Nguvu ya msemo "HAPA KAZI TU" imeishia wapi?

Nguvu ya msemo "HAPA KAZI TU" imeishia wapi?

Wewe huoni hapa kazi inavyoshamiri?Hii hapa kazi si yakubahatisha,ndiyo maana hapo awali zilipigwa na push up.
 
Wakati utawala wa awamu ya 5 chini ya Magufuli ulikuja na kauli mbiu ya 'HAPA KAZI TU'

Watu maeneo mbali mbali nchini walitumia hii kauli mbiu kwa kasi sana,mitaani ukikutana na watu ni kusema hapa kazi tu hata wale wasio na kazi walijinasibu na hapa kazi tu.

Rais mwenyewe wakati anaanza kila hotuba yake lazima aweka kibwagizo cha "Chini ya serikali yangu ni kazi tu"

Wanyonge wakafurahia na kuwa na natumaini ya unafuu wa maisha hivyo wakazidi kuipamba kauli ya hapa kazi tu wakati kazi zenyewe hakuna
Lakini siku za hivi karibuni naona hii kauli mbiu kupotea na sasa kila mtu analia na kauli ya "Hali ngumu kiuchumi/Maisha" watu wasiojulikana,Ukosefu wa Uhuru wa kutoa maoni dhidi ya serikali,kuokotwa kwa maiti kwenye fukwe za bahari ,wawekezaji wa nje kulia na Sera mbovu za uwekezaji nchini,watumishi wa umma kutoongezewa mishahara na Shida nyingine nyingi
Neno HAPA KAZI TU linazidi kupotea kuanzia mitandao hadi mitaani
Nani atashabikia kusema HAPA KAZI TU ili hali hajui mlo wa siku ataupataje,ajira hakuna ,wenye ajira wanakatishwa tamaa ,Nani atafurahia HAPA KAZI TU.

N.B Chini ya utawala wa Magufuli na CCM tusitegemee maendeleo ya kiuchumi na nchi kiujumla
OVA[emoji41] [emoji41] [emoji41]
Imepotea kama kauli ya "Niombee" cku hz haskiki akisema tumuombee. Au maombezi yametosha...
 
Umesahau kua kauli ilipo sasaiv mtaani na mitandaoni ni "pambana na hali yako"!?
Ukishafanya kazi tuu, yaani kazi isiyo na tija, kinachofata ni kauli isemeyo pambana na hali yako.Kwa mfano kama mazao yako hayauziki au bei ni ndogo sana,ushauri pekee toka kwa wale wasiolima ni kukueleza kula tu mwenyewe hilo si zao la biashara.
 
Mkuu kashasema yalikuwa ni Maneno ya kampeni.....sasa kampeni zimeisha tuendelee na hali zetu paka kampeni zitakapokuja tena
 
Umenifanya nikumbuke enzi hizo chuo mwaka wa kwanza nasoma Business Law, hapa naona hii kauli ilikua INVITATION TO TREATY. Jamaa alituita kumpigia kura kwa kauli ilokua na hamasa ya utendaji kazi na kuleta maendeleo na tukaingia mkenge bila kuchunguza kama alikua na sera to implement huu msemo.
Makosa si yake bali ni ya waTZ tuliomchagua. Alichotaka kashapata. 2020 we have another chance to amend our mistakes but I bet kwa mwendo huu ikifika 2019 zile 50M kila kijiji zinatoka na atachaguliwa tena.
Eti "umenikumbusha wakati nasoma Business Law"...Nimecheka sana. Utakuwa ni lile kabila la jamaa zangu wala ndizi na panzi.
 
Tanzania ya viwanda sijui imepotelea wapi..si isikii kabisa!!
Subiri kwanza! Waziri wa viwanda anahangaikia soko la mbaazi huko India ili mbaazi ya Tanzania ikatumike kama mali ghafi katika viwanda vya India. Akimalizana na mbaazi ataimarisha soko la biskuti kutoka India hapa nchini. Ndiyo biashara enyewe hiyo!
 
Hakuna mtanzania mwenye furaha kila sehem ukipita watu wana nyuso za huzuni huyu ni rais wa ajabu haijawahi tokea
 
Kiukweli sasahivi ukionekana unasema hapa kazi tu itaonekana Mnafiki sabab mambo yapo wazi kabisa kaulimbiu haina uhalisia Na mambo ya sasa
 
Kanikera kubana mshahara!!!!
Amekukera kubana mshahara!!! Kumbe nawewe mtumishi was serikali!!!!! Hongera ila nkuulize hujadanganya miaka maana sasahivi wanakuja Na ajenda mbalimbali mpaka malipo ya mishahara kwenye bajeti yasome bilioni 150 badala ya 550
 
Amekukera kubana mshahara!!! Kumbe nawewe mtumishi was serikali!!!!! Hongera ila nkuulize hujadanganya miaka maana sasahivi wanakuja Na ajenda mbalimbali mpaka malipo ya mishahara kwenye bajeti yasome bilioni 150 badala ya 550
Sijadanganya umri! si hata vyeti vya kumaliza form four (leaving) si wanaonesha mwaka wa kuzaliwa!!!
 
Back
Top Bottom