Ni bajeti ya kumuua mkulima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni bajeti ya kumuua mkulima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kyindokyakombe, Jun 14, 2012.

 1. K

  Kyindokyakombe Member

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika serikali haimjali MKULIMA imemntengea asilimia moja ya BAJETI nzima.WANANCHI wanapaswa waamke wajue hii SERIKALI haiwatambui imewajali wanaoishi MIJINI.WANANCHI sasa jiandaeni mtakunywa GONGO vileo bei juu na gharama za kupiga simu zimeongezwa.INASIKITISHA Wtz wenzangu MUNGU ibariki Tz.
   
 2. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hili suala la mkulima bado ufumbuzi wake uko mbali sana. Kwa mfano Waziri amesema ongezeko kubwa la inflation lipo kwenye chakula, moja ya mikakati ambayo inafanywa kupunguza hali hiyo ni pamoja na kuongeza uzalishaji pamoja na kutoa vibali vya wafanya biashara kuagiza kutoka nje ili kuimarisha supply ya vyakula na hivyo kupunguza bei. Hii imeangaliwa kwa upande mmoja tu wa mlaji ambaye yuko mjini, wale wazee wanaoteseka kule vijijini kulima wakizani bei zitapanda ili wapate kulipa ada za watoto shule kuvaa, na hata kuburudika sasa matumaini yao yanakwisha. Bei ya mazao yao itapungua bila kujali gharama za uzalishaji kama bembe jeo, madawa, gharana za kilimo chenyewe n.k

  Ingekuwa bora pia kama serikali inaweka mfuko wa kuwasupport (subsidy) vinginevyo hatuwezi kumaliza umaskini hwich is a rural phenomena.
   
 3. samilakadunda

  samilakadunda JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 1,701
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkulima afe marangapi mkuu?? Nilidhani tujadili juu ya Matanga ya mkulima!
   
Loading...