Ni basi gani zuri la Dar - Mwanza?

Ni basi gani zuri la Dar - Mwanza?

TANGANYIKA BUS SERVICE COMPANY LIMITED

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Unanikumbusha enzi hizo za Tanganyika Bus Service. Mhindi (au sijui Mwarabu?) huyo alikuwa ameitawala route hiyo miaka ya 60 na 70. Mwanza ndiyo ilikuwa makao makuu ya kampuni na njia ya Mwanza - Dar ndiyo ilikuwa ndefu kuliko zote. Kila siku saa 10 jioni kuna gari linatoka Mwanza na jingine linatoka Dar. Yanapishana Singida. Saa 10 jioni kesho yake, saa 24 baadaye, linafika liendako. Kumbuka, siku hizo hakuna lami mpaka unapoingia mji. Lakini magari yalikuwa hayachelewi sana. Mbali na hiyo route ndefu, zilikuwepo zingine za masafa ya kati, kama vile Mwanza - Tabora; Mwanza - Bukoba; na Mwanza - Musoma. Aidha, zilikuwepo za masafa mafupi, kwa mfano Mwanza - Shinyanga. Ukifika kituoni Mwanza, safari za basi zinatangazwa kwa loudspeaker sawasawa na matangazo ya treni yanavyofanywa stesheni: "Gari liendalo Tabora sasa linapakia. Abiria wanaombwa kupanda na gari litaondoka baada ya dakika 15". Kwa Dar kituo kilikuwa Kisutu, karibu na jumba la senema la Odeon.
 
Back
Top Bottom