Nguvu ya UKAWA imeonekana kwa 70% ya wananchi kususia uchaguzi

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Nguvu ya chama chochote cha siasa huonekana kutokana na uwezo na umahili wa kuishawishi jamii kukubaliana na mawazo na mipango yake. Ukikuta chama kinapuuzwa au kupata mwitikio mdogo pindi kinapoitaka jamii kukiunga mkono, jua chama hicho ni mfu, au ni chama cha viongozi wa juu pekee yake.

Kwenye uchaguzi uliopita, katika majimbo ya Singida Kaskazini na Songea Mjini jumla ya wapiga kura 220,359 walitarajiwa kupiga kura lakini ni wapiga kura 69,898 tu waliojitokeza, hiyo ni sawa na asilimia 31.7 ya waliotarajiwa, ndiyo kusema karibu asilimia 70 ya wapiga kura hawakujitokeza, kwa lugha ya kisiasa asilimia 70 wameungana na vyama vya upinzani UKAWA kususia uchaguzi.
Matokeo Jimbo la Singida Kaskazini msimamizi; waliopinga kura 22,298 kati ya 91, 518 ya waliojiandikisha, watu 69,220 ambao ni 76% hawakupiga kura.

Jimbo la Songea Mjini; waliopinga kura 47,600 kati ya 128,841 ya waliojiandikisha, takribani watu 81,241 ambao ni sawa na 63% hawakupiga kura.

Asilimia 70 ya watu kususia si jambo la kubezwa, hii inaonyesha ni jinsi gani vyama vya upinzani vilivyo na nguvu ya USHAWISHI kwa wananchi au hawakubaliani na mwenendo wa utawala unavyoendesha siasa nchini. Ina maana 70% hawakubaliani na utawala wa Magufuli? Hiyo ni topic nyingine.

Matokeo haya yametoa funzo si kwa watawala pekee bali kwa NEC na Chama Cha Mapinduzi kuwa, uonevu, unyanyasaji wa wanachama wa vyama vyenye itikadi tofauti na chama tawala haujengi Umoja bali unaligawa taifa.

Matokeo haya yameonyesha kuwa, wananchi walio wengi (70%) hawana imani na Tume ya Uchaguzi, hawana sehemu nyingine ya kutolea dukuduku lao, wameona leo wawaonyeshe watawala na NEC kwa njia ya kususia uchaguzi, kuwa hawapendi kunyanyaswa, hawapendi kudhulumiwa haki yao, kuwa wanataka uchaguzi ulio huru na wa haki, kuwa wanataka utawala bora wa sheria, na kuwa wanataka haki sawa kwa wananchi wote.

Hilo ndilo somo KUU la Matokeo ya uchaguzi uliopita, mwenye akili ataelewa mwenye kubeza na aendelee kubeza.
 
Nguvu ya chama chochote cha siasa huonekana kutokana na uwezo na umahili wa kuishawishi jamii kukubaliana na mawazo na mipango yake. Ukikuta chama kinapuuzwa au kupata mwitikio mdogo pindi kinapoitaka jamii kukiunga mkono, jua chama hicho ni mfu, au ni chama cha viongozi wa juu pekee yake.

Kwenye uchaguzi uliopita, katika majimbo ya Singida Kaskazini na Songea Mjini jumla ya wapiga kura 220,359 walitarajiwa kupiga kura lakini ni wapiga kura 69,898 tu waliojitokeza, hiyo ni sawa na asilimia 31.7 ya waliotarajiwa, ndiyo kusema karibu asilimia 70 ya wapiga kura hawakujitokeza, kwa lugha ya kisiasa asilimia 70 wameungana na vyama vya upinzani UKAWA kususia uchaguzi.

Asilimia 70 ya watu kususia si jambo la kubezwa, hii inaonyesha ni jinsi gani vyama vya upinzani vilivyo na nguvu ya USHAWISHI kwa wananchi au hawakubaliani na mwenendo wa utawala unavyoendesha siasa nchini. Ina maana 70% hawakubaliani na utawala wa Magufuli? Hiyo ni topic nyingine.

Matokeo haya yametoa funzo si kwa watawala pekee bali kwa NEC na Chama Cha Mapinduzi kuwa, uonevu, unyanyasaji wa wanachama wa vyama vyenye itikadi tofauti na chama tawala haujengi Umoja bali unaligawa taifa.

Matokeo haya yameonyesha kuwa, wananchi walio wengi (70%) hawana imani na Tume ya Uchaguzi, hawana sehemu nyingine ya kutolea dukuduku lao, wameona leo wawaonyeshe watawala na NEC kwa njia ya kususia uchaguzi, kuwa hawapendi kunyanyaswa, hawapendi kudhulumiwa haki yao, kuwa wanataka uchaguzi ulio huru na wa haki, kuwa wanataka utawala bora wa sheria, na kuwa wanataka haki sawa kwa wananchi wote.

Hilo ndilo somo KUU la Matokeo ya uchaguzi uliopita, mwenye akili ataelewa mwenye kubeza na aendelee kubeza.

Wa Songea walikuwa busy na mashamba yao. Uchaguzi kipindi hiki cha mvua siyo deal kule. We jipe moyo tu eti nguvu ya UKAWA. Kule huo ukawa haupo kabisaaaaa
 
...Asilimia 70 ya watu kususia si jambo la kubezwa, hii inaonyesha ni jinsi gani vyama vya upinzani vilivyo na nguvu ya USHAWISHI kwa wananchi

I thought vyama karibia vyote vya ''upinzani'' vilishiriki isipokuwa CHADEMA, vikiongozwa na le professeri Lipumba. Bila shaka msukumo huu wa kususia uchaguzi ni kwa kuwa CHADEMA hawakushiri. Lakini hii turn-out ndogo inaashiria kwamba na wana CCM hawakwenda kupiga kura au siku zote CCM imekuwa ikichakachua kwa kiwango cha kutisha sana?
 
Nguvu ya chama chochote cha siasa huonekana kutokana na uwezo na umahili wa kuishawishi jamii kukubaliana na mawazo na mipango yake. Ukikuta chama kinapuuzwa au kupata mwitikio mdogo pindi kinapoitaka jamii kukiunga mkono, jua chama hicho ni mfu, au ni chama cha viongozi wa juu pekee yake.

Kwenye uchaguzi uliopita, katika majimbo ya Singida Kaskazini na Songea Mjini jumla ya wapiga kura 220,359 walitarajiwa kupiga kura lakini ni wapiga kura 69,898 tu waliojitokeza, hiyo ni sawa na asilimia 31.7 ya waliotarajiwa, ndiyo kusema karibu asilimia 70 ya wapiga kura hawakujitokeza, kwa lugha ya kisiasa asilimia 70 wameungana na vyama vya upinzani UKAWA kususia uchaguzi.

Asilimia 70 ya watu kususia si jambo la kubezwa, hii inaonyesha ni jinsi gani vyama vya upinzani vilivyo na nguvu ya USHAWISHI kwa wananchi au hawakubaliani na mwenendo wa utawala unavyoendesha siasa nchini. Ina maana 70% hawakubaliani na utawala wa Magufuli? Hiyo ni topic nyingine.

Matokeo haya yametoa funzo si kwa watawala pekee bali kwa NEC na Chama Cha Mapinduzi kuwa, uonevu, unyanyasaji wa wanachama wa vyama vyenye itikadi tofauti na chama tawala haujengi Umoja bali unaligawa taifa.

Matokeo haya yameonyesha kuwa, wananchi walio wengi (70%) hawana imani na Tume ya Uchaguzi, hawana sehemu nyingine ya kutolea dukuduku lao, wameona leo wawaonyeshe watawala na NEC kwa njia ya kususia uchaguzi, kuwa hawapendi kunyanyaswa, hawapendi kudhulumiwa haki yao, kuwa wanataka uchaguzi ulio huru na wa haki, kuwa wanataka utawala bora wa sheria, na kuwa wanataka haki sawa kwa wananchi wote.

Hilo ndilo somo KUU la Matokeo ya uchaguzi uliopita, mwenye akili ataelewa mwenye kubeza na aendelee kubeza.
Wamepata nini baada ya kususia au huo ndiyo ushindi?
 
Lazima tukubali Kuna tatizo sehemu....
Hela yingi zitatumika bila tokeo
 
Hata vyama vya upinzani visiposusia uchaguzi mkuu ujao idadi ya wapiga kura itapungua mno. Ile morali haipo tena kila kona ni kukatishana tamaa sio chama tawala wala wapinzani so bora kusaka pesa hadi jumapili kuliko kwenda kusimama kwa masaa tele kupigania maslah ya watu wachache
 
Back
Top Bottom