Kwa karne hii ya 21 yenye vizazi vya wasomi waliobobea katika nyanja mbalimbali hapa Tanzania hatuna mahakama ya kuhoji matokeo ya Urais ni aibu sana
Vinchi vidogo vidogo vyenye population ndogo kama Malawi wamekuwa na uelewa wa kuwa na mahakama ya kuhoji matokeo ya Urais halafu Tanzania tunakuwa na wasomi wanaojali matumbo yao na kuabudu watawala
Nchi nyingi duniani wanaofanya uchaguzi wa vyama vingi waliishaona mbali kama kutoridhika kwenye uchaguzi iwepo mahakama ya kuhoji matokeo ili kuondoa utata still sisi tupo kwenye ujima ni aibu kwa wanaojiita wasomi kwenye hii nchi
Kenya walijifunza kwa uchaguzi ule uliozua ghasia chini ya Samwel Kiwitu na kuja na katiba ambayo imeweka kila kitu separated, na isingekuwa katiba mpya hii referendum ingelete mzozo mnoo
Mnaojiita maprofesa,madakrari na wanazuoni wa Tanzania ni aibu kwenu na vizazi vyenu
Kama haiwezekani basi Tanzania ijulikane ni nchi ya kishoshilisti na tufute mfumo wa vyama vingi kama zilivyo nchi za kishoshilisti tusifanye maigizo
La sivyo muundo huu wa uchaguzi kama sio sasa utakuja kugharimu maisha ya watanzania kwa malaki
Mpaka sasa jeshi la polisi wanapata wakati mgumu kwa sababu wangewambia upinzani nendeni mahakamani mkadai haki,mahakama haipo imebaki jeshi la polisi kutoa vitisho kila dakika hii ni aibu Tanzania na wasomi wake