Nguvu ya kitanda

Joined
Oct 9, 2017
Posts
23
Reaction score
48
%"NGUVU YA KITANDA" %

Utafiti umeonyesha baadhi ya vitu vilivyosababisha ndoa za babu zetu zidumu ilikuwa babu na bibi kulala pamoja kwenye vitanda, ngozi za wanyama au mikeka yenye ukubwa usiozidi futi 2.5. Umbali wa futi 2.5 uliwawezesha wanandoa kuwa pamoja na kugusana usiku kucha.

Hiyo iliwalazimisha waongee hata kama wamegombana mchana, maana bila kusema sogea huko huwezi kupata nafasi ya kulala. Baridi ilivyokuwa inaongezeka kunapokaribia kucha iliwalazimisha wasameheane hata bila ya kuombana samahani, maana kugusana kule kuliwapa joto lililokuwa linafuta lenyewe makosa yote waliyofanyiana mchana na kuanza upya.
Vitanda vyetu vya 6 x 6 vinakwenda anti-clockwise na kazi iliyokuwa inafanywa na vitanda vya akina babu.

Vitanda vyetu havina ubavu wa kufuta makosa ya wanandoa waliyofanyiana mchana. Kila mtu anakuwa kwenye kona ya 6x6 na kujisikia aibu kuanza kumgusa mwenzie, nani aanze kupandisha mguu kwenye paja la mwenzie wakati kulikuwa na ugomvi?

Ngoma inakuwa droo hadi asubuhi na ugomvi ukiwa palepale na kila mtu akijfanya nunda wa kukataa kujishusha kwa kusema samahani ama kumpapasa mwingine.

Rudisheni vitanda vyenu kwa fundi seremala avipunguze viwe 3 x 6 ili viweze kuwasuluhisha wanandoa mnapokoseana sio kwenda kwa mshenga, shoga, wazazi, majirani kutafuta suluhu.
 
Hoja imeisuka vizuri , vile vitanda vya zamani kiboko kwani vinapatanisha watu kiaina .
 
Sio kweli kuwa babu zetu walikuwa wanalala na wake zao kitanda kimoja. Jamii nyingi za Kibantu wanaume walikuwa wana sehemu/tengo/chumba au nyumba ya baba tofauti na mama tafauti. Kukutana kwao ni pale wanapotaka kushiriki tendo na wakimaliza mama anarudi kwake. Hiyo ilijenga heshima kwa baba tofauti na nyinyi wa sasa hivi mke hata akiwa bleed au kikohozi mnalala pamoja ndo chanzo cha wanaume kukosa unadhifu na wanawake kuwapima waume zao nguvu. Ni kosa kubwa sana mfano mke amejifungua halafu mwanaume unang'ang'ana kulala kitanda kimoja na mtoto.
Wazungu wanatuvurugia tamaduni zetu kwa staili zao za maisha.
 
Mkuu hakuna mzungu anayelala kitanda kimoja na mtoto.
Mtoto analala kwenye crib yake.
 
6x6 maeneo ya joto bado tabu tupu, kitu 8x8 angalau... Maswala ya kusameheana ni maelewano tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…