Ni ajali ya ndege?

Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,323
18,793
Wadau mlioko karibu na uwanja wa ndege wa Arusha hebu tupeni habari kuna ndege yenye reg no 5H-PAY ya kampuni ya Zan Air iko kwenye majani nje ya runway na abiria wake wametokea kwenye emergency doors nini kimeisibu ndege hiyo
 
Nimewasiliana na jamaa zangu wa kiwanja cha ndege Arusha juu ya kadia hii, wanasema kimsingi ilitokea.
Wanasema ndege hiyo si ya Zan air parse, bali wao waliikodi ili kuwapeleka abiria wao Zanzibar. Inamilikiwa na kampuni ya Tan-Wing ya Zanzibar

Wameeleza kuwa rubani wa ndege hiyo wakati akijaribu kugeuza ndege kwenye njia ya kurukia, ili aanze kukimbia na kuchukua kasi ya kuruka, alienda nje ya eneo lililoshindiliwa, akaingia kwenye matope na kuzama.

Chanzo kinasema Ilibidi abiria washuke, na ndege hiyo kusukumwa na kundi la watu ndipo ikakwamuliwa.

Taarifa zaidi zinasema kuwa baadhi ya abiria hao walikataa kuruka na ndege hiyo tena, wakajigharamia kutafuta njia zingine za usafiri.
Nawasilisha.
 
Asante sana kwa habari hii

Back
Top Bottom