Gospel Preacher
JF-Expert Member
- Jan 17, 2018
- 233
- 264
Dhambi ni uasi, kila lisilo jema ni dhambi, dhambi ipo isiyo ya mauti,
Watu wengi wamewaza kama dhambi haina nguvu katika maisha ya mtu, lakini ukweli ni kwamba dhambi ina nguvu saaana kuliko uweza wa mwanadamu, (kama akiwa hana Mungu.)
Unaweza kuwaza kuwa kuna watu wanahukumiwa kwa makosa mabaya sana mfano mtu mzima kumbaka mtoto wa miaka mitatu, kesi hizi zipo nyingi sana,mbali na mashariti ya waganga wa kienyeji lakini mtu huyo anakuwa ameshikwa na kamba za dhambi.
Dhambi inanguvu sana kwasababu nyuma ya dhambi(tendo) kuna roho chafu (mapepo) yanayokusimamia kuitekeleza dhambi hiyo hivyo huwezi kushinda usichokiona ni mpaka ukipambanishe na kisichoonekana chenzake ili viumanie huko kusikoonekana. Na ndio maana kuna mambo huyapendi lakini unayafanya.
Mungu ni wa rehema huwa hamhukumu mtu mpaka dhambi zake ziongezekee na zijae na kufurika kwenye kikombe cha uovu then mabaya yatamoata mtu huyo. Unaweza ukawa unashiriki dhambi ya uzinzi,uasherati,ufiraji, wizi,mauaji,husda,uchongezi,fitina,ufisadi na n.k lakini still bado unapumua na upo hai, hii haimaanishi kama Mungu amekupbdelea NOO hapana ni kikombe cha uovu wako hakijajaa bado, siku kitakapo jaa utafanya kitu kidogo tuu na utaumbuka kila kitu chako kitakuwa wazi.
Mwanzo 18:20
Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana,
Hivyo ni vema kujitafakari mtu binafsi Mungu ni wa rehema na huwezi kushibda dhambi kama hauna Mubgu ndani yako.Ukimpokea Yesu Kristo anafanya uweza wa kuishinda dhambi kuwepo ndani yako( yaani ile nguvu ya kushibda dhambi inakuwa ndani yako) na kuishinda huku sio kama hautatamani kutenda dhambi ila utakuwa na uzito wa kuitenda uliojawa na hatia ya kuigopa kumkosea Mungu, hiyo ndio itakayokufanya uishinde Dhambi. Kumbuka Dhamira ikifa dhambi inakuwa shemu ya maisha yako.
Warumi 6:17
Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake.
SEMA SALA HII KWA UFUPI:
Bwana Yesu, mimi(.........taja jina lako) ninaomba msamaha kwa uovu nilioufanya, nimkuwa mtumwa wa huo, naomba unisamehe leo, nakupokea uwe Bwana na Mwokozi Binafsi wa Maisha yangu, nipe nguvu ya kuishinda dhambi Kwa Damu ya Yesu. Namkataa shetani na kazi zake zote na nakupokea Bwana kuanzia leo. Naomba ulinzi wako siju zote za maisha yangu.
Amen.