Goodluck Mshana
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 1,271
- 1,119
Salamu kwenu wana JF,
Nimeona nikisemee hili humu JF kwani nina imani wahusika wa NHIF baadhi ni members humu. NHIF mmekuwa na utaratibu wa ajabu sana na kero kwa wateja wenu pale ambapo mteja anakosa huduma kwa kutokuwa na kitu kinachoitwa ' Verification Number '.
Hii ni namba ambayo hutolewa na NHIF makao makuu na hazitolewi hospitalini! Ni jambo la kuudhi na kusikitisha sana juzi niliposhuhudia mgonjwa wa Figo pale Muhimbili anakosa huduma kwakuwa hana hiyo number.
Hivyo alilazimika kufunga safari hadi headquarters NHIF. Nilitafakari mgonjwa huyu ambaye hata hakuwa na mtu wa kumuagiza huku akiwa hoi kajichokea. Huu sio uuwaji? Maana kama mtu anakatwa mshahara wake ama kwa namna yoyote ile tunatarajia apate huduma nzuri asiweze jutia pesa yake. Lakini kwa NHIF ni tofauti!
Jana usiku nikiwa TMJ hospital nahangaika kuhakikisha mtoto wangu anapata huduma ya haraka baada ya kuonesha kuwa na joto kali likiashiria homa au infection pia nilikosa huduma ya 'BIMA'!! Maelezo ya mtoa huduma ni kukosekana kwa Verification Number!! Huu ni upuuzi kabisa.
Naambiwa mpaka makao makuu ndio nitapewa hiyo namba then ndio huduma itaendelea?! Kweli? Muda huo ni saa sita usiku...sasa mtuambie makao makuu yapi yapo wazi muda huo kuweza ku verify hizo namba! Ni kwa bahati tu nilikuwa na emergency money mtoto wangu akapata huduma kwa cash!
Kitu ambacho sio sahihi kabisa maana ikifika mwisho wa mwezi huwa mnakata pesa zenu bila kupewa verification namba na wateja wenu! This mess should stop!
Lipo swala la kukosa mtandao wakati wa ku upload ama ku dowland taarifa za vipimo kwa wagonjwa. Endapo mtandao upo down basi mgonjwa atasubiri mpaka mtandao ukae sawa! Hapo pia kuna risk ya kupoteza uhai! Kwanini msiwaze kutengeneza Mobile Application (Apps) ambayo itakuwa user friendly kwa mawakala wenu kwenye kila hospitali?!
Hata kama mtandao upo chini bado wanaweza kutumia simu zao kutoa huduma na ku print out majibu ama taarifa zozote za kimatibabu. Hata hicho mnachoita verification number kingeweza kupatiwa ufumbuzi kwa kuingiza ID number kwenye App na ku update information.
NHIF mmebeba jukumu kubwa sana la kulinda afya za watanzania. Kwa kuendelea na mizaha hii kwenye maisha ya watu ipo siku tutapoteza watanzania wenzetu. Tuumize akili kuweza kuwa na huduma za kasi na kisasa.
Tuache umakini wa kukata kwenye mishahara tu...ongezeni umakini kwenye utoaji huduma! Habari ya centralization sio afya kwenye shirika lililomakini na lenye kutaka ufanisi kwenye utendaji wake!