Divine... ameshaongea yote. Ila kuna kipande ngoja tu na me niongezee, who knows....
Kichwa kinabeba baraka, mamlaka, maono, ndoto, maamuzi, mawazo etc
Kichwa ndio kiungo kinachobeba dira ya mwili mzima, kichwa kikiharibika basi mfumo mzima wa mwili unaharibika pia. Kichwa kinaamuru viungo vingine vifanye sawasawa na taarifa iliyopo kichwani. Kichwa ndo muamuzi wa mwisho, kikiamuru miguu tembea itatembea, mikono nyanyuka itanyanyuka n.k. maamuzi yanayofanywa na kichwa ndo yanamtofautisha mtu mwenye akili timamu na asiye na akili timamu. Mtu asiye na akili timamu anapoteza ule uwezo wa kuamuru viungo vingine kufanya kazi na kujiongoza yeye mwenyewe. No wonder kichaa (sijui ni sahihi kumuita hivi) hatambui kama anachokifanya si sahihi, ataondoka na nyumbani pia coz kichwani kwake hakumbuki hata kama ana nyumbani kwake. Me niongelee mume kuwa kichwa cha familia
MUME NI KICHWA
Efeso 5:23
Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa, naye ni mwokozi wa mwili
Kwa sababu Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu, basi hata kwenye familia aliweka utaratibu. Hivyo mume ndiye kichwa cha mkewe, kichwa cha familia. Mke ana kazi kuu ya usaidizi na ndo maana Mke tunamuita shingo. Na Mungu amefananisha uhusiano wa mke na mume, kama uhusiano wa Kristo na kanisa. Mume ana wajibu gani
1. MAMLAKA
Mume amtawale na kumuongoza mke na familia yake pasipo ubinafsi wala unyonyaji.
Mathayo 20:25- 28
Lakini Yesu akawaita, akasema, mwajua ya Kuwa wakuu wa mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha
26: Lakini haitokuwa hivyo kwenu, bali mtu yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu.
Kwa sababu wewe ni kichwa, sio ndo busy kumuamrisha mkeo tu kila kitu. Kuna muda inabidi wewe mwenyewe utumike pia. (Mkeo ni msaidizi wako)
2. UPENDO
Mume anatakiwa ampende mkewe kama anavyojipenda yeye mwenyewe. Kuna mtu anayejipenda akajiwazia mabaya, akajiumiza au kujinenea mabaya??? Mke ni mwili wako, je Kuna anayeweza kuuchukia, kuuumiza au kuutesa mwili wake mwenyewe?
Efeso 5:25- 29
25:Enyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akalitoa kwa ajili yake
28: vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe, ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe
29: Maana hakuna anayeuchukia mwili wake popote, bali huulisha na kuutunza. .....
Mume ameagizwa kumpenda mkewe kama Kristo alivyolipenda kanisa lake
3. HESHIMA, HEKIMA NA UFAHAMU
1 Petro 3:7
Kadhalika ninyi waume kaeni na wake zenu kwa akili na kumpa mke heshima kama chombo kisicho na nguvu. .....
Mume awe na hekima na ufahamu wa kuiongoza familia yake. Obviously kutakuwa na ups and downs za kutosha but mume lazima asimame kwenye nafasi yake, akairudishe ndoa yake kwenye mstari. Ajiheshimu na kumuheahimu mke wakw pamoja na maoni yake. Kushindwa kufanya hivyo ni kuzuia maombi yake yeye mwenyewe.
4. KUITUNZA FAMILIA
Uanaume ni majukumu. Kama Huna kazi au biashara utaitunzaje familia yako
Mwanzo 3:19
Kwa jasho la uso wako utakula chakula
Mwanaume inabidi atoke jasho, kutafuta kipato. Mungu hataki mume legelege, uihudumie na kuitunza familia yako kwa jasho. Mwanaume usiwe mario eti
1 Timotheo 5:8
Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yani wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko asiyeamini
5. ASIYE MWEPESI WA HASIRA
Uanaume haupimwi kwa jinsi unavyozikimbia changamoto, ila kwa jinsi unavyokabiliana nazo pasi kuwa na hasira. Siyo umegombezwa na boss wako huko kazini, basi ukirudi hasira zote kwa mkeo. Ukipatwa na tatizo, kimbilia kwa Mungu then relax kupata ufumbuzi. Usifanye maamuzi ya hasira
Mithali 16:32
Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa. ...
6. MNYENYEKEVU
Tumeshazoea siku zote mke ndiye anayetakiwa kuwa mnyenyekevu kwa mumewe, Lakini mume pia inampasa awe mnyenyekevu. Asiwe mtu wa kujiona bora zaidi ya mkewe au kushindana naye kwa kila kitu. Awe anamshirikisha mkewe vyema
Wafilipi 2:3
Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu. Kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa ni bora kuliko nafsi yake