Nguvu ya Umma itaishinda CCM

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,330
33,962
Ibara hii ya Nane ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania ndiyo msingi wa Falsafa ya CHADEMA ya "Nguvu ya Umma". Nguvu ya umma inayosimamiwa na CHADEMA si nguvu ya vurugu bali ni mkakati mahsusi wa kurudisha serikali ya watanzania mikononi mwao kwa lengo la kutumia rasirimali walizojaaliwa na Mwenyezi Mungu kujiletea maendeleo yao na ya vizazi vijavyo.

Serikali na watu Sheria ya 1984 Na.15 ib.6
IBARA YA NANE YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuatamisingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo

(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikaliitapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwawananchi kwa mujibu wa Katiba hii;

(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;

(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;

(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao
kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

Wapinzani wa falsafa yetu ya nguvu ya Umma mara nyingi kwa kutokuelewa msingi wa falsafa hiyo hudhani kwamba inatokana na wazo kwamba nguvu ya Umma ni nguvu ya kuchukua madaraka kwa nguvu. CHADEMA msingi wa falsafa yetu inatokana na Ibara hiyo ya nane ya katiba ya Tanzania ambayo inaelekeza jinsi serikali inavyotakiwa kuweka madarakani na jinsi gani inatarajiwa kuhudumia wananchi.

Kwa bahati mbaya sana serikali iliyopo madarakani chini ya CCM imeshindwa kabisa kukidhi vigezo vinavyotajwa na kifungu hicho cha katiba. Sisi CHADEMA tunachofanya ni kuwahimiza wananchi kukumbuka kwamba Katiba yao (pamoja na udhaifu wake) inatambua kwamba madaraka ya serikali yanatokana na wananchi.

Nguvu hii ya Umma ambayo kwa muda mrefu sana imekuwa ikipuuzwa na CCM ndiyo sisi tunaitumia kutaka kuijenga Tanzania mpya. CHADEMA inaamini kwamba vyama vya siasa ni vyombo tu vya kutafsiri mahitaji ya wananchi na kuyatimiza lakini vyama hivyo vinapata ridha ya kufanya hivyo kutoka kwa wananchi wenyewe.

Nguvu ya Umma ndiyo itakayoipeleka CHADEMA madarakani, ndiyo itaiwezesha kutenda na kusimamia sera zake, ndiyo itakuwa msingi wa serikali ya CHADEMA ikiwa madarakni. Nguvu ya Umma ni mahitaji ya watanzania,matarajio yao na tunu zao ambazo CHADEMA imefanikiwa kuzitafsiri, na watanzania wameamua kwa dhati kabisa kuiunga mkono CHADEMA kwenye kuirudisha serikali mikononi mwa wananchi.Nguvu hii ya Umma haiwezi kuzuiwa na CCM kwani ndiyo wananchi wenyewe!!
 
Back
Top Bottom