Nguvu iliyotumika kudhibiti Waandamanaji Oktoba 29, 2025 ilikuwa kubwa kuliko uhalisia

Ghwema

Member
Joined
Dec 6, 2025
Posts
7
Reaction score
7
Nguvu iliyotumika kudhibiti Waandamanaji Oktoba 29, 2025 ilikuwa kubwa kuliko uhalisia

Katika historia ya Tanzania, suala la matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji imekuwa ni suala geni na lenye gumzo kubwa ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Jamii ya kidemokrasia, maandamano ni moja ya njia halali ambayo wananchi hutumia kuonyesha hisia zao, madai yao na mwenendo mzima wa kutoridhishwa kwao dhidi ya mamlaka au maamuzi Fulani ya serikali.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya ibara ya 20 inatoa haki ya watu kukusanyika na kutoa maoni yao kwa amani.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025, mnamo Oktoba 29, 2025, kulitokea maandamano makubwa ambayo hayakuwahi kutokea na waandamanaji walitumia mitandao ya kijamii kuripoti maandamano hayo, ambayo mwanzoni yalianza kwa Amani na waandamanaji walikuwa wakipinga uchaguzi kwa sababu haukuwa wa haki na huru.

Kuelekea kwenye uchaguzi huo kulikuwa na matukio kadha kwa kadha yakiripotiwa na wanaharakati kama, vile Maria Sarungi, Mange Kimambi na Edson Mwakabela “Sativa”, yalihusu kutekwa kwa watu waliokosoa mwenendo mzima wa serikali.

Wengine ni waliouawa na kutekwa ni pamoja na waliokuwa makada wa CHADEMA, Ali Kibao, Mdude Nyangali pamoja na Deusdedith Soka na wenzake.

Kutokana na matukio yote hayo ya utekaji, malalamiko ya kijamii kuhusu huduma za maji, afya, elimu bora na miundombinu, uminywaji wa haki za binadam na uchumi kulipelekea hasira vifuani mwa wananchi na kusababisha kutokea kwa maandamano wakati wa siku ya uchaguzi (Oktoba 29, 2025).

NGUVU ILIYOTUMIKA ILIKUWA KUBWA
Nguvu iliyotumika dhidi ya Waandamanaji kuanzia Oktoba 29, 2025 haikustahili kwa namna yoyote ile. Mamlaka zinajaribu kuhalalisha matumizi ya nguvu kuwa ilikuwa njia ya kuzuia mapinduzi.

Hoja hiyo inakosa mashiko pale tunapotazama aina ya silaha zilizotumika dhidi ya raia.

Nguvu inayostahili ina lengo la kudhibiti na kutawanya na sio kuangamiza na kupora uhai wa raia. Huwezi kuhalalisha matumizi ya risasi za moto dhidi ya waandamanaji ambao hawakuwa na silaha yoyote mikononi mwao.

Sheria za kimataifa na utu wa kibinadamu unakataza kutumia nguvu ya kuua (lethal force) dhidi ya watu wasio na uwezo wa kujihami.

Kwa mantiki hiyo nguvu hiyo inastahili kivipi ikiwa matokeo yake ni mamia ya miili ya watanzania kujazwa kwenye vyumba vya maiti na makaburi ya siri? Ikiwa muandamanaji hana bunduki wala bomu, kumpiga risasi ya kichwa, kifuani au tumboni siyo ulinzi wa Amani bali ni matumizi mabaya ya mamlaka na ukiukwaji mkubwa wa haki ya kuishi.

Amani haiwezi kupatikana kwa kumwaga damu ya raia ambao kosa lao pekee ni kuelezea hasira zao dhidi ya mifumo ya uchaguzi.

HIZI NI SABABU KWANINI NGUVU ILIYOTUMIKA ILIKUWA KUBWA
Uchunguzi ulifanyika ikabainika, Wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, majira ya saa 10; 45 kulianza kuripotiwa matukio ya waandamanaji wakipinga uchaguzi, ripoti hizo walizitoa waandamanaji wenyewe kupitia mitandao yao ya kijamii.

Video hizo zilionyesha jinsi maandamano yalivyokuwa yakipamba moto huku baadhi ya mikoa kama Mwanza, Dar es Salaam na Arusha video zilionyesha kuchomwa kwa ofisi za CCM, Mali ambazo zilisadikika ni za watu wa CCM kama magari na ofisi zao za biashara, hali hii ilionyesha maandamano yalikuwa na fujo na vurugu ndani yake.

Sababu ya maumivu na hasira zilizomo mioyoni mwao kutokana na serikali kutofanyia kazi masuala ya watu kutekwa na kuminywa kwa Haki za Binadamu.

Siku ya Uchaguzi Mkuu, vituoni wapiga kura walikuwa wachache na vituo vingine kulikuwa hakuna wapiga kura kabisa, hii ni kwasababu wengi waliweka mgomo na baadhi kuhofia kutoka nje kwenda kupiga kura.

Fujo ziliongeza, waandamanaji waliingia vituoni kufanya uharibifu ikiwemo kutupa maboksi ya kura na kuwavamia wasimamizi wa vituo ili zoezi lisiendelee, ndipo wakati huo Vyombo vya Usalama vikaanza kudhibiti waandamanaji.

Risasi zilisikika, mabomu ya machozi na virungu, tamko la kukatwa kwa internet likatoka na wananchi walikosa internet ndani ya siku sita kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 3, 2025.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ikamtangaza Samia Suluhu Hassan kuwa mshindi, akaapishwa ambapo alisema amesikitishwa na uvunjifu wa amani.

View: https://youtu.be/1gXHeLA0qxg?si=KU1J4fGx7XhTf6Fd

Baadaye iligundulika kuwa kulikuwa na idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha, mashahidi wakaeleza kupitia mitandao kuwa walishuhudia watu wengi wakipoteza maisha iwe ni chini ya usalama au wakiwa mtaani.

Video zilisambaa na kuonesha jinsi watu walivyopoteza maisha, mjadala unakuja. JE, NGUVU ILIYOTUMIKA DHIDI YA WAANDAMANAJI WENYE HASIRA KALI ILISTAHILI?

HOTUBA YA RAIS SAMIA SULUHU
Hotuba ya rais wa awamu ya sita mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ni hotuba ya kihistoria na yenye hisia kali aliyoitoa Desemba 2, 2025, alipokutana na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa JNICC.

View: https://www.instagram.com/reel/DRwdfFZjelu/?igsh=YnVsMmVlbGMzNzln

RIPOTI ZA MASHIRIKA YA HAKI ZA BINADAM NA VYOMBO VYA HABARI
Mashirika ya nje na ya ndani yaliripoti kuhusu matukio hayo kama ifuatavyo;

OMCT (WORLD ORGANIZATION AGAINST TORTURE); ilieleza kulikuwa na mauaji ya waandamanaji kwa kutumia risasi nzito za moto na kukamatwa kwa mamia ya watu katika mikoa tofauti tofauti kama vile Mwanza, Dar es Salaam na Arusha na kupewa kesi za uongo za uhaini.

AMNESTY INTERNATIONAL; Ilitoa ripoti ikisema kuwa vyombo vya usalama nchini Tanzania vilitumia nguvu mbaya na isiyo ya lazima, ripoti yao ilidai kuwa na ushahidi wa video uliionyesha zaidi ya miili 70 ikiwa imerundikwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala (Dar) na video nyingine zikionyesha miili HospitalI ya Sekou Toure (Mwanza).

Pia, waliripoti kuwa baadhi ya watu waliuawa wakiwa ndani ya nyumba zao na wengine wakiwa wapiti njia.

HUMAN RIGHT WATCH (HRW); Waliripoti kuwa Polisi na watu waliovalia nguo za kiraia walifyatua risasi za moto dhidi ya waandamanaji na raia, HRW ilinukuu vyanzo vya habari vya upinzani (CHADEMA) vikidai kuwa idadi ya vifo nchi nzima inaweza kufika 700 hadi 1000, ingawa walikiri kuwa ni vigumu kuthibitisha idadi kamili kwasababu serikali ilizuia upatikanaji wa taarifa.

UMOJA WA MATAIFA (UN – OHCHR); Kamishna Mkuu wa Haki za Binadam wa UN, Volker Turk alieleza wasiwasi wake kuhusu taarifa za miili ya watu waliouawa kuondolewa mtaani na kupelekwa kusikojulikana ili kuficha ushahidi. Mwanzoni walikadiria kuwa ni vifo vya watu wachache lakini baadaye walitambua idadi halisi inaweza kuwa mamia ya watu.

Ripoti za Vyombo Vya Habari vya Kimataifa
CNN (Uchunguzi wa Larry Madowo): Ripoti yao ilionyesha kuwa Askari Polis walifyatulia risasi za moto waandamanaji ambao wengi wao walikuea hawana silaha, iliripoti kuwa kuna dalili za kuwepo kwa makaburi ya pamoja ambapo miili ya wahanga ilizikwa kisiri ili kuzuia idadi kubwa ya vifo isijulikane duniani.

View: https://www.instagram.com/reel/DRTwtwWAiX1/?igsh=MXFveGNjbzBjeHkxag==

Ripoti nyingine ni kutoka:

View: https://www.instagram.com/reel/DRBPL8bDdf9/?igsh=MWZjenRscmNuOHVqcg==
BBC Swahili

RIPOTI YA NDANI (LHRC - Tanzania): Pamoja na asasi zingine za ndani walilaani mauaji ya kulipiza kisasi dhidi ya vijana wasio na hatia. Waliripoti vifo vya Waandishi wa Habari kama Master Tindwa wa Clouds Media na Kelvin Lameck wa Baraka FM ambao waliuawa katika maeneo ya makazi yao.

TUNASISITIZA WATANZANIA WANASTAHILI USALAMA NA KUHESHIMU HAKI ZA BINADAM. SAUTI ZETU ZISIKIKE
 
1000438616.png

Jamaa zako wanajilinganisha na nchi nyingine... Meaning ni kwamba bado wanafikiri kuua wengine zaidi!
 
Ukishastuka baada ya 29 okt wahamasishaji maandamano wakawa wanahamasisha maandamano ya amani na kusisitiza mabango, itakua ndo unaanza kuelewa kwamba hata kama unadai haki usipokua na mipango sahihi ni kufeli tu
 
Hakuna sheria inayosema maandamano lazima yawe na mabango, kulazimisha mabango ilisemwa kama mtego na washika mabango ndiyo wangekuwa target kwanza wengine wangefuata baada ya wao.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
RIPOTI YA NDANI (LHRC - Tanzania): Pamoja na asasi zingine za ndani walilaani mauaji ya kulipiza kisasi dhidi ya vijana wasio na hatia. Waliripoti vifo vya Waandishi wa Habari kama Master Tindwa wa Clouds Media na Kelvin Lameck wa Baraka FM ambao waliuawa katika maeneo ya makazi yao.
 
Hakuna sheria inayosema maandamano lazima yawe na mabango, kulazimisha mabango ilisemwa kama mtego na washika mabango ndiyo wangekuwa target kwanza wengine wangefuata baada ya wao.
Mambo yalishaingiliana mkuu, siasa nchi hii ngumu sana
 
Back
Top Bottom