Ni ajenda gani ya siri na hii hama hama ya wabunge?

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,115
katika historia ya nchi yetu tumeshuhudia makubwa yanayofanyika katika siasa. hususani la viongoz wa majimbo kuhama chama hiki na kujiunga na ccm harafu kugombea majimbo hayo hayo kuutaka ubungo ule ule walio achana nao.

je tutulie tukiamin kwamba lengo lao ni kuunga juhudi za rais hakuna lililo nyuma ya pazia?? ina maana miaka yoote ya uongozi imezidiwa na awamu hii kwa kuleta maendeleo kias kwamba ndio awamu pekee iungwe mkono kuliko zote zilizo pita?? hapa kuna jambo linaandaliwa tukibweteka na kuponda tu hii hama hama tutakua hatutumii akili. hebu tuanze kushughulisha vichwa vyetu . ninini ajenda ya serikali hii ya ccm inapanga kufanya huko mbeleni??

wafanyakaz mwaka wa tatu hakuna nyongeza za mishahara lakn watu wanasema hii awamu inafanya makuu!!
ya kweli haya?? kuna ninini kinaandaliwa kufanywa kikubwa??

tukumbuke ni bajet kabisa inapangwa kuwapata hawa wabunge na madiwani.
kuna wakati inaweza pita miezi sita hutosikia mtu akiunga juhudi za mweshimiwa. ila bajeti ikitoka mwezi mmoja au miwili hivi utasikia watu wanaunga mkono juhudi za mheshimiwa. bajeti ikiisha kunakua kimyaaaa. je wanaambizana Tanzania nzima, huu ni wakati wa kuunga mkono juhud za mheshimiwa??kumbukeni tulipumzika kuzisikia hizi mambo

sasa twende kwenye hoja nini ajenda ya hii hama hama???

tumegundua hawahami kwa hiali yao bali wanasawishiwa na serikali ya ccm je ajenda ya wanaoongoza serikali ninini?? sina majibu juu ya kilicho nyuma ya hii hama hama ila nawaasa watanzania wenzangu tunapaswa kujadili lililo mbele yetu kuliko kuponda tuu hii hama hama. siku tukishituka tutajikuta wametutumbukiza shimoni huku sisi tulikua tunaona kabisa tunasombwa na kupakiwa kwenye maroli ila hatukushituka je sisi ni mizigo hadi tusione tunaenda wapi??

binafsi naona wana mpango wa kubadilisha katiba huko mbeleni sasa wanaandaa wabunge wengi wa kuunga mkono jambo lao. sio kubadirisha kutupa nzuri baki kandamizi ikiwemo kuongeza muda wa uraisi.

kingine wanaatuandaa kasaikojia huko mbeleni wabunge wa upinzani wapatikane wachache ikiwezekana wasiwepo na hatutashituka maana tutasema ccm imeanza kupendwa hata kabla ya uchaguzi.

pia wanatutoa kwenye njia tusiende kupiga kura maana hatutakua na imani na viongoz wetu, tukiamini muda wowote watamuunga mkono tunaempinga.

kubwa zaidi hawataki vyama vya upinzani. hata vikiwepo basi viwe ni vile vyenye kuendeshwa na wao. lakn wapinzani halisi wanawafuta wote.
tujiandae mwaka 2020 kutowaona wabunge wote machachali maana hawataki kukosolewa. kama kuna mpinzani ataingia bungeni basi ni yule asiye na madhara kwao. ila akina LEMA , LISSU , MDEE, ZITTO ba wengineo tutaweka historia waliwahi kuwa wabunge.

huo ni mtizamo wangu. je nyie wana jamvi mnahisi hawa wanunuzi wamepanga kutufanyia nini huko mbeleni?? njooni tujadili hatima ya siasa za nchi yetu. tukikaa kimya hatufikilii yaliyo mbele yetu.
 
Tulipofikia ni bora itangazwe kuwa tuna mfumo wa chama kimoja kwani sioni maana na uwepo wa vyama vingi kama utaratibu ndio huu wa kuchagua watu na kuhama kisha kuchagua tena.
 
Lengo ni kupandikiza mamluki ndani ya CCM. NI mkakati wa Chadema. Fight the enemy them from within philosophy.
 
Mkakati wa CHADEMA kwa kutumia fedha za Chama kingine!!?? Hii ngumu kuamini.

Binafsi naona ni upigaji tu kama ulivyo upigaji mwingine. Sema huu wameadvance kidogo baada ya kugundua udhaifu wa rubani. Ukitumia mwavuli wa CHAMA utapiga hadi uchoke wala hutaguswa.

ANGALIZO:
Ole wao wanaokubali mchezo huo wakija kukengeuka mbele ya safari huku fedha nyingi zimemwagwa kwa ajilimyao,watakiona cha moto kutoka kwa wahusika wa hiyo biashara.

***Wakishinda katika hilo,waandae majibu mazuri kwa Mungu,maana wanatugharimu maisha yetu kwa namna mbalimbali**
 
Hahaha Mkuu, kutumia fedha za chama kingine inaweza kuwa sehemu ya mkakati. Yaani hawa wabunge wa Chadema wajifanye wananunulika na fedha ziingie Chadema. Si unaona Sugu alipewa offer ya Tshs 2 billion ahamie CCM kwa hiari au wam-deal?
 
Lini hiyo mkuu na nni alitoa offer?

Kuna watu hawataki kuelewa kitu kimoja..... Uchaguzi mkuu ujao utakuwa mgumu kuliko wengi wanavyotarajia. Ila ninachoomba ni kuwa anayestahili na ashinde awe CCM au Upinzani. Ilimradi ameshinda kwa kura halali.
 
Juzi tu hapa Mkuu. Sugu akatoa hadharani kwamba kwanza wawanunue wapiga kura wake wote halafu yeye ndio awe wa mwisho kununuliwa
 
Hatari sana
Sana Mkuu

1533630138404.png
 
katika historia ya nchi yetu tumeshuhudia makubwa yanayofanyika katika siasa. hususani la viongoz wa majimbo kuhama chama hiki na kujiunga na ccm harafu kugombea majimbo hayo hayo kuutaka ubungo ule ule walio achana nao.

je tutulie tukiamin kwamba lengo lao ni kuunga juhudi za rais hakuna lililo nyuma ya pazia?? ina maana miaka yoote ya uongozi imezidiwa na awamu hii kwa kuleta maendeleo kias kwamba ndio awamu pekee iungwe mkono kuliko zote zilizo pita?? hapa kuna jambo linaandaliwa tukibweteka na kuponda tu hii hama hama tutakua hatutumii akili. hebu tuanze kushughulisha vichwa vyetu . ninini ajenda ya serikali hii ya ccm inapanga kufanya huko mbeleni??

wafanyakaz mwaka wa tatu hakuna nyongeza za mishahara lakn watu wanasema hii awamu inafanya makuu!!
ya kweli haya?? kuna ninini kinaandaliwa kufanywa kikubwa??

tukumbuke ni bajet kabisa inapangwa kuwapata hawa wabunge na madiwani.
kuna wakati inaweza pita miezi sita hutosikia mtu akiunga juhudi za mweshimiwa. ila bajeti ikitoka mwezi mmoja au miwili hivi utasikia watu wanaunga mkono juhudi za mheshimiwa. bajeti ikiisha kunakua kimyaaaa. je wanaambizana Tanzania nzima, huu ni wakati wa kuunga mkono juhud za mheshimiwa??kumbukeni tulipumzika kuzisikia hizi mambo

sasa twende kwenye hoja nini ajenda ya hii hama hama???

tumegundua hawahami kwa hiali yao bali wanasawishiwa na serikali ya ccm je ajenda ya wanaoongoza serikali ninini?? sina majibu juu ya kilicho nyuma ya hii hama hama ila nawaasa watanzania wenzangu tunapaswa kujadili lililo mbele yetu kuliko kuponda tuu hii hama hama. siku tukishituka tutajikuta wametutumbukiza shimoni huku sisi tulikua tunaona kabisa tunasombwa na kupakiwa kwenye maroli ila hatukushituka je sisi ni mizigo hadi tusione tunaenda wapi??

binafsi naona wana mpango wa kubadilisha katiba huko mbeleni sasa wanaandaa wabunge wengi wa kuunga mkono jambo lao. sio kubadirisha kutupa nzuri baki kandamizi ikiwemo kuongeza muda wa uraisi.

kingine wanaatuandaa kasaikojia huko mbeleni wabunge wa upinzani wapatikane wachache ikiwezekana wasiwepo na hatutashituka maana tutasema ccm imeanza kupendwa hata kabla ya uchaguzi.

pia wanatutoa kwenye njia tusiende kupiga kura maana hatutakua na imani na viongoz wetu, tukiamini muda wowote watamuunga mkono tunaempinga.

kubwa zaidi hawataki vyama vya upinzani. hata vikiwepo basi viwe ni vile vyenye kuendeshwa na wao. lakn wapinzani halisi wanawafuta wote.
tujiandae mwaka 2020 kutowaona wabunge wote machachali maana hawataki kukosolewa. kama kuna mpinzani ataingia bungeni basi ni yule asiye na madhara kwao. ila akina LEMA , LISSU , MDEE, ZITTO ba wengineo tutaweka historia waliwahi kuwa wabunge.

huo ni mtizamo wangu. je nyie wana jamvi mnahisi hawa wanunuzi wamepanga kutufanyia nini huko mbeleni?? njooni tujadili hatima ya siasa za nchi yetu. tukikaa kimya hatufikilii yaliyo mbele yetu.
mkuu umeongea kitu nyeti kabisa yaani naiyona Tanzania ya Uganda,rwanda,burundi,congo:(:(:(
 
Kufuatia hili sakata la hama hama, ni kuwa kuna siri nzito mno maana hata suala la kujua ni nani atafuata imekuwa kizungumkuti kwani tunayekuwa tunamdhania anakua siye!
Inaonekana hii biashara inafanyika kwa siri na pengine kuwa na viapo au pengine vitisho n.k!
Imekuwa kwamba zinaposambaa habari kuwa fulani yupo mbioni kuhama basi, anakuwa siye anahama mwingine ambaye hakuwa akitegemewa!
Nani alikuwa akijua Waitara atahama?
Vipi kuhusu mbunge wa monduli?
Ni wazi kuwa tayari wapo ambao washafika bei ila wapo kimya, na siri zao zimefichwa ila ipo siku itafika watajitokeza kama ilivyokuwa kwa Mtatiro!
Ukimya wa hawa watu wengine kama Mayor wa jiji la Dsm, jiji la Arusha, Said Kubenea, hata hawa akina Mnyika, Msigwa n.k unatia shaka juu ya hii hama hama....
Kati ya hao wapo watakaotimka lakini ni dhahiri kutakuwa na watangulizi wao wengine ambao wala hakuna anayewajua zaidi ya walioweka mzigo mezani!
Lakini hili ndio kaburi la ccm, muda ni mwalimu mzuri sana...
 
Hakuna mwanasiasa wa Upinzani mwenye akili timamu atakwayebaki na UDIKTETA Mbowe bora akawe kwenye udikteta mwingine lakini sio huo wa kijuha.
Wabunge wanachanga pesa zao kuendesha chama halafu Mbowe anasema kuwa hakuna mtu wa kuongoza Chama zaidi yake. Hii ni akili au matope?

Kwa nini Mtu muhimu kama Mtatiro asiende CCM akateuliwa kiwa kuwa katibu wa Wizara au Mkuu wa Mkoa akawatumikia wananchi kwa vitendo.

Anayejua Mbowe anafanya harakati gani za kujenga chama au kuilazimisha serikali ikae na kurudi kwenye misingi ya Kisheria atuambie.
Wakurugenzi ni watu wadogo sana lakini wameamua wenyewe tu kuvuruga demokrasia nchini bila kulazimishwa na mtu yeyote. Mbowe hamna jambo lolote analofanya la maana la kudhibiti huu ujinga wa wasimamizi wa uchaguzi tena wadogo kabisa kwenye kata halafu anajisifu kuwa bila yeye chama kitakufa.
Ujinga mtupu.
Mbowe MPAKA sasa hajawahi kuleta takwimu ya ushindi wa kura zilizoibwa.
Hajafungua kesi yoyote mahakamani. Anadanganya watu KUWA mahakama hazitendi haki kisa ana kesi mahakamani .
Kesi ambazo bila shaka zinaweza zikamgaiya miaka mitatu au minne ya kwenda kupumzika gerezani.
Mahakama zetu bado zinatenda haki sana. Hakuna jaji anayeweza kupindisha haki duniani.

Tumewaona majaji wastaafu wakisimama na kusema kweli tofauti na Watu wengine.

Narudia tena na tena Bila Mbowe kuachia Kiti cha uenyekiti na kukabidhi mtu mwingine na mbowe arudi jimboni ajizatiti kwenye jimbo lake ili 2020 ashinde halika Chama kitarudi kilipotoka.

Woga wa Mbowe ni 2020 akikosa jimbo basi abaki kama Mwenyekiti wa chama. Japo wakati huo ruzuku za vyama zitakua zimefutwa naada ya uchaguzi wa 2020. CCM wao wejianda na wanaanza kuweka Mali zao vizuri ili chama kijiendeshe.
 
Back
Top Bottom