Ni aibu kiongozi wa dini kuitupa injili na kutumika kisiasa

Uzi wako mzuri ila huwa nashangaa siku ambayo viongozi wa dini wanatumika kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu kwenye shughuli mbalimbali za kitaifa pamoja na kuisifia serikali (hiyo inakuwa sio siasa) lakini viongozi hao hao wakikosoa baadhi ya mambo (tunaanza kuwaambia wachague moja Injili ama Siasa)....
Ni kama taifa la Marekani!!! Korea ya kaskazini akipinga maazimio ya umoja wa mataifa anawekewa vikwazo, lakini Marekani akipinga maaazimio ya umoja wa mataifa hakuna anayedai naye awekewe vikwazo!!
 
Habari wanabodi,

Tangu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Magufuli kutangaza vita kubwa ya kiuchumi dhidi ya rushwa, wezi wa rasilimali zetu, wauza ngada ambao wanaharibu vijana wetu. Mh rais amegusa maslahi ya kundi kubwa sana lenye mtandao mpana wenye nguvu ambao hadi leo unatafuta kila namna kumchafua Rais na juhudi zake nzuri za kufanya ukombozi wa kiuchumi.

Kundi hili la wapiga dili linajaribu kutumia watu wenye image na influence kubwa katika kutekeleza mipango yao haramu na kila njia ili kuihujumu Tanzania.Watu hao wanaotumika ni kama wanasiasa uchwara kama tulivyokuwa tunaona kwa mh wa Nairobi pia hawakuishia hapo wakaenda mbali hadi kutumia viongozi wa kiroho tumeshuhudia jinsi gani baadhi ya viongozi wa kiroho wakiitupa injili na kutumika kisiasa kuchafua Serikali yetu pendwa ya awamu ya tano .

Ni aibu kubwa kwa kiongozi wa dini kuacha kondoo wa wakipotea na kutumika kisiasa.


Hivi unashindwaje kutafakari hata kidogo kabla ya kuandika thread yako? Hivi Rais kuambiwa atubu ni kupinga vita dhidi ya rushwa? kama unaamini Lissu alikuwa anapinga juhudi za kuzuia rushwa ebu tuambie ule ushahidi uliopelekwa takukuru wa viongozi kuwanunua madiwani umefanyiwa kazi? ujinga ukiwa mwingi kuliko maarifa ni hatari
 
the power of propagandas,sasa siasa yenyewe ni ya shetani au,hivi siasa si masuala mazima ya uongozi katika eneo fulani,sasa viongozi wa dini wana tatizo gani wakiizungumza? hawawezi kuikwepa kwani nao ni sehemu ya siasa
 
Watumishi wa Mungu wanapokuwa madhabahuni basi wanakuwa hawana mipaka kabisa kwani wanapaswa kuongea na kuhubiri vitu ambavyo vinaugusa jamii kwa sasa na kukemea km watumishi wa Mungu, mbona awo awo wanaombwa pia kuimbea serikali pamoja na viongozi wake,
Wakiikosowa serikali madhabahuni mnawaita wachochezi, huwo ni udoublestandandar mkubwa sana!
 
programmer95,
Umeandika kama mganga wa kienyeji mpiga ramli. Hili ni jukwaa la watu wenye akili zinazojitosheleza, na siyo wapiga ramli. Maswali machache kwako:

1) Hilo kundi la wapiga dili, unaweza kututajia japo wachache wanaoliunda?
2) Katika hilo kundi, ni nani wanawatumia watu wenye image na influence, na hao watu wenye image na influence ni akina nani?
3) Ni kiongozi gani ameitupa injili na kwa namna gani?
4) Una uthibitisho wowote wa kuonesha serikali yetu ni serikali pendwa?
5) Ni kiongozi gani aliwaacha kondoo wakipotea, na hao waliopotea ni akina nani?
6) Kuuza nyumba za serikali kwa ndugu na kimada kwa bei ya kutupa ya sh 10m, tena kimada ambaye siyo mtumishi wa serikali wakati mwongozo ilikuwa ziuzwe kwa watumishi wa umma, ni nini? Ni upigaji dili, wizi, ukosefu wa maadili, ujambazi au ni uongozi uliotukuka?
Ukijibiwa hizi nondo usisahau kunitag na mm
 
26166514_10155962664961726_3483064440778089644_n.jpg

Yamkini na hapa ni kanisani na alikuwa anahubiri :D:D:D
 
Habari wanabodi,

Tangu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Magufuli kutangaza vita kubwa ya kiuchumi dhidi ya rushwa, wezi wa rasilimali zetu, wauza ngada ambao wanaharibu vijana wetu. Mh rais amegusa maslahi ya kundi kubwa sana lenye mtandao mpana wenye nguvu ambao hadi leo unatafuta kila namna kumchafua Rais na juhudi zake nzuri za kufanya ukombozi wa kiuchumi.

Kundi hili la wapiga dili linajaribu kutumia watu wenye image na influence kubwa katika kutekeleza mipango yao haramu na kila njia ili kuihujumu Tanzania.Watu hao wanaotumika ni kama wanasiasa uchwara kama tulivyokuwa tunaona kwa mh wa Nairobi pia hawakuishia hapo wakaenda mbali hadi kutumia viongozi wa kiroho tumeshuhudia jinsi gani baadhi ya viongozi wa kiroho wakiitupa injili na kutumika kisiasa kuchafua Serikali yetu pendwa ya awamu ya tano .

Ni aibu kubwa kwa kiongozi wa dini kuacha kondoo wa wakipotea na kutumika kisiasa.
02c154849464c5f71ed1076f7cd7c42f.jpg
 
Lumumba pamechafuka naona pesa wiki hii imetoka yakutosha....polepole si wamchezo
 
Ukweli sisomi katiba yoyote ile. Feedom of speech ni sawa,lakini ikiwa na effect kwa wasikilizaji hupendeza zaidi.
Back to the point,Askofu wangu amejihesabia haki sana,kujivika kiatu cha Mungu kwa kumwamuru mtu atubu siyo fundisho la biblia. Kwani ajidhaniye amesimama....,ni wajibu wa mtumishi kumuombea mfalme hekima,na kwa hekima atayajua makosa yake na kuyaungama kwa hiari yake.
Huo ndiyo ujinga wangu unavyonipa kuamini.
Hivi unawezaje kutenganisha dini na siasa?Someni ukristo ulianzaje duniani..ndo mlete hoja
 
Uwezekano wakutenga dini na siasa ni mdogo sana kwakuwa zote ni dini na zote ni siasa..zinamalengo yake na nia zake pamoja na mitazamo yake..hapa napenda nitabaishe jambo kidogo kwakuwa wapo wanaodhani dini ni IMANI NA SIASA NI IMANI..OK ipohivi katika siasa mfano siasa za ujamaa nakujitegeme wao husema(kuhusu Mali za ulimwengu huu na ndizo ugomvi mkubwa wa ulimwenguni hapa) CHAKO NI CHANGU NACHANGU NI CHAKO..heee wote nadhni mnajuwa kinacho tokea juu ya falsafa hiyo ambao hao walio ianzisha waliona kuwa ingeweza kusaidia ulimwengu nawalimwengu ... Kwakweli nimoto na nadhani niseme kuwa imeshindwa..UBEPARI ;Hii nayo ni siasa ambayo nadhani mwanzilishi mkubwa ni nafsi ya mwanadamu meenyewe juu ya Mali za ulimwengu huu husema CHAKWAKO NI CHAKWANGU NA CHAKWANGU NI CHAKWANGU TU..Katika mfumo na mtazamo huo ninani Asiyejuwa yanayotokea ulimwenguni hapa sasa..ni shida kati ya walionscho na wasionacho..vita machafuko nsmengi yanaendelea.. Watu wa dini nao wanafalsafa yao nao husema..WAHITAJI NA WASIO JIWEZA ,WANYONGE NA MASKINI NI FARAJA YA ROHO KWA WOTE WENYE NACHO NA WASIO NACHO ; Hivyo hukusanya kote kwa fukara na kwa Mwenye Mali na matokeo pia yanaonekana..Lakini katikati ya MTU wa dini na MTU wa SIASA ;Kuna MTU wa IMANI juu ya MUNGU kadili ya mafundisho yake MTU huyu juu ya Mali ya ulimwengu jibu lake ni tofauti sana yeye anasimama kati ya ulimwengu na mbingu na hana hofu ya Mungu kwakuwa anaamini alitoka kwake na kwake atarejea tu...hivyo ataishi kwa kiasi katika kila jambo..atamwambia mkomonisti(mjamaa)na ( bepari) pamoja na MTU (dini)=CHAKO, NI CHAKO..CHAKWANGU PIA NI CHAKWAKO KWAFAIDA YETU WOTE..Na katika hayo MTU wa IMANI anautumia ulimwengu huu kama hayupo ulimwenguni hapa na hana kwazo katika ulimwengu huu wala was katika jsmii anayoishi
 
Back
Top Bottom