Nguvu nyingi arusha ilikuwa ni diversion ya mjadala wa DOWANS?

Mtaka Haki

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
492
149
Watu wengi wanajiuliza kwa nini CHADEMA wakubaliwe kufanya mkutano na maandamano na kisha zikiwa muda mfupi kabla ya tukio anaingia IGP kukataza maandamano?
Kuna tetesi kuwa walijua wazi kuwa CHADEMA wataendelea na maandamano kwani walishapewa barua. Hivyo nia ilikuwa ni kuepusha mjadala wa DOWANS ili mjadala wa kitaifa uhamie kwenye maandamano kuzuiliwa na nguvu kutumika.

Ninaomba hoja ya DOWANS na Maandamano ziende pamoja. Watanzania wakiendelea kushangaa mambo ya maandamono pekee watajasikia tu kuwa pesa zililipwa tayari.
Vyombo vya habari vinatakiwa vibebe mambo yote mawili. Utata unaokithiri wa DOWANS na maandamano. Walioko katika nafasi mbalimbali wanapaswa walinde kuhakikisha hakuna shilingi yetu inalipwa kwa wezi.

Makubwa yaliyofichwa yataendelea kufunguka. Kuna uwezekano mkubwa ikamlazimu mkulu ajiuzulu kama ataamua kumaliza kwa heshima.
Wengi serikalini wanajua kuwa haraka inayofanywa ya kulipa pesa hizi ni maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao. Yeyote atakayeonekana kuwa kinyume na hili la DOWANS kulipwa inajulikani kuwa ni ole wake.
 
Kuna haja ya kuwa loyal kwa katiba kuliko kwa watu wenye maslahi binafsi katika nchi hii.
 
Back
Top Bottom