Nguvu Za dola tuu, uchaguzi ni kiini macho!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nguvu Za dola tuu, uchaguzi ni kiini macho!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPadmire, Nov 20, 2011.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,633
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndio hali halisi.

  Kama mtu ana uwezo wa kutumia Nguvu za dola kupata maradaraka, shida iko wapi? Hata akifanya ufisadi mchana kweupe nani atamfanya nini? Wadanganyika tutaishia kupiga kelele tu na kelele za mpita njia hazimnyimi mwenye nyumba usingizi.

  Kashfa za ufisadi haziwashtui tena viongozi au wagombea, wanajua kuwa wataiba kura tu,watachakachua matokeo tuu.

  Kila mtu ana kumbukumbu vizuri jinsi matokeo ya majimbo ya uchaguzi yalivyochelewesha, matokeo ya uraisi yalivyochezewa.

  Nguvu za dola (Polisi, JWTZ, Usalama wa Taifa) hawako independent kusimamia masilahi ya Taifa. Kila kitu ni shaghala baghala.

  Sana sana wale watanzania wenye upeo na wale viongozi wa upinzani wakisema wanaambiwa wanahatarisha amani, ooh ni wachochezi.
  Asilimia kubwa ya watanzania ni wajinga, yaani hawana elimu ya uraia, hawajui katiba, wako vijijini hawana taarifa, ni waoga, wana hofu, wako busy kutafuta angalau mlo mmoja wa siku,. umasikini umewafuna, hawa wanahitaji kukombolewa kifikra kwanza, wajue nani amewafikisha hapo walipo.

  Tulitegemea katiba ingekuwa mkombozi, ila sasa katiba ndo hivyo imetekwa na mafisadi. Sasa jamani tufanyeje watanzania???

  Tuchangiane mawazo, nani afanye nini, na huyo nani asaidiweje, lazima kuwe na nguvu ya umma nyuma ya huyo nani///
   
Loading...