NHIF ingine ya TANESCO

pepsin

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
3,480
6,162
Service charge kwenye LUKU ilikuwa ni wizi,ni kero kubwa.Serikali ya awamu ya Tano imeondoa hiyo kero.Sasa hamna tena service charge.Kweli tunalipia umeme kadiri tutumiavyo.
NHIF pia kuna kero,wizi.Mtumishi analazimishwa kukatia bima watoto,mke/mme na wazazi pekee.Ikitokea mke na mme wote ni watumishi wa umma,basi wanufaika hubaki ni haohao,pande zote.Ina maana kila mnufaika atapata kadi mbili.Huu ni wizi maana mgonjwa hutumia bima mojawapo tu aendapo hospitali.
NHIF igeni mfano mzuri wa TANESCO kwa kuruhusu idadi fulani ya wanufaika pindi wanandoa wote ni wanachama wenu.
 
Mimi pia ni mwanachama wa NHIF, kuna utaratibu wa kuwasajili watoto wadogo chini ya miaka 18, gharama sh 50,400, utaratibu wa watu walio kwenye vikundi sh 76,800, Lakini duniani kote hakuna biMa holela kwamba ukiwa mfanyakazi utaweka mtu yeyote, lazima kuwepo na limiti hasa umri.kwa watoto,
 
Back
Top Bottom