tandabui2021
JF-Expert Member
- Nov 5, 2021
- 3,120
- 5,362
Kulala njaa siku tatu ,nne ,tano,kushindia uji na maji
Ingenifanya niwe sawa na yeye tu.Ulitakiwa umwambie kwanini bado upo duniani.
Ni mipango tu imekosewa na kizazi chake kilichotangulia, kitu chochote kikikosa msingi mzuri kitabomoka au kuyumba mbele ya safari hata kwa dhoruba kidogo, hao wazee unaosema awapelekee utakuta hawakuwa na uchungu wa kulinda ukoo wao katika swala la uchumi ili mbele ya safari ukoo uwe wenye kubarikiwa Sasa akijipendekeza kupeleka hicho Cha shida anachopata ndo kwanza wanaweza kumtumbikiza shimboni kwa wivu, watu wanaojua maana ya kulinda jina la familia wazee huwa wanahakikisha wanajenga msingi kwaajili ya kizazi Cha mbele na hata jina la familia linalundwa sana hata mwanafamilia akikwama hawezi kuyumba sana kimaisha maana anakuwa na msingi mzuri na wale walioharibika tabia unakuta ukoo unawawajibisha ili walinde kizazi kizuri na jina la ukoo, Sasa huyu anatakiwa arudi Kijijini kupata sapoti ya wazee ili ainuke Tena na siyo kuwapa asichonacho.Rudi bush angalia mila zenu zipo sawa, kuna kaela huwa unatakiwa kuwapa wazee wako katika kipato chako cha kwanza chochote kile pita kwa shangazi wape chochote, ukiona bado, chungulia kwa babu shida ipo wapi,
SIAMINI KAMA MUNGU AMEUMBA MWANADAMU APATE SHIDA, shida zote huwa tunazikwaa hapahapa duniani.
Hujasoma watu wametafuta vibarua wakakosa,unaweza kukosa hata kazi ya kuzoa taka ,we usidharu wanao sema yaliwakuta .Dah
Mi najua mtu asie chagua kazi halali njaa
Wewe jamaa!Muwa paipu au muwa gani?
Kamwe do not entertain kumwaga chakula ndani kwako, hakikisha chakula kinapikwa cha kutosha watu kushiba vizuri lakini kisiwe kinamwagwa. Kosa/dhambi kubwa sana hii kumwagamwaga vyakula.Leo namwona beki tatu kamwaga ugali
Hii kitu ni kweliNa Daima shida zinakujaga kwenye hali hii ya mke na mtoto mdogo. Ile kauli ya SINA HATA MIA ukisikia mtu anasema unaweza sema ana utani.
saleni, hukupata tena dili jingine la pharmacy?Wanawake wengine wajanja, wakiona Maisha magumu, wanazoea nyumba zenye unafuu ukifika pale unasaidia kazikazi, wakipika chakula unakula na mtoto, kama kunachochote kitu unapewa unaondoka jioni, mi nimewakuta Sana home watu wa dizaini hii.
daah aiseee...umenikumbusha mbali. nilikopa godoro nikailaza chini sikuwa na kitanda akaniongezea na stuli ya kukalia alafu nikaoa siku 15 mbele wakati wa jion wife anasonga ugali jamaa anapiga hodi karibu mara paap nataka pesa ya godoro na ya stuli mbele ya wife daah nikamuomba aniongezee siku 15 inafika asubuhi napiga mswaki kurudi ndani nikakuta wife kabeba vitu vyake kampelekea daah
Mzee anajikaushaa kama vile hakukutendea ubayaaa...!!Hii comment yako imenikumbusha mbali sana.
Kipindi cha mapito magumu nilikutana na ndugu kabisa wa mzee wangu. Nikamwambia hali halisi ya maisha.
Yule mzee alinijibu unakosaje hata mlo mmoja, huoni unajaza dunia tu si bora ungekufa na baba yako tu.
Hii kauli iliniliza kama mtoto mdogo.
Ila Mungu si wa mmoja, hivi karibuni tu kulipitishwa mchango wa kifamilia, mzee kashikwa na tezi dume analia kama mtoto. Watoto wake hakuna hata mmoja mwenye muelekeo.
Nilistopisha ule mchango na nikasimamia operation yake mpaka kutoka kwake hospitali.
Yule mzee anajifanya kasahau kila kitu ila najua nafsi yake inamsuta kila akiniona.