Makusudically
JF-Expert Member
- Feb 3, 2014
- 2,203
- 1,235
Napenda kuwashauri Wale woote ambao wanatumia mda mrefu sana kuilamu Serikali kwa kila inachofanya, na wanafanya hivyo bila kushauri nini kifanyike ili kurekebisha kile wanachokilalamikia.
Inasikitisha watu wazima wanatumia muda mwingi kuishutumu Serikali bi hata kushauri, huko kunaitwa ni kulalamika na siyo kukosoa. Mkosoaji wa Serikali hukosoa sera, na anafanya hivyo kwa kuleta Sera mbadala, nakusema Sera iliyopo ina mapungufu moja mbili tatu, na kwa kutumia Sera hii itaweza kuziba mapengo moja mbili tatu. Sasa humu mitandaoni utawakuta watu wanalalamika tu, Rais mbabe, Demokrasia inaminywa, Makonda vyeti feki, Rais hana huruma kuna njaa, fedha ya rambirambi imeliwa, n.k. Lakini ukiwataka walalamikaji wa mambo haya wathibitishe pasipo shaka wote huishia mitini na wengine huanza kutukana. Nijuavyo mimi kwa mjibu wa vitabu vitakatifu, tabia hii ya kulaumu bila kutoa mapendekezo ilianzishwa na Lucifa (Shetani), ambaye alimpinga Mungu bila hata kutoa sababu ya kueleweka, ba kwa bahati mbaya aliungwa mkono na malaika wengine wenye mawazo finyu na yenye chuki kama Lucifa. Hivyo hatushangai hata kwenye Serikali hii ya Tano wakati Rais ambaye amepewa dhamana na Wananchi walio wengi kwamba anafaa kuwaongoza, kwa makusudi tena bila aibu mtu anajitokeza kumponda JPM pamoja na Serikali yake, na wakati huo huo bila kutoa mapendekezo kwenye hicho anachodai kuwa siyo sahihi. Hii ni tabia ya Kishetani.