Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
- Thread starter
- #61
Nakushukuru kwa mchango wako mkuu, kila wazo na maoni ya wadau wa siasa tunayachukua, na hili nimelichukua.... Shukrani sana.Ujinga ni kujifariji kwa matumaini hewa. Nasema haya kama mtu ninayeamini kwa dhati umuhimu wa Chadema na vyama vingine vya upinzani. Lakini kutamani kuwa na upinzani ni kitu kimoja. Kuwa na upinzani usio na mwelekeo ni kitu kingine. Kuwa na upinzani wenye mwelekeo lakini unakandamizwa pia ni kitu kingine. Na kuwa na upinzani wenye mwelekeo lakini unakandamizwa lakini wanaokandamizwa wanategemea miujiza au kujihadaa kuwa "chama hakifi" sidhani kama ni wazo la busara.
Katika makala yako ndefu hakuna sehemu yoyote ya kumpa matumaini "mtu asiyejua kinachoendelea ndani ya Chadema" kuwa who is next kwenye hiyo hama hama. Lakini kibaya zaidi, hakuna anayejua nani wa kumwamini.
Adui mkubwa kabisa wa Chadema kwa wakati huu ni huko kujipa matumaini hewa. Hii hama hama sio tu inapunguza idadi ya wabunge na madiwani wenu bali pia ina athari za kisaikolojia kwa wafuasi wenu. Sintoshangaa kuona kampeni za Chadema katika uchaguzi mkuu wa 2020 zikizorota kulinganisha na 2015 au 2010 kwa sababu kuna kuvunjika moyo miongoni mwa wafuasi wa chama chenu japo ninyi makada mkiambiwa hayo mnakuwa wakali kama pili pili.
Uhai wa Chadema unategemea pia mechanisms za ndani ya chama hicho kuwa hai. Sio kila kifo husababishwa na kitu cha nje. Chadema ina tatizo kuhusu demokrasia japo jina la chama ni cha DEMOKRASIA na Maendeleo." Mnaweza kukwepa hoja ya uchaguzi mkuu, mnaweza kujidanganya kuwa "kwani Nyerere aliongoza CCM miaka mingapi" lakini athari zake mtaziona huko mbeleni.
Kuna tuhuma alizotoa Waitara kuhusu viti maalum. Wako wapi hao wakinamama waliozawadiwa viti maalum zaidi ya kuwaona baadhi yao huko insta wakiuza sura?
Badala ya makada kama wewe Yericko, Malisa, na wengineo "kuuweka mtu-kati" uongozi wa chama chenu na kusiaitiza haja ya kuthamini foot soldiers mnaohangaikia chama chenu mtaani na mtandaoni, mpo bize kujihadaa kuwa "ni ujinga kudhani Chadema itakufa."
By the way, kufa kwa chama cha siasa sio lazima kumaanishe imezikwa kaburini. Kunaweza kutokea kwa namna ya KANU huko Kenya au hata NCCR-Mageuzi (ya Mrema 1995 vs ya leo).
Mnachopaswa kuhangaikia muda huu ni kuwaondoa mamluki waliojazana kwenye chama chenu kabla hawajafanikisha madhara makubwa zaidi.
Na kosa mlilofanya 2015 kumpokea "Lowassa na watu wake" litawagharimu mno maana kuna idadi kubwa tu ya watu waliokuja na Lowassa ambao wapo kwenu kimwili lakini kiroho wapo CCM.
Mwisho, ushauri wangu muhimu kabisa kwenu ni hii: DO NOT EVER DARE TO UNDERESTIMATE DHAMIRA YA JIWE KUUA UPINZANI. Mkidhani kuwa "ah hawezi huyu" mtarudia kusoma bandiko hili kwa majonzi baada ya election ya 2020. Kwa taarifa tu, dhamira ya Jiwe ni kuhakikisha Chadema haipati mbunge hata mmoja kwenye uchaguzi huo. Hilo linatekelezwa kwa njia kuu mbili: Moja, hawa wanaonunuliwa (kuna watano hivi - wawili kutoka mkoa mmoja - ninaofahamu kuwa wapo njiani kuelekea CCM). Mbili, hujuma zinazoendelea ndani ya vyama hivyo ambazo zitashika kasi zaidi mwakani na ambazo zinaratibiwa na CCM na kitengo na lundo la mamluki lililomo ndani ya CDM.
Matarajio ya Jiwe ni kwamba laiti Chadema ikishindwa kupata mbunge hata mmoja katika uchaguzi mkuu huo basi itaelekea ICU kuanza safari ya kifo cha taratibu.
Badala ya kutuambia "Chadema haitokufa" basi angalau mtupe moyo kuwa "wale wasaliti wote wa kuhama Chadema kwenda CCM wamekwisha, tumebaki tunaokipenda chama kwa dhati." Can you do that?