Ni aibu na upuuzi kutumia jina la Lowassa kufunika uovu wako

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,252
8,003
Sikupenda kulizungmzia hili lakini imenibidi baada ya kuona watu waliofilisika kimawazo na kisiasa kila kona kutumia jina la mtu kufunika maovu yao.

Kumekua na watu humu hasa wafuasi wa chama cha mapinduzi bila as aibu kupenda kulitumia jina la aliyekua Mgombea wa urais kupitia UKAWA Mh Edward Lowassa.

Watu hawa bila hata kumwogopa Mungu hupenda kutimiza Malengo yao binafsi kutumia jina la mtu ambaye alishsutangazia umma kua yeye mikono yake ni safi na aliamua kumwachia Mungu kwa yote yanayosemwa juu yake.

Hawa watu ambao binafsi kwa Lugha mimi huwaita wafu wa kisiasa ni kwanini wanashindwa kukuelewa haya?
1. Huko Bandarini kwenye Makontena na mita za mafuta Lowassa yupo?
2. Huko NIDA kuna mkono wa Lowassa?
3. Huko UDA kuna mkono wa Lowassa?
4. Majipu yote yanayotumbuliwa na mtu amesikia Lowassa akitajwa?Maana kuna hata wengine wameshaambiwa hawachomoi.

Unapokosa kitu cha kuongea ni bora kukaa kimya maana aliyetaka kuzamisha hii nchi umma watanzania unamjua na hata dunia inajua na sio Lowassa.
 
Polepole Mahanju si kila anayemponda LOWASSA au CHADEMA for that matter ni mfuasi wa CCM! Nenda taratibu ukichambua hoja yako. Nawajua watu kibao walioipuuza CDM na Lowassa kwa kuwa hawakuwaelewa na ngonjera zao za "mfumo" lakini waliwahi kumpigia kura Mzee Slaa na waliamini katika CDM.
Kuna vijana walioiponda CDM sana tu wakati wakiamini Lowassa atapata tiketi kijani lkn wamehama naye na sasa ni waumini huko CDM!
 
lowassa ni fisadi .... hili kila mtanzania anajua...

Ahsante tundu lisu na viongozi wengine wa Chadema kwa kuzuunguka mikoa yote kunadi ufisadi wake...

Ahsante mwanahalisi kwa kutumbua hili jipu "lowassa hasafishiki"
 
Mi mwenyewe nawashangaa Hawa wazee wa Lumumba kila kitu lowasa, ila mpaka sasa kwenye majipu yote sijasikia lowasa akitumbuliwa zaid ya viwav. Soon tutaona wakiaibika
 
Angalia uozo wa kutisha bandarini, hazina kukombwa na kusafishwa, NSSF, hela ya wastaafu East Africa, DART, Na alitaka kujenga bandar bagamoyo 10 Billions $
 
lowassa ni fisadi .... hili kila mtanzania anajua...

Ahsante tundu lisu na viongozi wengine wa Chadema kwa kuzuunguka mikoa yote kunadi ufisadi wake...

Ahsante mwanahalisi kwa kutumbua hili jipu "lowassa hasafishiki"
Fisadi ni wale walio iba ela za escrow,
 
kutumia jina la mtu kusawazisha mambo yako. ushalifu wa kiuchumi uliowekwa wazi ni zaidi ya Lowassa ambaye anatuhumiwa bila ushahidia.

Mimi ninachoamini wizi ni wizi tu hata kama ni mdogo kabla ya kumtuhumu mwenzako hakikisha uko safi.

Inawezekana kabisa sisi wenyewe tunaoandika humu tumewaibia ndugu zetu au mahali unapofanya kazi hata wikii haijakwisha .
 
Richmond ilitokana na maagizo kutoka ngazi za juu, mwenye ushahidi apeleke mahakamani-Lowassa
 
Yeye mwenyewe Lowasa amekaa kimya hawezi nyanyua mdomo wake maana anajua Magofuri ni nani
 
Tatizo humu ndani watu wanadhani hata Magufuli ni Masafi?
Wamuulize Dr Slaa aliivyomchana pale Tabora
Na hata wakati wa kampeni !
Lakini hamsemi au Kwa sababu analindwa kofia ya Urais ??
Hata huyo dr ana ya kwake kama wengine !!

ni swala LA muda tu
 
uyo mzee ni nembo ya wizi na ujambaz and that will never go away
 
Back
Top Bottom