri wao umedharauliwa tena kwa kejeli sasa nani ashauri zaidi? ya nini kujichosha kushauri kisicho shaurika?? ,

mnafiki yeyote hupenda kuyasikia yaufurahishayo moyo wake na hupenda kuugeuza ukweli kuwa uongo nanuongo kuwa ukweli, hufumbia macho yale yasiyo faa na kufanya kana kwamba hayapo , hupenda kutukuza na kusifu kila jambo liwe kheri ama shari , mnafiki ni mtu mbaya sana na ndiye anaye zid kuliingiza gizan taifa hili yote uliyo jifanya unataka kujibiwa hapo juu una majibu yake vyema kabisa lakin unafiki ndio unao kitafuna .
 
Napenda kuwashauri Wale woote ambao wanatumia mda mrefu sana kuilamu Serikali kwa kila inachofanya, na wanafanya hivyo bila kushauri nini kifanyike ili kurekebisha kile wanachokilalamikia.
Inasikitisha watu wazima wanatumia muda mwingi kuishutumu Serikali bi hata kushauri, huko kunaitwa ni kulalamika na siyo kukosoa. Mkosoaji wa Serikali hukosoa sera, na anafanya hivyo kwa kuleta Sera mbadala, nakusema Sera iliyopo ina mapungufu moja mbili tatu, na kwa kutumia Sera hii itaweza kuziba mapengo moja mbili tatu. Sasa humu mitandaoni utawakuta watu wanalalamika tu, Rais mbabe, Demokrasia inaminywa, Makonda vyeti feki, Rais hana huruma kuna njaa, fedha ya rambirambi imeliwa, n.k. Lakini ukiwataka walalamikaji wa mambo haya wathibitishe pasipo shaka wote huishia mitini na wengine huanza kutukana. Nijuavyo mimi kwa mjibu wa vitabu vitakatifu, tabia hii ya kulaumu bila kutoa mapendekezo ilianzishwa na Lucifa (Shetani), ambaye alimpinga Mungu bila hata kutoa sababu ya kueleweka, ba kwa bahati mbaya aliungwa mkono na malaika wengine wenye mawazo finyu na yenye chuki kama Lucifa. Hivyo hatushangai hata kwenye Serikali hii ya Tano wakati Rais ambaye amepewa dhamana na Wananchi walio wengi kwamba anafaa kuwaongoza, kwa makusudi tena bila aibu mtu anajitokeza kumponda JPM pamoja na Serikali yake, na wakati huo huo bila kutoa mapendekezo kwenye hicho anachodai kuwa siyo sahihi. Hii ni tabia ya Kishetani.
Alisema HAPANGIWI
HASHAURIKI
 
Back
Top Bottom