Ni aina gani ya water pump ni imara na madhubuti?

nacho1

Member
Aug 31, 2014
82
67
Poleni na mapambano na mikikimiki ya uzalishaji kama ilivyo utamaduni wa wanajukuaa hili( ijapokua kule Japan mtu anayapambana haambiwi pole bali anaambiwa pambana au kazana)

Naomba kujulishwa aina nzuri ya water pump imara kwa ajili ya umwagiliaji shambani yenye sifa zifuatazo:
a) inayoweza kuvaa bomba la
2" au 3"
b) yenye uwezo wa kusukuma
maji umbali wa mita 200
kwenye mwinuko mdogo
c) inayodumu kwa muda mrefu.

Anayefahamu mambo mengine mbali na hivyo vigezo ni vizuri akiyabainisha. Asante
 
Swali lifananalo na hili lishawahi ulizwa humu siku chache zilizopita na likawa na mjadala mrefu,jaribu kutizama hio thread ila kumbukumbu yangu wazoefu walishauri zakijapani aina ya honda
 
Asante mkuu gimmy's kwa ushauri, ngoja niusearch fasta japo nimeona uzi uliorushwa na jamaa wa msasani anaeuza pump ila sikubahatika kuona za saizi yangu niliyonayo ya chini ya 400,000
 
Ok,kwa bei hio hunabudi kununua zakichina baada ya kuanza kazi utajipanga kuta ilioimara.Lakini pia endelea kufuatilia kama zipo za mtumba pia ufaham ubora wake huenda kwa pesa yako ukapata kilicho bora
 
Back
Top Bottom