Nguvu ya umma yaigeuka CHADEMA

MAFILILI

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,377
1,194
* Sasa kutumika kuung’oa uongozi
* Milioni 50/- za hongo zawatesa
* Ujumbe wa Dk. Slaa wapondwa

NA SHAABAN MDOE, ARUSHA

HALI si shwari ndani ya uongozi wa CHADEMA wilayani Arusha, baada ya kuzuka mvutano, wanachama wakitaka uchaguzi ufanyike ili kuwaondoa viongozi walio madarakani. Imeelezwa kuwa viongozi wa kata 18 wilayani humo walikaa kikao na kukubaliana viongozi wa mkoa waitishe uchaguzi, wakidai waliopo madarakani si halali. Akizungumza baada ya kumalizika kikao hicho, kwenye hoteli ya Palson, mjini hapa, Mwenyekiti wa kata ya Kati, Shubeti Rashid, alisema viongozi wote wa wilaya wamekuwa wakikaimu nafasi walizonazo kwa muda mrefu. "Wanakaimu nafasi hizo kwa zaidi ya mwaka mmoja unaotakiwa kikatiba," alisema. Aliwataja viongozi wanaokaimu nafasi hizo kuwa, Mwenyekiti wa chama hicho wa wilaya, Derick Magoma, Katibu wa uenezi wa wilaya, Gabriel Lucas, Mwenyekiti wa baraza la wanawake, Joyce Mukya, Katibu wake Margaret Olotu na wajumbe wanne wa kamati ya utendaji wilaya. Rashid alisema kukaimiwa kwa nafasi hizo kwa kipindi kirefu kumetokana na sababu za maslahi binafsi kabla ya kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Alisema licha ya uchaguzi kutangazwa miezi minne iliyopita ulifutwa bila maelezo. “Uchaguzi ulitangazwa miezi minne iliyopita lakini kuna tetesi watu walihongwa sh. milioni 50 ili uahirishwe kwa kuwa walidai wanachama waliokuwa wakigombea nafasi hizo ni mamluki na wasingekuwa na faida katika kuwawakilisha wanachama," alisema Rashid.

Alisema viongozi wa kata 18 wameweka maazimio kadhaa, likiwemo la kutoa siku saba ili uongozi wa chama hicho mkoa utoe tamko kuhusu uchaguzi.
Rashid alisema uongozi ukishindwa watatumia nguvu ya umma kuitisha uchaguzi.

Naye Mwenyekiti wa chama hicho kata ya Terati, Gerald Josephat, alisema nguvu ya umma itakayotumika itahusisha maandamano ili kushinikiza viongozi wasio halali kutoka madarakani kupisha uchaguzi ufanyike. Alisema pia watazifunga ofisi za mkoa hadi uchaguzi utakapoitishwa. Viongozi hao waliutaka uongozi wa mkoa kuhakikisha chama hicho kinakuwa na ofisi ya wilaya, kwani ni aibu kwa chama chenye wabunge watatu kukosa ofisi, licha ya kupokea ruzuku ya sh. 800,000 kila mwezi ambazo zingeweza kulipia kodi ya pango.
Walisema wabunge hao kwa umoja wao kama wasingekuwa na maslahi binafsi wangeweza kuchagia kupatikana ofisi na mahitaji mengine kama njia ya kukijenga chama hicho. Viongozi hao waliponda maagizo ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, aliyoyatoa kupitia ujumbe mfupi wa maneno, akiwataka waache kujadili mambo hayo. Kwa mujibu wa viongozi hao, ujumbe huo unaonyesha nia ya kuficha maovu na unaweza kisambaratisha chama hicho. Kikao hicho kimefanyika wakati Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe, akiwepo jijini hapa na kuna tetesi atakutana na viongozi hao kujadili suala hilo.

Source: Gazeti la Uhuru, Juni 27, 2011

DALILI ZA MVUA NI MAWINGU; CDM MKAE CHONJO!
 
mimi nilikwenda kutafuta gazeti la uhuru leo mpaka makao makuu sikulipata, viongozi wakanambia sasa hivi wanatoa online copy tu maana uraiani hakuna anayelinunua
 
mimi nilikwenda kutafuta gazeti la uhuru leo mpaka makao makuu sikulipata, viongozi wakanambia sasa hivi wanatoa online copy tu maana uraiani hakuna anayelinunua
Hata wanamagamba hawanunui? wanatoa online! mbona watakao visit huo mtandao ni wachache sana kama wapo na kwa mujibu wa wanamagamba huwa wanasema base yao kubwa ni vijjini, na sehemu kubwa ya vijijini hawajui hata mtandao.
 
Baada ya kukosa wanunuzi sasa hivi wanawatumia Clouds FM kufikisha porojo zao. Clouds huwa wanosoma habari zozote mbaya kuhusu chadema na kusifia magamba yao
 
Source: Gazeti la Uhuru, Juni 27, 2011

DALILI ZA MVUA NI MAWINGU; CDM MKAE CHONJO!
 
Taarifa hizi ni za uwongo na bahati mbaya sana mbinu mbovu zimefanywa kwenye maufaka wa meya iila zimejulikana kwa urahisi zinashuhulikiwa kwa ukaribu sana ameanza Lema leo kutoa tamko
 
Gamba mkubwa wewe na gazeti lako la udaku uhuru ndiyo mana limepotea mtaani,Usisahau zimebaki siku 11 kuwatoa mapacha watatu mana siku 90 ndiyo zinaisha hivyo,NAPE kimyaa aibu yake inakuja baada ya siku 90.ANGUKO LA CCM LIMETIMIA.
 
Ok. Lkn kuna hoja ya mapacha 3 wahame chama. Tukiweza hilo tutaigeukia cdm

kuna wakatikichwa kikubwa kinatumiaka kufikiri lakini kuna wakati unapenda kweli kutumia kile kichwa cha kidogo pale chini katikati
 
Lo watu Wa magamba wanataka kupoteza watu humu naomba viongozi Wa Chadema Arusha au kitaifa wakae chonju maana Magamba wamepta njia ya kuvuruga washindwe na walegee
 
Hivi hao walionukuliwa wapo na ni viongozi wa CDM huko Arusha. Isiwe tunazikanusha habari lakini hao watu wapo na wameongea halafu mkaanza kuiraru Uhuru kumbe wamenukuliwa kweli.
 
Hata wanamagamba hawanunui? wanatoa online! mbona watakao visit huo mtandao ni wachache sana kama wapo na kwa mujibu wa wanamagamba huwa wanasema base yao kubwa ni vijjini, na sehemu kubwa ya vijijini hawajui hata mtandao.

vijijini hela ya kula yenyewe shida ndio ije ya kununua gazeti, mtandaoni ndio kama likiletwa hapa JF unaweza kulisoma
 
Hivi kuna mtu mwenye akili timamu anaweza akatoa hela yake kununua kipeperushi kinachoitwa uhuru?
 
Back
Top Bottom