NHIF Kinondoni mnakera, Kadi za Bima hazitoki kwa wakati

Flight_controller

JF-Expert Member
Dec 4, 2018
246
396
May mwaka huu kadi yangu ya NHIF ilisitishwa kwa kuwa nimezidi miaka 18, hivyo mwezi uliofuata nikaamua kujinyima na kulipia bima kutoka kwenye kipato changu.

Baada ya malipo nikaambiwa nisubiri mwezi mmoja ndipo nichukue kadi yangu. Cha ajabu ni mara ya 3 sasa tokea mwezi uishe kila nikienda naambiwa njoo wiki ijayo au leta passport upewe kibali cha muda.

NHIF Kinondoni huu ni upuuzi badilikeni
 
Bima ya Afya hukatwa ukiwa huna tatizo na kikawaida hupaswa kuchukua mpaka miezi 3 kwa mwanachama mpya. Unajua maana ya BIMA? By the way ukiwa unaumwa then ukahisi garama zitakuwa kubwa ukakimbilia BIMA ni kosa kisheria kama ukiipatiwa chini ya miezi 3.
 
Mkuu hao NHIF mimi nafatilia card mwezi mzima unaisha sasa
 
Bima ya afya hukatwa ukiwa huna tatizo na kikawaida hupaswa kuchukua mpaka miezi 3 kwa mwanachama mpya. Unajua maana ya BIMA? By the way ukiwa unaumwa then ukahisi garama zitakuwa kubwa ukakimbilia BIMA ni kosa kisheria kama ukiipatiwa chini ya miezi 3
Nimekata nikiwa sina tatizo na hata sasa sina tatizo ila haijulikani matatizo yanakuja lini mkuu
 
Hivi kama ile ya kwanza imefungwa....unaruhusiwa kuendelea nayo?????
 
Mkuu ningependa kufahamu gharama za kukata bima ya NHIF Ni shingapi na Ni ya muda gani?
 
Mkuu ningependa kufahamu gharama za kukata bima ya NHIF Ni shingapi na Ni ya muda gani?
Mwaka mmoja kwa mtu aliye single n 192,000/= kwa makadirio kila mwezi n 16,000/= hiyo n kwa kiwango cha chini.
 
Mwaka mmoja kwa mtu aliye single n 192,000/= kwa makadirio kila mwezi n 16,000/= hiyo n kwa kiwango cha chini.
Asante Sana. Kwahiyo ukiwa na hiyo ya kiwango Cha chini Kuna hospital ukienda hautahudumiwa sababu Ni ya chini ?
 
Mbona sahvi wako fasta sana kutoa huduma zao, me nlipata kadi ya wife ndani ya wiki moja au kwako taratibu zipo tofauti?
 
May mwaka huu kadi yangu ya NHIF ilisitishwa kwa kuwa nimezidi miaka 18, hivyo mwezi uliofuata nikaamua kujinyima na kulipia bima kutoka kwenye kipato changu.

Baada ya malipo nikaambiwa nisubiri mwezi mmoja ndipo nichukue kadi yangu. Cha ajabu ni mara ya 3 sasa tokea mwezi uishe kila nikienda naambiwa njoo wiki ijayo au leta passport upewe kibali cha muda.

NHIF Kinondoni huu ni upuuzi badilikeni
Tatizo lako limetatuliwa au bado unasumbuliwa?
 
Yap...kuna vipimo, huduma za upasuaji na kulazwa hutopata.
Utapata huduma kulingana bima uliyokata .. kama kulazwa ukilipia 192,000 utakuwa na siku 30 za kulazwa mwaka mzima
 
IMG_20200823_181015_899.jpg
 
Haya mambo basi ni bahati tu.Mimi nilifuatilia chini ya mwezi mmoja nikawa nimepata.Dada mmoja ye hazikuisha Wiki mbili ikawa tayari.Sasa hizi za kufuatilia miezi mitatu sijui inakuaje
 
Back
Top Bottom