ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,543
Eti ukimlipia mtoto kadi ya matibabu wanakupa risiti tu halafu unaambiwa kadi ufuate baada ya siku tisini na kwamba mtoto ataweza kuanza kutibiwa kwa kadi hiyo baada ya hizo siku tisini yaani miezi mitatu, hili limekaje?
Kwanini sasa pesa mnachukua? Mimi mwananchi masikini ninapojibana na kuwakatia watoto wangu bima ni kusudio langu ije inisaidie pindi ikitokea ugonjwa sasa mnaponiambia hadi siku tisini zipite sidhani kama ni kutenda haki.
Tuombe Wizara husika wajaribu kulifuatilia na kurekebisha kasoro hii. Huenda vikwazo hivi ndio vinafanya bado wazazi wengi washindwe kujiunga na mpango huo ambao ni mzuri isipokua wenye masharti magumu.
Tuombe NHIF pamoja na Wizara tusaidiwe wananchi kwa hili, mbona ukienda fungua account bank wanakupa ATM card yako kwa wakati muafaka?
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app