The Retired Planner
Senior Member
- Sep 22, 2015
- 188
- 241
Wasalaaaaaaam Wanajamvi
Leo nimeona nifunguke kwa upande huu, kama “heading” yangu inavyosema ili kusaidia wanajamvi wenzangu kuondokana na hali hii ngumu ya kimaisha ambayo kwayo sisi watanzania tulio wengi tumekuwa tukilalamika kila uchwao ya kwamba “ “MAISHA HAYASOGEI”
Nianze kwa kusema, wengi wetu tumekua tukisikia kelele za wadau mbalimbali kuhusu kujikwamua kiuchumi kwa kufanya Biashara au ajasiriamali na kuondokana na dhana ya KUAJIRIWA. Sikawii kusema wengi tumekuwa tukiyatupilia mbali mawazo hayo kwa sababu 1 au 2 hivi; utasikia mtu akisema
1. Mtaji wa hiyo Biashara/Ujasiriamali nautolea wapi wakati mimi ndio kwanza nimemaliza chuo/shule au;
2. Niache kazi (Kuajiriwa) wakati bado sijajipanga?, natafuta mtaji kwanza halafu baadae nianzishe Biashara yangu
Ngaja niseme hivi wadau, tunajicheleweshea wenyewe hayo maisha mazuri ya asali na maziwa. Mafanikio yangu ama yako yapo kwenye maamuzi yako binafsi. Ni mimi au wewe wa kuamua sasa nahitaji kuwa na pesa kwa kiasi gani.
Ajira tulizonazo zinatusaidia tu kupata pesa ya kuendesha maisha tena yale ya kawaida sana. Mwezi haujaisha lakini kamshahara kako kamekatika siku nyingi sana kutokana na majukumu tuliyonayo kifamilia na kijamii kwa ujumla na kama ofisi yako haina yale magumashi wanayopigaga wenzetu, basi madeni yanaanzia hapo mpaka mshahara mwingine utakapokuja. Mwisho wa siku mshahara wako unakuwa ni nusu kulipia madeni na nusu kukusogeza tena kwenye nusu nyingine ya mwezi ujao.
Hali hii ya maisha itaendelea hivyo mpaka pale utakapofanya MAAMUZI wewe mwenyewe(kwa ku‘resign’) ama kwa kusaidiwa na mwajiri wako (kwa maana ya kufukuzwa kazi). Kwani hata mwajiri wako akikuongeza mshahara bado matumizi yako pia huongezeka. Hivyo hali huendelea kuwa ile ile.
Maamuzi ya kile unachokihitaji kwa maisha bora ukijumlisha na jitihada stahiki kwenye hayo maamuzi, amini usiamini utaona ni kama ndoto kwenye maisha yako. Nina mifano kadhaa ya marafiki zangu ambao walifukuzwa kazi na kwa kupitia hali hiyo walijua hakuna namna nyingine ya haraka ya kuendelea kuwaingizia kipato ili familia zao zisione hilo “gap”. Basi WAKAAMUA kungia kwenye Biashara na kufanya yale mambo ambayo kabla walikuwa wakiyapenda na kufikiria kuyafanya lakini kwa sababu ya Ajira zao walishindwa na kudhani walistahili kutafuta mtaji kwanza.
Hivi leo hakuna hata mmoja ambaye utamwambia arudi kuajiriwa akakuelewa unampigia stori gani. Kimsingi walifanya MAAMUZI na wanayaona matunda ya MAAMUZI yao. Haya sasa tuachane na hizi stori nyingi, nashauri kuanzia muda huu ambao umemaliza kusoma hizi hadithi ambazo wengine watadhani ni zile za aina ya kusadikika, Ufanye UAMUZI.
Sijakwambia uache kazi (kwa wewe uliye kazini kwa sasa), na kwa wewe ambae ulikuwa unatafuta kazi achana na mawazo hayo, naomba vile vitu ambavyo ulikuwa unafikiria kuvifanya na ukadhani vinahitaji mtaji ili kuviaanza vianze sasa. Kinachohitajika hapa ni MAAMUZI na sio Mtaji.
Kama unadhani haiwezekani, mimi nakwambia INAWEZEKANA na naomba unitafute kwa ushauri zaidi endapo unadhani unahitaji ushauri zaidi. Tanzania hii ni yetu na ninakuomba kwa moyo wote kabisa tuijenge kwa pamoja.
MAAMUZI + JITIHADA = MAFANIKIO