NHC waombeni msamaha Watanzania walio wengi kwa kuwadanganya

NHC waombeni msamaha Watanzania walio wengi kwa kuwadanganya

State Propaganda

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2024
Posts
609
Reaction score
1,426
Tarehe 2 Septemba 2022, aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemia Mchechu alisema yafuatayo wakati akiwakilisha mipango waliyonayo NHC kwa wadau wa Sekta ya Milki Nchini ambapo
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limesema hivi karibuni linatarajia kuanza ujenzi wa 'nyumba za bei nafuu' katika eneo la Kawe Tanganyika Packers lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

"Kwanza tunaangazia suala la kutawanyika mji unakwenda mbali zaidi, lakini pili tuna-focus kwenye vertical expansion kwa hiyo katika hili, ingawa kulikuwa na ujenzi mwingi unafanyika kulikuwepo nyumba za ubia wa maghorofa yamejengwa, lakini tumesema wakati huu twende 'tukalenge watu wa kundi la affordable' housing ambazo tunakwenda kuanzisha katika eneo la Kawe, Tanganyika Parkers"......
......"Kama kuna mtu mwenye uwezo wa kununua bedroom zake tutamwambia ruksa, nunua na kuna mtu mwenye kununua studio bedroom tunamwambia ruksa nunua"......
....."Hataki hizi nyumba zije zizidi shilingi milioni 200, hiyo milioni 150 ndiyo target yetu 160, 170, inategemeana saiti mambo yatakayokuwa, hii ndio affordability tunaenda kuitekeleza. kwamba mtu mwenye milioni 50 atapata, mwenye 100 mwenye 150 atapata. Na niseme hii sio concept mpya sana niseme ni concert ambayo hapa katikati tulienda tukaisahau kuitengeneza."...

...."Lengo ni kwamba tunajikuta kwamba kwa sasa tuna Watanzania wanakaa mjini wanafanya kazi Mjini wakae hapo hapo Mjini na wanatembea kwenda maofisini kwao."
MWISHO WA KUNUKUHU.

Miaka minne (4) baadaye....

WhatsApp Image 2026-02-16 at 9.42.57 AM.jpeg

Nyumba SM 131, yenye vyumba viwili bei (pamoja na VAT) Tsh 478 Milion.
Milioni 478!!!! ndio affordable house!!!
BLOODY HELL!!

Huku si sawa na KUWATUKANA , tena MATUSI ya NGUONI kabisa kundi kubwa la Wananchi !!
ACHENI DHARAU AISEE..

Ni bora mngesema walengwa walikuwa ni VIBOPA/VIGOGO ama first class society.
 
Yaani hizi nyumba ni ghali sana. Je serikali inaweza kutwambia kwa nini apartments za NHC ni ghali kiasi hiki? kununua apartment ya vyumba 3 kwa sh milioni 700 au penthouse kwa bilioni moja kweli? Kununua Dar es salaam nyumba ni ghali sana kuliko nairobi
 
Nisaidie nipate mshangazi wa NHC basi
Mishangazi mnaipatapateje
Nami naipatapateje
 
Hapo unasemea almost 500 Mill .na ndio nyumba ya bei ya chini.
Tena utakuta iko kule juu ghorofa ya 15.

Si bora ununue kiwanja 100 Mill.
Ujenge nyumba Classic kwa 200 Mill.

Yaan nusu ya hiyo hela ya kununua 2 bedroom house unanunulia kiwanja kizur na unaaangusha bonge moja ya nyumba.
 
Usiyaamini Sana maneno ya viongozi wa bongo, ukisikia kiongozi bongo anasema "Itakuwa hivi sijui vile" basi kaa mguu nje na mmoja ndani...Kwa bei hizo ni mafisadi, wazee wa shortcut, matajiri wawili watatu, foreigners ndo wanaweza kuchukua hizo.
 
Yaani hizi nyumba ni ghali sana. Je serikali inaweza kutwambia kwa nini apartments za NHC ni ghali kiasi hiki? kununua apartment ya vyumba 3 kwa sh milioni 700 au penthouse kwa bilioni moja kweli? Kununua Dar es salaam nyumba ni ghali sana kuliko nairobi
Kuna jambo halipo sawa kabisa.
Hizo bei sio 'realistic' kabisa.
Samabamba na hilo, hayo mabadiliko ya bei ya awali wakati mradi unaanza kutoka TZS 50-200 Millions to TZS 400 Mil up to 1 Billion ni kwa maelekezo au manufaha ya nani????.
Tunaitaka serikali ije itoe ufafanuzi?
 
Hapo unasemea almost 500 Mill .na ndio nyumba ya bei ya chini.
Tena utakuta iko kule juu ghorofa ya 15.

Si bora ununue kiwanja 100 Mill.
Ujenge nyumba Classic kwa 200 Mill.

Yaan nusu ya hiyo hela ya kununua 2 bedroom house unanunulia kiwanja kizur na unaaangusha bonge moja ya nyumba.
exactly
 
Usiyaamini Sana maneno ya viongozi wa bongo, ukisikia kiongozi bongo anasema "Itakuwa hivi sijui vile" basi kaa mguu nje na mmoja ndani...Kwa bei hizo ni mafisadi, wazee wa shortcut, matajiri wawili watatu, foreigners ndo wanaweza kuchukua hizo.
Inachoumiza zaidi hizi nyumba ni za serikali ambazo zimejengwa na NHC kutumia kodi zetu, lakini gharama zake nafuu hata za zile Hamidu City Park kule Kigamboni
 
Hawana nia ya kuwajengea watu makazi ya bei nafuu !

Ova
 
Hawana nia ya kuwajengea watu makazi ya bei nafuu !

Ova

Alaf sijui nani kawadanganya kuwa NHC lazima iwe kwenye prime areas.

Kuna sehem Hapa Dar. pembezon mwa mji. Kama Wakiwekeza leo kwa kujenga phase 1 ya mradi wenye makaz ya maghorofa machache ya bei nafuu
Baada ya miaka 10. mrad utakuwa umewalipa vizur na kujenga phase 2 na 3.

Sasa wao wamepewa kiwanja bure. Alaf nyumba za kawaida tu na bei zimeshoot balaa.

Wanchenz sana
 
Wakijenga prime area wale wenzangu na mm wasahau
Mfano zile kota za manyanya pale uchafu mtupu zilitakiwa zipigwe chini zote wajenge kitu cha maana
Kodi wanayolipa pale ghetto zile kwa mwezi 10000 tu
Ni kweli waende pembezoni wWajenge watu nyumba za bei nafuu tu

Ova
 
Kuna madubwasha yao mengine yapo wazi.
Huko watu wanatoreshea pesa huko..
 
Back
Top Bottom