Nguvu ya mitandao ya kijamii, mijini na vijijini

Jack Daniel

JF-Expert Member
Sep 23, 2021
2,151
10,395
Habari wanajamvi.,

Tupo kwenye ulimwengu wa kisasa, ambao Teknolojia imechukua nafasi kubwa kwenye Dunia na kuteka baadhi watu na kujikuta nusu ya maisha ya wengi yametawaliwa na Teknolojia.

Faida ni nyingi si haba, mitandao ya kijamii inatuletea ushahidi namna watu wengi wanavyofanikiwa kupitia huko.

Mifano ni mingi sana, watu wengi wanamiliki simu janja, ili kuendana na wakati, leo hii Diamond platinum akiachia ngoma mpya, hata yule kijana anayeishi Kijiji cha mara moja Liwale huko, anapata ngoma huku akiipakua kwa ubora anaoutaka yeye .

Hizi siyo enzi za Msondo ngoma kuwa lazima ngoma uisikie kupitia RTD au ukatafute Kanda (Cassette) ili uburudike.la hasha.

Leo hii huwezi kumbania msanii ili wimbo usichezwe kwe radio na TV, eti ili asitangazwe, unaweza kujisumbua tu kwani Ngoma inaweza kupenya na kusambaa sehemu nyingi huku muhusika akipata shows nyingi ambapo tayari anakuwa na followers Kila mahali.

Biashara, matangazo na mambo kadha wa kadha yanafanyika kwa njia ya mtandao, huku utitiri wa online TV ukiwa haupo nyuma, lengo ni kujihakikishia kipato kinatengenezwa kwa njia zozote zile ili mradi mtu havunji sheria.

Kwasasa mambo ni mukide Kila mtu kwa namna yake anaenjoy atakavyo awe kwenye gari, awe njiani ana walk kikubwa ni earphones tu mtu unaenda/kurudi kazini Ukiwa unasikiliza Ngoma ya cardi B, iliyotoka Leo kana kwamba unaishi viunga vya Nevada state, kumbe unaishi Bunju B.wiki iliyopita nilishangaa nikiwa mkoa Mmoja hapa nchini nikikutana na kijana, ambaye, anasema hajawahi kufika Dar es salaam akiimba wimbo wa Kendrick Lamar, humble.

Iko hivii, wakati Gari langu limepata pancha, nilisogea Hadi sehemu fulani palipochangamka ili kutafuta msaada , ndipo nilipopark gari huku vijana ambao Wala hawakutaka malipo wakinisaidia kupiga jeki , ndipo nilipomsikia dogo fulani akiimba, be humble, be humble,

Kwanza nilishangaa Kisha nikamuuliza , unaujua huo wimbo .
Akajibu anajua kaimba fulani na kamsubscribe huyo msaanii , akionesha anamfuatilia sana , akinionesha Baadhi ya nyimbo nyingine, kupitia simujanja yake.

Ndipo nilipoiamkia mitandao ya kijamii kwa Mara nyingine huku, nikiwaza kuwa , watu wengi wanaoishi Dar hujifanya unajua wanajua vitu vingi kuliko wa mikoani huko ndani ndani, ndugu yangu utawapita vitu vinavyofundishwa shuleni ila siyo umbea wa mitandaoni,watu wanamfahamu Carry mastori na Kila siku lazima waingie insta wajue kapost Nini.

Huko unakoita Madongo kuinama, Ukiwa Sinza ukiwakashifu wenzio ukijiona ukijiona mjanja, ni kwamba watu wanazijua ligi zote maarufu, huku vijana wakibet bila wasiwasi, nilishangaa sana, mtu analala kibanda Cha nyasi lakini ana simu janja huku Akiwa na apps zote za kijanja.

Hongera umeme wa REA na Sundarsolar, huku mitandao ya kijamii ikiwa haichagui Wala haibagui.

Wengi wetu
Tumekuwa addicted na mitandao ya kijamii kiasi Cha mtu kujinyima baadhi ya vitu ili awe angalau na MB kadhaa ili atembelee kunako social media, hili Mimi mwenyewe ni muhanga yaani siwezi kumaliza siku bila kutembelea Jamiiforum, siwezi.

Siyo kwamba haiwezekani ila ni kitu ambacho nimeshakuwa na uraibu nacho, kwa asilimia fulani nimejifunza mengi kupitia jamii forum, nikitembelea kila jukwaa huku nikifurahia namna yalivyopangiliwa vyema.unachagua tu unataka kuenjoy jukwaa gani,
Au hata kuchungulia kupitia timeline

Nirudi kwenye negative
Sasa basi , kuoneana, kudharauriana, mtu kukuandika vibaya kwasababu anazozijua yeye, imekuwa ni kawaida tu, kama vile mateso ya mlevi aliyetoka kuifurahia pombe muda si mrefu, huku matokeo yake hayo yakimnyanyasa zaidi.

Super handsome men na Beautiful weman wote, wamekimbilia huko, unajua kwanini, ni sura na mionekano yao, Yaani mtu akijikuta yupo hivyo kama si kukimbilia usanii wa muziki basi ataenda kwenye uigizaji, akiamini atatoka au kutoboa na hii ipo ulimwenguni kote huku ikichangia
Kudumaza tasnia husika.mbaya zaidi watu wameharibika kabisa, yaani mtoto wa kiume anakurembulia na kuombaomba vitu kimahaba kabisa , wahudhuriaji wa night clubs wanajua haya, ninayozungumza.

Huku mamende na wanaume wenye vinasaba hivyo, wakivutiwa kabisa na wanaume wenzao, tena mtu mkuyenge unasimama kabisa kwa mwanaume mwenzake. Dah
Dunia simama nishuke, wala sihitaji unirudishie nauli.

Lakini na wale sura ngumu nao hatupo nyuma, kwani mitandao imetuweka kwenye makundi yetu huku Kila mtu akinufaika kwa namna yake, wapo walioingia kwenye uchekeshaji, huku wakipata wafuasi na kujizolea umaarufu.

Wengine kupitia sura zao wamekimbilia boxing, yaani hapa panachekesha sana, mtu akishajiona kavimba mwili akienda gym miezi kadhaa basi anajiona anaweza, mbaya zaidi anashawishiwa na watu au kundi fulani linalompa moyo, ili tu watengeneze pesa, huku mhanga anayejiita bondia akishindwa kufanya calculations za UHAI wake.
Kwa kutaka kuwaridhisha wengine.

Ni mambo mengi sana ya hatari yanafanyika, huku serikali ikiingilia Kati kwa Baadhi ya wanaovuka mipaka na kutumia mitandao vibaya, yote kwa yote, ni lazima kuwa makini na unachopost,kwani ulimwengu unajua haraka sana , na kujikuta either unajiweka au kumuweka mtu matatani.
 
cc: Unamsema MANDONGA AU?
 
Hongera umeme wa REA na Sundarsolar, huku mitandao ya kijamii ikiwa haichagui Wala haibagui.
Hii yote ni jitihada za Jakaya. Umeme vijijini,Mkonga wa Taifa, kubadili mfumo wa kurusha matangazo ya televisheni toka analogies(minara) kwenda digital (Satellite) na shule za sekondari za kila kata zimesaidia sana kubadili maisha na mtazamo vijijini.

Changamoto inabaki kuwa matumizi sahihi ya hivyo vitu. Vijijini wanaiga kila kitu.
 
Umekuja kumjadili mandonga
 
Back
Top Bottom