Ni binadamu mjinga tu ndie atainua kinywa na kusema CHADEMA inakufa

Kuhangaika kununua watu si kuhangaika?. Kweli we BWAKILA
Suala la watu kuhama chama ni haki na ni kitendo cha kidemokrasia. Ni demokrsia gani ninyi mnaipigania? Je Lowassa alipohamia CDM na kupewa kile anachotaka licha ya hao hao CDM kumsema kwa makando kando mengi aliwalipa kiasi gani? Vp kuhusu Kuhama kwa Makongolo Mahanga mlimlipa sh ngapi, Lembel je? Nyalandu? Rwakatare? Paulina Gekul, Ruth Molel, Masha, taja kwanza bei mliowanunulia ndo useme mmewauza kwa kiasi fulani!
 
slaa alipata kura milioni 2,lowasa alipata kura milioni 6
umeshajua hapo nani asset nani liability
Lowasa alisimama kwa tiketi ya CDM chini ya sapoti ya vyama vingi wakati Slaa alisimama kwa tiketi ya CDM pekee. Hapa hutanijibu cha maana zaidi ya kubashiri tu kwamba hata angepata hiyo nafasi ya kuwakilisha vyama vingi asingefikisha hiyo idadi ya kura
 
kwa uzoefu tu vile vyama vimechangia kura ngapi hapo?
angesimamishwa slaa hata kura milioni tatu zisingefika
yule mzee hakuwa na jipya,nilikuwa namfatilia sana
jukwaani alikuwa anaongea mambo yaleyale
kumbuka pia waislam walikuwa hawamkubali huyu kutokana na background yake ya upadri
alikuwa ni liability
 
Kujifariji kijinga kijinga hakuwezi kumaliza matatizo yaliyoko CDM pambaneni na maboriti katika malango yenu kabla ya vibanz vya jirani.
Mtajifariji, mtachekwa na mtaendelea kupata tabu sana!
Punguza kutoa ushuzi....bichwa taka tupu
 
After all, CHADEMA sio Mbowe sio Heche, CHADEMA ni "Ideology" hivyo inaishi kwa watu na sio wanasiasa wanoongoza hii "Dhana" pekee, hawa kazi yao ni kuonesha trend, wakifa hao watakimbiza wengine
 
Hofu yangu kubwa ni kuwa watu wa CCM, Wanafurahi hawa watu kuja na kuingia kwenye chama chao na kuwapa madaraka, yaani kuwaingiza kwenye system.

na wakiwa wanondoka wanaita press na kutoa hoja nyepesi sana..

so how sure, hawa watu wamekuja ku spy chama chao (CCM) na baadae kusikia bada ya muda wamerudi zizin??..

nimependa YERICKO, Ulivyosema mabadiliko ya Technolojia na Ulinzi vimeimarika ndani ya CDM, Hapo kiukweli umewaondolea hofu wana CDM..

Hofu yangu, nisije kuona MBOWE anadhoofu kama tulivyoona kwa Mrema, Maalimu, Lowasa, mwenyekt wa UDP, Na wengine..

coz sumu wanazotumia kufanya assenation ndio zile zile, hazina tofaut kwa mtu A, B, C n.k maana nahofu kuwa Ccm, wanaenda taratibu sana kulingana na mabadiliko ya tech, ndio maana kuana sehemu ya kutumia akili wao wanatumia nguvu
 
Uhuru w
Uhuru wa kutoa maoni....dhana ya demokrasia haitazamwi kwenye tafsir.
Kwa hiyo uhuru wa kutoa maoni unamilikiwa na upinzani? Maoni ya tofauti na hayo yanatukanwa? Ukishindwa kuheshimu mawazo ya watu wengine wakati huu nini tofauti yako na hao unaowalalamikia?
 
Kwamuda wa miezi kadhaa nimezunguka kukijenga chama changu cha Chadema, mimi kama mwanachama mtiifu na mtaalamu mtafiti wa siasa na mambo mengine ya kijamii, naweza kueleza machache juu ya hali ya sissa nchini.

Tulifika sehemu nyingi katika vikao vya ndani tukiwa tumetaraji kukutana na wajumbe wa Chadema wa mkutano mkuu ngazi ya wilaya, kimsingi kwamuundo wa Chadema ngazi ya wilaya inatakiwa angakau wasizidi wajumbe miambili hili hili linategemea idadi ya kata katika wilaya husika, lakini kote tulikopita, tulikuwa tunakaribishwa na wanachama/wajumbe zaidi ya elfu mbili kila mkutano, na wote hawa wanakula yamini yaani viapo kwamba Chadema ndio jawabu la maisha yako yaliyotopea kwa umasikini na ugumu wa maisha yao.

Hapo ndipo nikatambua na kuja na tafakuri yangu kwamba, siasa za Afrika zinafanana kwa kiwango fulani hasa kwenye hulka za watawala na watawaliwa huku machipuzi ya demokrasia yakichelewa kustawi huku wimbi la kupembuka kwa watawaliwa likishika kasi.

Kwa upande wa siasa za Tanzania nikuwa zinabeba sura tatu zote zenye asili ya Afrika, Ghiliba ni sehemu ya siasa za Afrika, mauaji ni sehemu ya siasa za Afrika, Kung'ang'ania madaraka ni sehemu ya siasa za Afrika,

Siasa za upinzani nchini Tanzania zimepita kwenye kipindi kigumu sana tangu kuingia kwa mfumo wa vyama vingi nchini, nitaangazia kwa kifupi mapito ya vyama vya siasa tangu mwaka 1995 mpaka leo tunakwenda 2020 na huko tuendako,

NCCR ya Mrema ilipitia kipindi kigumu sana hasa baada ya ule uchaguzi uliotikisa chama tawala na kuamua kuiundia mkakati rasmi wa kuiangamiza, ni kipindi ambacho nchi ilikuwa imetoka kwenye mfumo wa chama kushika hatamu,

System ilipewa majukumu kamili ya kuhakikisha wanaizima kabisa NCCR na moja ya kituko cha kuvutia ni kujazana kwa majasusi ndani ya chama hicho mpaka kufikia mshika mikoba halisi wa Mrema alikuwa nyoka (Maswi).

Lakini licha ya CCM kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kumdhibiti Mrema, jambo lingine lililomdhoofisha ni serikali kudhibiti uchumi wake.

2000 Aina hii ya udhibiti wa upinzani ilitumika japo si kwakiwango kikubwa hasa kutokana na aina ya siasa za CUF pale Zanzibar, lakini bado system iliendelea kutumika kwa kila njia kuvuruga mission za CUF, na mwisho wamefanikiwa kuwanasa Mwenyekiti Lipumba na Naibu Katibu Mkuu Bara bwana Julius Mtatiro.

Kuingia madarakani kwa Mbowe na safu yake kwenye siasa za CHADEMA kulibadili sura halisi ya siasa na kufanya ccm ibadili kila kukicha mbinu ya kukabiliana na CHADEMA.

Mbinu yakutumia System kudhoofisha CHADEMA ilianza kufeli zaidi baada ya CHADEMA kubadili mbinu na kuunda mfumo stahiki wa ulinzi wa Chama na hasa ujio wa mageuzi ya kiteknolojia na mwitikio wa vijana katika siasa mpya miaka ya 2O1O hadi miaka 2O15 hivi.

Baada ya kufeli watawala wakaja na mbinu ya kudhoofisha viongozi kiuchumi, hapo ndipo nguvu ya Mbowe ilipodhihirika, Mbowe anayekadiriwa kuwa na utajiri wakuzaliwa wa thamani ya 850b-1.2tr amekuwa kisiki kikuu kwa CCM kuvunja upinzani, licha ya serikali ya Magufuli kupora na kuvuruga miradi mikubwa ya Mbowe iliyokuwa imeajiri maelefu ya watu, bado Mbowe ni yuleyule wa jana leo na kesho, zaidi tu ccm na vibaraka wake wamewaumiza maelfu waliokuwa wameajiriwa katika miradi na biashara za Mbowe huku serikali ikijikosesha kodi tu.

CCM ilibadili mbinu na kurejea mbinu zake za kale zilizofeli za kununua wapinzani kama Mrema (TLP), Cheyo (UDP), Mtikila (DP) nk. Hawa CCM imefanikiwa kuwaweka mfukoni rasmi, wanapumua kwa gharama ya ccm, yani CCM inamaamuzi makubwa juu yao kisiasa na kiuchumi.

Uwezo binafsi wa kiuchumi, kimtazamo na kifikra wa Mbowe, Uwezo wa kifikra na kimsimamo wa timu yake ya uongozi vimekuwa gharika kwa ccm na kuifanya itumie mabilioni ya pesa kununua viongozi wa ngazi ya chini kama sehemu ya kuibomoa CHADEMA. Jambo ambalo sisi wataalamu wa siasa tunalitazama kwamba ni mradi wa uhalifu unaoteketeza kodi za umma badala ya kuisaidia ccm.

Nasema hivyo kwakuwa katika mradi huu hakuna mwanachama au mpiga kura anayehama isipokuwa ni diwani au mbunge tu aliyenunuliwa ndie anahama na pengine hata familia zao zinawakatalia kuhama. Vyama vya siasa vya kileo vinatakiwa kuongozwa na watu wenye financial stable, bila hivyo chadema ingeshakuwa kama UDP, Cuf nk.

Umma unahitaji mabadiliko, unahitaji kubadilisha chama na viongozi wote waliochini ya ccm, Chadema licha ya sera na itikadi yake nzuri, Uhai wake unajengwa zaidi na hasira za umma dhidi ccm na serikali. Iwe kwa matendo mauvu ya ccm au mazuri ya ccm, bali binadamu kwaasili huhitaji mabadiliko, ukifika muda wa mabadiliko binadamu hazuiliki na haambiliki, hivyo ndivyo Watanzania wanavyotaka, hakuna cha ccm asili wala ccm ya wahamiaji iitwayo ccm mpya.

Kwa tafsiri hiyo, Hivyo Chadema haiwezi kufa, labda kipatikane chama mbadala wa ccm zaidi ya Chadema ambapo kwa hakika hakipo, Umma uko upo tayari kufa na Chadema kwakuwa umechoka na kufedheheshwa na ccm na hauko tayari kugeukia ccm.

Ili Chadema ife, ni lazima kiwepo chama mbadala ambacho kinakonga vilivyo nyoyo za umma kwa kuikabili ccm na serikali yake vilivyo zaidi ya Chadema, na sio vilivyo kama Cuf, TLp, nk ambavyo ni vibaraka vya ccm na umma unajua fika. Ukitazama dhamira na maneno ya Mwenyekiti wa ccm Magufuli anasema moja ya ahadi zake ni kuua upinzani, hili anajidanganya au kudanganya wanachama wake, na zaidi ni kujivika bomu. Wataalamu wa siasa wa ccm wanaekelewa umuhimu wa vyama pinzania, na wale waliohudumu kipindi cha Nyerere wanajua kwanini siasa za vyama vingi zilikubaliwa haraka. Nyerere hakuwa mjinga.

Na Yericko Nyerere

View attachment 833416View attachment 833416
Mwanzo mpaka mwisho sijaona nafasi ya Lowasa! kwa lugha nyingine ameshakuwa Liability.

Samaki wakubwa huwala wadogo katikati ya wimbi la viongozi wakubwa kuhama ni vigumu sana kuwaona wasiojulikana/wanachama wa kawaida wakihama utaona 2020 au 2019.

Mpaka mtu anakuwa kiongozi kihalali means anaushawishi mkubwa na niamini mimi mtu Kama mtatiro amehama na ushawishi wake japo hauwezi kuwa 100% but upo hicho ndicho kinakuja kuumiza vyama vya upinzani baadae.

Ccm ya leo haina mwenyewe zaidi ya mwenyekiti hata polepole analijua hilo unaweza shangaa unaamka asubuhi polepole katumbuliwa hii inawaandaa kisaikolojia wanachama wote wa ccm kutegemea lolote muda wowote hakutakuwa na ugomvi mkubwa wa nafasi kama mwanzo/ilivyozoeleka ndani ya ccm.

Cdm isipochukua hatua mahususi inaweza kufa japo sio leo but naamini baada ya 2020 hali itakuwa mbaya sana kwa sasa jpm anaogopa kisiki cha 2020 akikivuka/na sina shaka atavuka kama ccm wenyewe hawataamua kumuondoa ndipo mtaiona rangi yake halisi naamini hamjaiona hata nusu ya jpm.

Niamini mimi msipojitathimini cdm itakufa na pengine act ikashika nafasi ya cdm tuombe uzima.
 
We Yeri ko ukipewa laki mbili unahama chama...halafu acha uongo Mbowe hana utajiri huo haha eti bilion 850...angekuwa nazo hizo asingekula ruzuku
 
Kwamuda wa miezi kadhaa nimezunguka kukijenga chama changu cha Chadema, mimi kama mwanachama mtiifu na mtaalamu mtafiti wa siasa na mambo mengine ya kijamii, naweza kueleza machache juu ya hali ya sissa nchini.

Tulifika sehemu nyingi katika vikao vya ndani tukiwa tumetaraji kukutana na wajumbe wa Chadema wa mkutano mkuu ngazi ya wilaya, kimsingi kwamuundo wa Chadema ngazi ya wilaya inatakiwa angakau wasizidi wajumbe miambili hili hili linategemea idadi ya kata katika wilaya husika, lakini kote tulikopita, tulikuwa tunakaribishwa na wanachama/wajumbe zaidi ya elfu mbili kila mkutano, na wote hawa wanakula yamini yaani viapo kwamba Chadema ndio jawabu la maisha yako yaliyotopea kwa umasikini na ugumu wa maisha yao.

Hapo ndipo nikatambua na kuja na tafakuri yangu kwamba, siasa za Afrika zinafanana kwa kiwango fulani hasa kwenye hulka za watawala na watawaliwa huku machipuzi ya demokrasia yakichelewa kustawi huku wimbi la kupembuka kwa watawaliwa likishika kasi.

Kwa upande wa siasa za Tanzania nikuwa zinabeba sura tatu zote zenye asili ya Afrika, Ghiliba ni sehemu ya siasa za Afrika, mauaji ni sehemu ya siasa za Afrika, Kung'ang'ania madaraka ni sehemu ya siasa za Afrika,

Siasa za upinzani nchini Tanzania zimepita kwenye kipindi kigumu sana tangu kuingia kwa mfumo wa vyama vingi nchini, nitaangazia kwa kifupi mapito ya vyama vya siasa tangu mwaka 1995 mpaka leo tunakwenda 2020 na huko tuendako,

NCCR ya Mrema ilipitia kipindi kigumu sana hasa baada ya ule uchaguzi uliotikisa chama tawala na kuamua kuiundia mkakati rasmi wa kuiangamiza, ni kipindi ambacho nchi ilikuwa imetoka kwenye mfumo wa chama kushika hatamu,

System ilipewa majukumu kamili ya kuhakikisha wanaizima kabisa NCCR na moja ya kituko cha kuvutia ni kujazana kwa majasusi ndani ya chama hicho mpaka kufikia mshika mikoba halisi wa Mrema alikuwa nyoka (Maswi).

Lakini licha ya CCM kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kumdhibiti Mrema, jambo lingine lililomdhoofisha ni serikali kudhibiti uchumi wake.

2000 Aina hii ya udhibiti wa upinzani ilitumika japo si kwakiwango kikubwa hasa kutokana na aina ya siasa za CUF pale Zanzibar, lakini bado system iliendelea kutumika kwa kila njia kuvuruga mission za CUF, na mwisho wamefanikiwa kuwanasa Mwenyekiti Lipumba na Naibu Katibu Mkuu Bara bwana Julius Mtatiro.

Kuingia madarakani kwa Mbowe na safu yake kwenye siasa za CHADEMA kulibadili sura halisi ya siasa na kufanya ccm ibadili kila kukicha mbinu ya kukabiliana na CHADEMA.

Mbinu yakutumia System kudhoofisha CHADEMA ilianza kufeli zaidi baada ya CHADEMA kubadili mbinu na kuunda mfumo stahiki wa ulinzi wa Chama na hasa ujio wa mageuzi ya kiteknolojia na mwitikio wa vijana katika siasa mpya miaka ya 2O1O hadi miaka 2O15 hivi.

Baada ya kufeli watawala wakaja na mbinu ya kudhoofisha viongozi kiuchumi, hapo ndipo nguvu ya Mbowe ilipodhihirika, Mbowe anayekadiriwa kuwa na utajiri wakuzaliwa wa thamani ya 850b-1.2tr amekuwa kisiki kikuu kwa CCM kuvunja upinzani, licha ya serikali ya Magufuli kupora na kuvuruga miradi mikubwa ya Mbowe iliyokuwa imeajiri maelefu ya watu, bado Mbowe ni yuleyule wa jana leo na kesho, zaidi tu ccm na vibaraka wake wamewaumiza maelfu waliokuwa wameajiriwa katika miradi na biashara za Mbowe huku serikali ikijikosesha kodi tu.

CCM ilibadili mbinu na kurejea mbinu zake za kale zilizofeli za kununua wapinzani kama Mrema (TLP), Cheyo (UDP), Mtikila (DP) nk. Hawa CCM imefanikiwa kuwaweka mfukoni rasmi, wanapumua kwa gharama ya ccm, yani CCM inamaamuzi makubwa juu yao kisiasa na kiuchumi.

Uwezo binafsi wa kiuchumi, kimtazamo na kifikra wa Mbowe, Uwezo wa kifikra na kimsimamo wa timu yake ya uongozi vimekuwa gharika kwa ccm na kuifanya itumie mabilioni ya pesa kununua viongozi wa ngazi ya chini kama sehemu ya kuibomoa CHADEMA. Jambo ambalo sisi wataalamu wa siasa tunalitazama kwamba ni mradi wa uhalifu unaoteketeza kodi za umma badala ya kuisaidia ccm.

Nasema hivyo kwakuwa katika mradi huu hakuna mwanachama au mpiga kura anayehama isipokuwa ni diwani au mbunge tu aliyenunuliwa ndie anahama na pengine hata familia zao zinawakatalia kuhama. Vyama vya siasa vya kileo vinatakiwa kuongozwa na watu wenye financial stable, bila hivyo chadema ingeshakuwa kama UDP, Cuf nk.

Umma unahitaji mabadiliko, unahitaji kubadilisha chama na viongozi wote waliochini ya ccm, Chadema licha ya sera na itikadi yake nzuri, Uhai wake unajengwa zaidi na hasira za umma dhidi ccm na serikali. Iwe kwa matendo mauvu ya ccm au mazuri ya ccm, bali binadamu kwaasili huhitaji mabadiliko, ukifika muda wa mabadiliko binadamu hazuiliki na haambiliki, hivyo ndivyo Watanzania wanavyotaka, hakuna cha ccm asili wala ccm ya wahamiaji iitwayo ccm mpya.

Kwa tafsiri hiyo, Hivyo Chadema haiwezi kufa, labda kipatikane chama mbadala wa ccm zaidi ya Chadema ambapo kwa hakika hakipo, Umma uko upo tayari kufa na Chadema kwakuwa umechoka na kufedheheshwa na ccm na hauko tayari kugeukia ccm.

Ili Chadema ife, ni lazima kiwepo chama mbadala ambacho kinakonga vilivyo nyoyo za umma kwa kuikabili ccm na serikali yake vilivyo zaidi ya Chadema, na sio vilivyo kama Cuf, TLp, nk ambavyo ni vibaraka vya ccm na umma unajua fika. Ukitazama dhamira na maneno ya Mwenyekiti wa ccm Magufuli anasema moja ya ahadi zake ni kuua upinzani, hili anajidanganya au kudanganya wanachama wake, na zaidi ni kujivika bomu. Wataalamu wa siasa wa ccm wanaekelewa umuhimu wa vyama pinzania, na wale waliohudumu kipindi cha Nyerere wanajua kwanini siasa za vyama vingi zilikubaliwa haraka. Nyerere hakuwa mjinga.

Na Yericko Nyerere

View attachment 833416View attachment 833416
BLAH BLAH..Upinzani hautakufa lakini CDM inajifia.
 
Back
Top Bottom