Kero ya mawasiliano NHIF

Chagga King

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
1,826
1,045
Ni muda sasa nimekuwa nikipiga simu za NHIF ili kupata huduma ya haraka, nimepiga namba za mkoa husika moja (landline) inaita, mobile zote hazipatikani, nikaona isiwe tabu, nikapiga za makao makuu (HQ) Dodoma, zote ni landline, moja nikipiga naambiwa namba yao haijalipiwa, nyingine haipokelewi kabisa.

Hii ni mara ya pili, mwaka jana Dec nilipata changamoto kama hii ikabd niende ofisini kwao.

Sasa hizi namba zimewekwa kwenye website zenu za nini? Si kila wakati mtu anaweza kuja ofisini kwenu, mambo mengine yanahitaji immediate attention.

Kiufupi hapa nimenyimwa huduma hospitali, inanibidi nilipe cash, inaumiza kwa kuwa nachangia kila mwezi.

Kama mna namba tofauti ziwekeni kwenye ubao mtandao wenu tuzipate, kilingana ma ukubwa na unyeti wa hii taasisi, haipendezi wala kuleta afya ikiwa mnashida ya mawasiliano ya simu, na huwezi andika email kwa vitu vya uharakana.

Be informed
 
Kama RITA yaan sim yao huwa haipokelewi sijui wako busy au makusudi dogo alienda RITA kinondoni akakuta watu Wana miezi miwili cheti cha kuzaliwa miezi miwili hawajapata yeye wk tatu akaamua kurudi kukaa kimya kuna umuhim gani wa kuwa kidijitali.
 
hili ni tatizo, serikali ifuatilie changamoto za "vitengo vingi vya huduma kwa wateja" kumekuwa na shida sana kipata msaada, namba nyingi hazitumiki na nyingine hazipokelewi
 
Kama RITA yaan sim yao huwa haipokelewi sijui wako busy au makusudi dogo alienda RITA kinondoni akakuta watu Wana miezi miwili cheti cha kuzaliwa miezi miwili hawajapata yeye wk tatu akaamua kurudi kukaa kimya kuna umuhim gani wa kuwa kidijitali.
Vyeti ni online mkuu. Achana na kusumbuka na wazembe
 
Back
Top Bottom