Mimi na familiya yangu ni watumiaji wa NHIF tangu ilipoanzishwa.
Kabla hata ya kupunguza hizo gharama zilizokuwepo kwa 60% bado kulikuwa na huduma nyingine tulikuwa tuna top up. Mathalani katika hospital ukilazwa, NIHF walikuwa wanalipa Tsh 5,000 kwa kitanda kwa siku. Lakini bei halisi ya kitanda katika hospital hiyo ni Tsh 10,000/- . Hivyo pamoja na kwamba hiyo hospital inahudumia wanachama wa NHIF, lakini ukitaka kulazwa wanakuambia u top up 5,000/-. Hili NHIF wanalijua vizuri kwasababu nilishakwenda ku report, na wakakili kwamba bei zao elekezi ziko chini wanatakiwa kuzi review.
Hivyo kwa baadhi ya vipimo na hata madawa. Unakuta kuna dawa ya India inauzwa Tsh 3,000/- na dawa hiyo imetengenezwa UK, inauzwa Tsh 15,000/-. Lakini watoa huduma wanakupata dawa ya India ya 3,000/- kwasababu ndiyo NHIF wamekubali kurefund ambayo kimsingi ni substandard.
NHIF kupuguza gharama za matatibu kwa watoa huduma ni mwiba mkali kwa sisi wanachama. Kitakachotokea ni kwamba Private hospitals nyingi zitaanza kukataa wagonjwa wa NHIF. Na zile zitakazokubali kutibu wanachama wa NHIF basi watapewa huduma substandard au kama mwanacahama atataka huduma standard basi itabidi a top up difference.
Kama kweli huduma za afya zimepungua hivyo kwa 60%, kwanini basi hata sisi wachangiaji tusipunguziwe kuchangia NHIF kwa 60%?! na badala yake tunaendelea kukatwa pesa ile ile? Huu uamuzi waliofanya NHIF ni wizi na dhuluma ya mchana kweupe kwa sisi wanachama.