kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,086
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema katika kuhakikisha changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa bei mpya ya gharama za matibabu, wameweka kipindi cha mpito cha miezi sita ili kufanyia kazi. Katika kipindi hicho cha Julai hadi Desemba mwaka huu, watapokea maoni kutoka kwa watoa huduma na kuboresha zaidi ili kuondoa changamoto zitakazojitokeza katika kipindi cha utekelezaji wa bei mpya.
Aidha umetoa ufafanuzi wa kuondolewa kwa wategemezi wa mwanachama wa mfuko huo kuwa ilitokana na udanganyifu, uliokuwa ukifanyika na kueleza wazazi bado wanapatiwa bima hiyo.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kutokea malalamiko kwa baadhi ya watoa huduma kutokana na mfuko huo kupunguza gharama zake, jambo lililowafanya wanachama wa mfuko huo, kukosa kufanyiwa baadhi ya vipimo na kukosa huduma mbalimbali.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bernard Konga alisema kuanzia Julai mwaka huu, mfuko huo ulianza kutekeleza matumizi ya bei mpya za huduma ya matibabu kwa watoa huduma wake, waliosajiliwa na kutoa huduma kwa wanachama wa mfuko.
Alisema maboresho ya bei za matibabu ni utaratibu wa kawaida wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma bora za matibabu kwa wanachama wake na kurekebisha changamoto, zinazojitokeza katika baadhi ya bei zilizokuwa zikitumika awlai.
Alisema maboresho hayo, yamefanywa kwa kuzingatia mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kubadilika kwa bei ya gharama za matibabu nchini, maoni ya wadau wakiwemo wanachama na watoa huduma, kubadilika kwa miongozo ya tiba na matumizi ya teknolojia mpya katika tasnia ya huduma za matibabu.
Konga alisema kwa kuzingatia dhana ya utawala bora na ushirikishwaji wadau, mchakato huo uliwashirikisha wadau wote muhimu wakiwemo watoa huduma binafsi kupitia Chama chao cha Watoa Huduma Binafsi (APHFTA), ambao walitoa mchango wao wa maboresho ya bei na huduma na kuridhia utekelezaji wake.
Alisema maboresho hayo yaliridhiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto yenye dhamana ya kusimamia mfuko huo.
Alisema maboresho yaliyofanyika, yamehusisha kuongeza huduma zinazolipiwa na mfuko kama dawa, vitendanishi, vipimo na huduma ambazo hazikuwepo kwenye ulipaji wa baadhi ya huduma.
“Kwa kiasi kikubwa sehemu kubwa ya maboresho ya bei zinazotumika hivi sasa, yametokana na ushauri na maoni ya wadau wote na kwa kiasi kikubwa zinatarajia kuongeza uwezo wa kifedha na vituo zaidi ya asilimia tisini na tano ambavyo vinahudumia watanzania wengi zaidi, tofauti na bei zilizokuwa zinatumika awali,”alisema.
Alisisitiza kwamba maboresho ya bei za huduma, hayahusishi kubadilika kwa kiwango cha uchangishaji bali kuhakikisha kwamba wanachama wanapata huduma bora na watoa huduma wanapata malipo stahiki.
Awali, Ofisa Mtendaji Mkuu wa APHFTA, Dk Samwel Ogillo alisema uamuzi wa mfuko huo, unafanya bei za huduma za afya zikiwemo dawa na uchunguzi, zifanane katika hospitali zote nchini. Alisema hatua hiyo italeta mabadiliko makubwa kwa ngazi za chini za huduma za afya, ambazo zinakaribia asilimia 95 ya watoa huduma wa afya binafsi.
“Kabla ya uamuzi huo, ilituchukua miezi sita kufanya majadilano na serikali ili kutekeleza utaratibu huo mpya ulioanza mwezi Julai,” ilisema sehemu ya taarifa ya Ogillo.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa NHIF, Angela Mziray alisema wategemezi wanaowatambua sasa ni wale wanaotambulika serikalini. Alisema hatua hiyo ilifikiwa baada ya kubainika kuwapo kwa udanganyifu kwa baadhi ya watoa huduma na baadhi ya wanachama, ambao walifikia hatua ya kuuza uanachama wa bima hiyo.
Alisema walitambua hilo baada ya kubaini mara nyingine kuwa unaweza kukuta mwanachama ni mswahili, lakini mtegemezi wake ni mwenye asili ya Asia, jambo lililofanya mfuko huo kuibiwa sana.
Alisema udanganyifu huo, ulifanyika hasa kwa wagonjwa wenye magonjwa makubwa, kama vile figo ambapo mgonjwa hutumia zaidi ya Sh milioni moja kwa wiki kusafisha damu.
Alisema lakini wazazi na hata mtoto wa ndugu yako, ambaye unamlea ili aweze kupata kazi hiyo, inabidi kupeleka nyaraka zinazoonesha kumuasili mtoto huyo.
Awali, baadhi ya baadhi ya wagonjwa walilalamikia mfuko huo kwa kupunguza baadhi ya vipimo, kama kutahiri watoto wa kiume, kipimo cha kupima kirusi cha Human Papiloma (HPV) kinachosababisha saratani ya shingo ya kizazi.
Mmoja wa wagonjwa hao, Fatuma Njaidi alisema “NHIF inatuibia, mimi nakatwa asilimia tatu ya mshahara wangu wa milioni mbili lakini nimelazimika kulipia vipimo vya masuala ya uzazi kama Chlamydia, Mycoplasma na vipimo vingine vya homoni kama Anti Mullerian(AMH) na Ukimwi, kwa nini bima isinilipie?" NHIF imefanya mabadiliko ya bei kwa watoa huduma za afya ikipunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 60 ili kufanikisha mpango wa huduma ya afya kwa wote (UHC), lakini pia umeongeza gharama za vipimo katika baadhi ya huduma.
Mfuko huo sasa utakuwa ukiwalipa madaktari bingwa Sh 15,000 badala ya Sh 30,000 za awali na madaktari wa kawaida watalipwa Sh 7,000 badala ya Sh 10,000. NHIF pia imeshusha malipo ya gharama za matibabu zikiwamo za upasuaji ambao awali ungegharimu Sh 600,000 sasa utalipiwa Sh 150, 000.
Habari Leo