Ni aibu Tanzania mpaka sasa hatuna Mahakama ya kuhoji matokeo ya Urais

Wakati mwingine najiuliza kwanini nilizaliwa Tanzania.

Nchi yenye watu hawaelewi HAKI na UTAWALA WA SHERIA.

Huenda nina kusudi huko mbeleni kufanya mabadiliko.

Mungu nisaidie nimalize kusoma SHERIA.

Nitafanya kitu kwa nchi yangu na kuwa mstari wa mbele kwenye kuleta HAKI NA UTAWALA WA SHERIA.

Ciao!
Kuna sababu, ili uje upiganie haki. Ndo mana Mungu akaona ni vema akulete huku kwenye uhitaji
 
Zitakuwepo siku upinzanI ukiwa serious na kujitambua.Upinzani uliopo ni wa ruzuku na kulea familia zao siyo kupigania taifa.
 
Haya mambo mlikua mnayasikia Nchi jirani mnachekelea, yameingia chumban mwako sasa
Kabisa mkuu. Kama vile utani yanatukuta. Sijawahi kufikiria Tanzania itakuja kufikia hatua hii. Yaani mtu kwa ubabe kabisa anaamua kufanya anachotaka. Bora angefanya mazuri basi sio yale ya kutupelekea kupigwa vikwazo vya kiuchumi. Tukipigwa vikwazo vya kiuchumi maisha yatakuwa magumu balaa. Tutaanza kuliwa na simba maporini tukikimbilia kwenda nchi jirani kwenda kutafuta unafuu wa maisha kama wanavyofanya wazimbabwe na waethiopia. "Mwenyezi Mungu tusaidie baba"
 
Kwa karne hii ya 21 yenye vizazi vya wasomi waliobobea katika nyanja mbalimbali hapa Tanzania hatuna mahakama ya kuhoji matokeo ya Urais ni aibu sana

Vinchi vidogo vidogo vyenye population ndogo kama Malawi wamekuwa na uelewa wa kuwa na mahakama ya kuhoji matokeo ya Urais halafu Tanzania tunakuwa na wasomi wanaojali matumbo yao na kuabudu watawala

Nchi nyingi duniani wanaofanya uchaguzi wa vyama vingi waliishaona mbali kama kutoridhika kwenye uchaguzi iwepo mahakama ya kuhoji matokeo ili kuondoa utata still sisi tupo kwenye ujima ni aibu kwa wanaojiita wasomi kwenye hii nchi

Kenya walijifunza kwa uchaguzi ule uliozua ghasia chini ya Samwel Kiwitu na kuja na katiba ambayo imeweka kila kitu separated, na isingekuwa katiba mpya hii referendum ingelete mzozo mnoo

Mnaojiita maprofesa,madakrari na wanazuoni wa Tanzania ni aibu kwenu na vizazi vyenu

Kama haiwezekani basi Tanzania ijulikane ni nchi ya kishoshilisti na tufute mfumo wa vyama vingi kama zilivyo nchi za kishoshilisti tusifanye maigizo

La sivyo muundo huu wa uchaguzi kama sio sasa utakuja kugharimu maisha ya watanzania kwa malaki

Mpaka sasa jeshi la polisi wanapata wakati mgumu kwa sababu wangewambia upinzani nendeni mahakamani mkadai haki,mahakama haipo imebaki jeshi la polisi kutoa vitisho kila dakika hii ni aibu Tanzania na wasomi wake
Aibu kwa nani?
 
Mie naisikitikia tu nchi yangu. Yaani mtu mmoja anaamua tu kufanya anachotaka na hakuna cha kumfanya. Hivi hakuna hata mtanzania mmoja mwenye ujasiri wa kumwuliza "kwa nini ameingiza kura fake? Haoni kama atatusababishia maisha kama ya wazimbabwe? Kwa nini asituhurumie? Mbona bila hata kura fake angeshinda tu?" Dah! Naililia nchi yangu, maskini nchi yangu.
Unafahamu wewe kilichotokea Zimbabwe? Je, una ushahidi wa hayo unayosema?
 
Matumbo yao indeed!

Sisi tuna wagombea njaa tu wanaoaim kulamba ruzuku kila baada ya uchaguzi kuisha.

Hii kufuru waliyofanya CCM bila shaka itatufumbua macho sote
 
Rais anapendwa na kila mtanzania wewe unataka kwenda mahakamani kuhoji nini!!
 
Kwenye katiba tuliyonayo tuna mahakama ambayo inaweza kusikiliza kesi za matokeo ya uchaguzi mkuu upande wa rais mahakama hiyo ni mahakama maalumu ya katiba (special constitutional court) Lakin changamoto yake ni kwamba
-tangu imeanzishwa haijawai kukaa yan ipo tu kwenye katiba kwenye maisha halisi haipo
-Kuna baadhi ya ibara zinazuia kutekeleza majukumu yake (Ouster clause) mfano ile inayosema hakuna mahakama yenye uwezo wa kusikiliza kesi kuhusiana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais


suluhisho..
rasimu ya katiba ya warioba ya 2014.. imeweka mahakama itakayohusika na maswala ya uchaguzi inaitwa mahakama ya juu (hii ni tofauti na mahakama kuu)
 
Back
Top Bottom