Ni club ngapi za soka bongo ziko na website?

shumanice

Member
Jul 21, 2011
64
25
Wadau habari za leo. Nilikuwa na jaribu kuangalia website za timu mbali mbali hapa bongo lakini cha ajabu nimekuta vilabu vyetu vingi havina website. Sasa nikawa najiuliza viongozi wa hizi timu wanajua umuhimu wa kuwa na website au hawajui? Na je huwa wanafuatilia habari za timu nyingine kama vile za ulaya kuona wenzao wanaendeshaje timu?

Kwa karne ya sasa habari nyingi za vilabu hujulikana kwa njia ya mtandao, mimi ninaamini kuwa kila timu inahabari nyingi sana za kuandika kwenye kurasa za internet. Nawapongeza viongozi wa Azam FC kwa kuliona hili ningependa kuona viongozi wengine wa vilabu vyetu wakiiga mfano huu.

Leo kocha yeyote akitaka kufuatilia habari za mchezaji yeyote hutumia njia ya mtandao, tunataka kuuza wachezaji wetu nje lakini habari zao hazipo!!! Je tutafuka namna hii???
 
hawa waliofungwa juzi na polisi dom?
Ni wale ambao waliwapiga Simba 1-0, wale walioanzisha jina wakaishia na SC Simba wakaiga, wakaanzisha gazeti, Simba wakaiga, wakafungua website, Simba wakaiga pia. Hivi Simba wao ni kuiga tu? Mmetuchosha nanyi vumbueni bwana, wala sio lazima mvumbue lindege!
 
dah huyu mtu sikumsikia sikunyingi saaaaana
aahaa jamaa yupo tu mission town mara ya mwisho nmekutana nae kwenye daladala mbagala - posta anabshana mambo ya simba na yanga kwnye gari.
 
Back
Top Bottom