Ngurumo: Ni kaburi la CCM au CHADEMA?

Ngurumo: Ni kaburi la CCM au CHADEMA?

watu wanaotamani chadema ife ni lazima watiliwe shaka kama wana akili timamu maana chadema ina wafuasi na wanaokiunga mkono kwa mamilioni. ni lazima wajue kuwa kufa kwa cdm kwa sasa ni kuyumba kwa nchi. na matarajio ya watu. hata kufa kwa ccm pia ni tatizo ni lazima vyama hivi vibaki kimoja kikiwa mpinzani. naweza kusema tu kuwa ccm ichukue kwanza nafasi ya upinzani ikajipange upya lakini sio ife. baadae vinaweza kufa taratibu maana kutakuwa na vingine vitakavyokuwa na nguvu.
 
Mmmhhhh! Waandishi wetu wengi wa mambo ya siasa hawana principles zozote.

Kama taifa ni janga kubwa sana kuwa na wanasiasa Kanjanja na waandishi wa habari Kanjanja.
 
A political party just like a football team must play as a team in order to win. You may have a collection of best players on earth but if they do not play as a team with a common strategy they will never win!
 
Waandishi wa namna hii ni disaster kweli kweli, Hivi hajui Chama na mwanachama ni zaidi ya kuku na Yai, Chama kinachoshindwa kumtendea haki mwanachama, wala hakiwezi kufika mbali.
Chama kinachowapikia jungu wananchama wake eti kisa wasigombee uenyekiti, ni chama kinachojichinja chenyewe.
Mwandishi ameonyesha ushabiki wa hali ya juu huku akijitwika joho la falsafa, "eti kitakufa kwa sababu kila chenye mwanzo kina mwisho". SO WHAT IF MWANZO NI 1992 NA MWANZO WA MWISHO NI 2013?.
Bahati mbaya sana mwandishi hajaeleza ni kwa namna gani chama hushamiri, na ni kwa namna gani chama hufa. LABDA NIMKUMBUSHE TU KWAMBA, HAKI KWA KILA MWANANCHAMA NDIYO MSINGI WA UHAI WA CHAMA. NA WAJIBU WA KILA MWANACHAMA NDIYO HUKIFANYA CHAMA KISHAMIRI ZAIDI.
kwa kuwatungia tuhuma za kizushi, Viongozi wa juu, halafu ukawahukumu viongozi hao, HALAFU UKAANZA KUTAMBA KAMA ZUZU ETI CHAMA KIMEFANYA MAAMUZI MAGUMU NI UJUHA WA HALI YA JUU.

Mwandishi huyu ni philosophical, a scholar of semantics and stylistics at advanced secondary level na kama mtu hujapitia field hiyo don't bother argue with him maana utaishia kutukana. Kutokumwelewa haina maana kuwa wewe ni mjinga. La hasha. It's a matter of background. Halafu mwandishi huyu ni mhaya. Hawa watu wa interlacustrine areas wana falsafa toka zama na zama. Kuna msemo kwa kule "kusiga omwa nyo kulaire okagya kuemba ogwo omwa mukasho" yaani literally ni kuwa unaacha kwa mama yako moto wa kupikia hamna unakwenda kusaidia kuwasha meko kwa mama wa kambo. Hii kwa kiigereza tunaita chameleon tears. Ndio CCM wanaowaonea huruma waliovuliwa vyeo CDM wakati kwao wana matatizo yanahtaiji uwajibikaji lakini hawafanyi chochote. Kuingilia yasiyowahusu hakuwezi kuiua CDM maana CDM ina ideology, policies na ina exist as per the law
 
Ngurumo ni maji marefu kaka huwezi mfikia na kumwelewa will take you time na ndiyo maana Kibanda alimkimbia pale .Ngurumo hebu ulizia tena habari zake kabla hujaja na comments nyepesi .Kichwa kingine kile .
 
Mwandishi huyu ni philosophical, a scholar of semantics and stylistics at advanced secondary level na kama mtu hujapitia field hiyo don't bother argue with him maana utaishia kutukana. Kutokumwelewa haina maana kuwa wewe ni mjinga. La hasha. It's a matter of background. Halafu mwandishi huyu ni mhaya. Hawa watu wa interlacustrine areas wana falsafa toka zama na zama. Kuna msemo kwa kule "kusiga omwa nyo kulaire okagya kuemba ogwo omwa mukasho" yaani literally ni kuwa unaacha kwa mama yako moto wa kupikia hamna unakwenda kusaidia kuwasha meko kwa mama wa kambo. Hii kwa kiigereza tunaita chameleon tears. Ndio CCM wanaowaonea huruma waliovuliwa vyeo CDM wakati kwao wana matatizo yanahtaiji uwajibikaji lakini hawafanyi chochote. Kuingilia yasiyowahusu hakuwezi kuiua CDM maana CDM ina ideology, policies na ina exist as per the law

Ngurumo ni product za Seminary katoliki Tanzania zenye uwezo mkubwa sana .
 
NATAKA kusema neno moja. Ni hivi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitakufa. Lakini hakifi leo, wala hakitakufa kwa sababu ya kumvua vyeo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na wenzake.

Kitakufa siku moja kama vyama vingine vyote vitakavyokufa, kwa sababu kila kilichoanza kina mwisho wake.

Kitakufa wakati wake utakapowadia. Si sasa. Si leo. Na hakitakufa kabla Watanzania hawajashuhudia kifo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM). Niamini.

Zaidi ya hayo, hakitakufa kwa sababu ya makundi ya wana CCM wanaojipanga nchi nzima kuzomea, kuchochea mgororo, kutisha viongozi wa CHADEMA na kubeza uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho.

Badala yake, kwa kufanya uamuzi mgumu, kwa kugusa baadhi ya wanachama na viongozi wanaodhaniwa kuwa hawagusiki; kwa kufanya kile ambacho CCM wamekuwa wanashindwa kufanya, CHADEMA kimejiweka katika mazingira mapya ya kukua na kukomaa.

Kinaonyesha kuwa sasa kimekuwa taasisi. Walio tayari kufanya kazi kitaasisi wataendelea kufanya kazi. Waliojiunga na chama kufuata watu, wataondoka na watu hao. Waliofuata sera watabaki. Chama kitapona.

CCM ilipokuwa bado imara iliwahi kufanya uamuzi mgumu. Katika kutetea kile ambacho uongozi wa chama uliona ni msimamo wao kuhusu Muungano, chama kilimfukuza Makamu wa Rais, Aboud Jumbe na Waziri Kiongozi, Seif Shariff Hamad.
Uzito na ukweli wa hoja zao ni jambo moja; na msimamo wa chama ni jambo jingine. Chama kilitetea msimamo wake. Viongozi wakubwa wa ngazi hizo wakaanguka, chama kikapona.

CCM legelege ya sasa haiwezi kufukuza hata wale inaowatuhumu kwa makosa makubwa na kuwashambulia hadharani. Inawaogopa.

Ndiyo maana kelele za kuvua magamba zilipopamba moto, Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, alikejeli harakati za wenzake akisema, “gamba limekwama kiunoni. Mwenye uwezo wa kulivua aje na shoka.”

Mwaka umepita sasa, gamba la Chenge limewashinda Rais Jakaya Kikwete, Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, na mashabiki wao.

Kwa hiyo haishangazi kwamba CHADEMA inapochukua hatua ndogo tu ya kubadilisha watu vyeo kwa sababu ya kukosa imani nao, wanaokerwa zaidi na hatua hiyo ni wana CCM.

Ndio wanaohaha nchi nzima wakitangaza kila kona “CHADEMA kinakufa, CHADEMA kinakufa.” Kisa, eti Kamati Kuu imemvua Zitto vyeo. Kwani yeye alivipataje? Si wale wale waliompatia vyeo ndio wameamua kumwondolea vyeo hivyo?
Na tangu lini CCM wakawa na huruma kwa CHADEMA? Iweje leo ‘CHADEMA inakufa’ halafu wanaoumia ni wana CCM?

Kwanini CCM wanasikitishwa na ‘kifo’ cha CHADEMA? Kuna jambo. Wenye akili wameshaligundua.

Iweje wanaoandaa magenge ya kuzomea viongozi wa CHADEMA na kubeza uamuzi wa Kamati Kuu ni baadhi ya wanachama wa zamani wa CHADEMA waliokimbilia CCM?

Wanatuma ujumbe gani kwa Watanzania? Zaidi ya hayo, mbona hawa wamenyang’anywa vyeo tu, tayari propaganda za udini na ukabila ndo zinaibuka tena?

Ni dini gani inayoagiza kwamba cheo ni haki ya kuzaliwa ambayo mtu akishapewa hapaswi kunyang’anywa, hata ikithibitika kwamba wenzake hawana imani naye?

CCM na makapi yao sasa wanahaha nchi nzima kuhubiri udini na ukabila. Huu nimeuita ujinga. Ni ugonjwa wa akili. Ni kichaa kama vingine.

Hivi CHADEMA ilipovunja uongozi wa chama Mkoa wa Mwanza ilikuwa inatetea dini na makabila?

Ilipofukuza madiwani wanne Arusha ilikuwa inapambana na Uislamu? Ilipomvua cheo Samson Mwigamba na Dk. Kitila Mkumbo ilikuwa inajadili dini na makabila yao?

Ni lini tumeanza kuficha udhaifu wetu katika makabila yetu na imani zetu za kidini? Kwa faida ya nani?

Ndiyo! Ipo siku CHADEMA itakufa. Lakini kwa mbinu hizi za CCM ya sasa, CHADEMA itazidi kushamiri. Jipeni muda, mtaelewa maneno yangu.

Wanaotaka kutumia mwanya huu kudhoofisha chama hiki wanapoteza muda. Hawataweza. Chama kimeshawazidi nguvu. Kimewazidi kimo.

Nakumbuka miaka kama 15 iliyopita, wana CCM walikuwa wanamwaga sifa kwa CHADEMA, wakisema ni chama cha watu wastaarabu, hakina fujo wala migogoro. Walikiona ni chama cha wastaafu na mabepari wenye pesa ambao hawana papara.

Leo wanakiona ni chama chenye fujo. Wamefikia hatua ya kukizushia tuhuma za ugaidi. Sababu ni moja. Wakati ule, CHADEMA hakikuwa tishio kwa chama tawala.

Kilipewa sifa hizo kwa kuwa kilikuwa kinaonekana ni mateka wa mfumo unaotawala.
Kilikuwa chama kwa sababu tu kina usajili.

Lakini hakikuwa kinaonyesha dalili zozote za kutaka au kukaribia kushika dola. Ustaarabu wa CHADEMA wa enzi zile ilikuwa silaha ya nyongeza ya CCM.

Leo CHADEMA ndicho chama pekee kinachokua kwa kasi hapa nchini. Ndicho kinachotetemesha wakubwa katika mijadala bungeni.

Ndicho kinachoongoza mapambano ya wanyonge dhidi ya watawala. Ndilo tishio kuu la serikali ya sasa.

Kwa hali ya sasa ya kisiasa, katika kutapatapa kukubalika na kubaki madarakani, CCM inajua kuwa haitapata kuungwa mkono na watu kwa mikutano ya hadhara au sarakasi zozote za kisiasa.

Inajua kuwa wananchi wamechoka, wanataka mabadiliko. Njia ya mabadiliko inayotazamwa sasa ni CHADEMA.
Watawala wamebaki na mambo mawili ya kufanya. Ya kwanza ni kupenyeza ‘virusi’ ndani ya CHADEMA. Ya pili ni kupenyeza rupia ndani ya CHADEMA katika ngazi mbalimbali.

Kinachowakera watawala ni kwamba tayari CHADEMA imeshaanza kugundua baadhi ya hatua zinazochukuliwa na CCM.

Kinachokera zaidi ni kwamba CHADEMA inaweza kuthubutu kuchukua hatua, na kupambana na matokeo. Hili nalo ni chukizo kwa CCM.

Kimsingi, CCM inatamani kuua CHADEMA, lakini haijajipanga vema. Haijui jinsi ya kuiua. Ijipange upya.
Watanzania wanajua kipi kinaelekea kaburini kati ya CCM na CHADEMA. Waachwe waamue.

CHADEMA haitakufa kisa tu imemvua nyadhifa zake Zitto au itamfukuza Zitto, kitachoiua CHADEMA ni kitendo cha viongozi wake wachache kuikanyaga demokrasia na kujifanya miungu wasiokuwa na makosa.

Nimesoma vizuri WARAKA wa CHACHA WANGWE, nimeusoma Vizuri MKAKATI WA MABADILIKO na nimelisoma TAMKO LA KAMATI KUU JUU YA MAAZIMIO YAKE ya kuwavua nyadhifa zao Zitto na wenziwe. Nimegundua tatizi ni uenyekiti na kila mwenye kukosoa uongozi wa Mbowe huitwa MSALITI na mbaya zaidi huambiwa katumwa na CCM. Tabia hii ndio itaiua CHADEMA kabla ya siku zake,,na katu kuvuliwa nyadhifa zake Zitto na hata akifukuzwa CHADEMA haitakufa.

Mara baada ya KAMATI KUU kumvua nyadhifa zake Zitto, sekretarieti ikatangaza ratiba na tarehe ya uchaguzi wa ndani. Tunajua kamati kuu iliagiza hadi mwezi huu uchaguzi wa ndani uwe umeshakamilika,,,sasa siku zote hiyo sekretarieti ilikuwa wapi? au ilikuwa inasubiria Zitto apate majeraha na kuvunjika mbawa? Kama ndivyo, je kile kikao cha kamati kuu na maamuzi ya kikao hicho si sehemu ya utekelezaji wa MKAKATI wa Mbowe kuhakikisha anabaki madarakani kwa kipindi cha tatu? Je, tukisema hata ile RIPOTI YA SIRI ni sehemu pia ya utekelezaji wa mkakati wa Mbowe kubaki madarakani? Sababu chama kilikaa kimya juu ya RIPOTI ile hadi pale raia yule wa ujerumani alipolalamika,,,lkn kuna propaganda nyingi chama imezijibu kwa haraka.

Hawa vijana wanaokesha kwenye mitandao kumchafua Zitto pia ni sehemu tu ya huo mkakati,,,sasa tunajiuliza,,,iweje MKAKATI WA KITILA uwe uhaini ila huu mwingine uwe ni mzuri? Pia tunajiuliza, Lema alitumia mitandao kumchafua na kumdhalilisha Zitto,,lakn kamati kuu haijatoa hata onyo kwa lema na hivi karibuni tumeshuhudia Msigwa akitumia mitandao kumshambulia Zitto na kwa mashambulizi yake kwa wajuzi wa mambo wameshajua kuwa yalikuwa na lengo la kuumpa Mbwa jina baya ili apate kuuliwa vizuri, kwa kifupi tushajua nini kitajiri kamati kuu kabla hata ya hiyo kamati kuketi.

Ngurumo mambo kama haya ndio yatakayo imaliza CHADEMA,,,lakini kufukuzwa kwa Zitto hakutaimaliza CHADEMA. Kikubwa viongozi wabadilike na waache mienendo yao michafu, wakifanya hivyo, hata kama wakimfukuza Zitto kutokana na chuki zao binafsi lakini chama kitabaki salama kinyume chake kitakufa kabla ya siku yake.

Mwisho makala yako imeangalia wakina nani wanaopinga maamuzi ya kamati kuu lakini hukuangalia hoja za watu hao wanaopinga maamuzi hayo. Hili pia ni tatizo ambalo linaweza kuimaliza chadema, wanaCHADEMA wengi hatuangalii hoja bali tunamuangalia mjenga hoja, na kwa tabia hii ndio maana tunapinga hoja hata kama hoja hiyo ni msingi na yenye kujenga chama.

Makala yako haijazingatia kuwa wandaaji wa ule WARAKA WA MKAKATI WA MABADILIKO ambao ni Kitila na Mwigamba walikiri kuandaa bila Zitto kujua au kumuhusisha.

Makala yako haijazingatia maudhui ya WARAKA wenyewe ambayo pamoja na mambo mengine maudhui hayo yanaonesha kuwa MHUSIKA MKUU ambaye Zitto kabwe hajui kinachoendelea.

Makala yako haijazingatia kuwa Zitto amekana kuhusika na kuufahamu huo WARAKA na ya kwamba ameuona kwa mara ya kwanza siku ya kikao cha kamati kuu.

Laiti makala yako ingezingatia nukta hizo na laiti makala yako ingeangalia
hoja za wanaopinga maamuzi ya kamati badala ya kuwaangalia watoa hoja hakika Usingeishia kusema kuwa CHADEMA itakufa bali ungeenda mbali zaidi kwa kuwataka viongozi wetu warudi kwenye mstari na kuacha siasa chafu za ndani ya chama.

MUNGU IBARIKI CHADEMA NA VIONGOZI WAKE.

Njano5.
0655345394
 
Ngurumo ni mwandishi professional na yeye zaidi huandika makala za siasa na si vuguvugu kama wengine bali amechagua upande wa kusimama na hiyo inaruhusiwa.Elimu yake inaeleweka na ameamua kuwa adui wa CCM bila kupepesa macho.
Waandishi wa habari wengi siwaamini, hata kidogo hususani hawa ambao wameajiriwa! Napata taabu kuamini kwamba leo hii Ngurumo apate bonge la offer(say three fold) somewhere else, like serikalini basi anaweza kui-turn down hiyo offer! Napata taabu kuamini kwamba akipata offer kama hiyo ataendelea na hiyo dhana hapo kwenye RED!!
 
!
!
ukome tena ukome na iwe mwanzo na mwisho kuandika 'yesu'....nyambafu wewe,andika Yesu au YESU, kama huwezi acha. una akili sana wewe,Mwalimu mkuu mama yako nini?

Ndyo kwaida yao hao uvccm wanataka madaraka kwa kutumia mgongo wa udini.. Nadhani ccm kuna janga wanataka kutuletea vita kubwa ya kidini na kikabila..watanzania tuwe makini na hyu mdudu shetani ccm ni majanga..
 
Waandishi wa namna hii ni disaster kweli kweli, Hivi hajui Chama na mwanachama ni zaidi ya kuku na Yai, Chama kinachoshindwa kumtendea haki mwanachama, wala hakiwezi kufika mbali.
Chama kinachowapikia jungu wananchama wake eti kisa wasigombee uenyekiti, ni chama kinachojichinja chenyewe.
Mwandishi ameonyesha ushabiki wa hali ya juu huku akijitwika joho la falsafa, "eti kitakufa kwa sababu kila chenye mwanzo kina mwisho". SO WHAT IF MWANZO NI 1992 NA MWANZO WA MWISHO NI 2013?.
Bahati mbaya sana mwandishi hajaeleza ni kwa namna gani chama hushamiri, na ni kwa namna gani chama hufa. LABDA NIMKUMBUSHE TU KWAMBA, HAKI KWA KILA MWANANCHAMA NDIYO MSINGI WA UHAI WA CHAMA. NA WAJIBU WA KILA MWANACHAMA NDIYO HUKIFANYA CHAMA KISHAMIRI ZAIDI.
kwa kuwatungia tuhuma za kizushi, Viongozi wa juu, halafu ukawahukumu viongozi hao, HALAFU UKAANZA KUTAMBA KAMA ZUZU ETI CHAMA KIMEFANYA MAAMUZI MAGUMU NI UJUHA WA HALI YA JUU.

AH AH, ENDELEENI KUMTETEA UYO ZITTO KWAN KALA ELA YENU NYING MLOMUONGA ILI AIDHURU CHADEMA NA MPANGO KK YA CDM IMEUKWAMISHA.

MASKINI CCM MNATIA HURUMA SIJUI INAYOWAUMA ATA KUMTETEA ZITO NI ILE ELA AU MPANGO WENU KUKWAMA, Dah BONGE LA BAO MACCM MMEPIGWA

NA MSIVO NA AIBU MNATOA MATAMKO KM WANACHADEMA NEXT DAY WANACHADEMA HALISI WANAYAKANUSHA,

DUH AIBU YENU, NA SASA MNASPEND ELA NYING KUANDAA WATU MAMRUKI ATI KUMPINGA MIKUTANO YA DOCTOR SLAA, MNAOWATUMA WANATOBOA SIRI, ITS SHAME TO U CCM
 
Waandishi wa habari wengi siwaamini, hata kidogo hususani hawa ambao wameajiriwa! Napata taabu kuamini kwamba leo hii Ngurumo apate bonge la offer(say three fold) somewhere else, like serikalini basi anaweza kui-turn down hiyo offer! Napata taabu kuamini kwamba akipata offer kama hiyo ataendelea na hiyo dhana hapo kwenye RED!!

Hahahaha! simtetei na nimewahi kumuona kwa karibu bukoba mjini hivyo usione labda namjua sana lakini nimewahi kusikia kutaka kupewa offer hizo enzi za mtandao akachomoa!!

Si unaona Salva anakula mema ya nchi?

Nadhani muda utaongea mkuu!!
 
Mmmhhhh! Waandishi wetu wengi wa mambo ya siasa hawana principles zozote.

Kama taifa ni janga kubwa sana kuwa na wanasiasa Kanjanja na waandishi wa habari Kanjanja.

Mkuu heshima mbele!

Najua huwezi kufurahishwa na Ngurumo hata kidogo.

Ngurumo awe kanjanja? uwe kanjanja alafu uwe na msimamo kama Ngurumo unajitaka?
 
Niwe wazi,

Ukimtoa Jenerali Ulimwengu hapa Bongo hakuna mwandishi ninayemheshimu kama Ngurumo.
Napenda abaki kuwa mchambuzi wa siasa asiingie kwenye siasa maana kwa umri wake tunahitaji watu kama yeye kunyoosha hii tasnia.
Ana msimamo usioyumba.
 
Hahahaha! simtetei na nimewahi kumuona kwa karibu bukoba mjini hivyo usione labda namjua sana lakini nimewahi kusikia kutaka kupewa offer hizo enzi za mtandao akachomoa!!

Si unaona Salva anakula mema ya nchi?

Nadhani muda utaongea mkuu!!
Kama anaweza kukisimami anachokiamini, then i've no problem! I've no problem kwa mwandishi kuisifia CHADEMA or CCM mwanzo mpaka mwisho ikiwa anafanya hivyo bila kusukumwa na external factors bali ndivyo anavyoamini kwamba CHADEMA or CCM ni chama cha hovyo! Tatizo langu linakuja pale cku yule yule aliyekuwa anaiponda CCM, sasa anaipaka uturi wakati hakuna kilichobadilika zaidi tu ya kubadilika maslahi yake binafsi!!
 
Waandishi wa namna hii ni disaster kweli kweli, Hivi hajui Chama na mwanachama ni zaidi ya kuku na Yai, Chama kinachoshindwa kumtendea haki mwanachama, wala hakiwezi kufika mbali.
Chama kinachowapikia jungu wananchama wake eti kisa wasigombee uenyekiti, ni chama kinachojichinja chenyewe.
Mwandishi ameonyesha ushabiki wa hali ya juu huku akijitwika joho la falsafa, "eti kitakufa kwa sababu kila chenye mwanzo kina mwisho". SO WHAT IF MWANZO NI 1992 NA MWANZO WA MWISHO NI 2013?.
Bahati mbaya sana mwandishi hajaeleza ni kwa namna gani chama hushamiri, na ni kwa namna gani chama hufa. LABDA NIMKUMBUSHE TU KWAMBA, HAKI KWA KILA MWANANCHAMA NDIYO MSINGI WA UHAI WA CHAMA. NA WAJIBU WA KILA MWANACHAMA NDIYO HUKIFANYA CHAMA KISHAMIRI ZAIDI.
kwa kuwatungia tuhuma za kizushi, Viongozi wa juu, halafu ukawahukumu viongozi hao, HALAFU UKAANZA KUTAMBA KAMA ZUZU ETI CHAMA KIMEFANYA MAAMUZI MAGUMU NI UJUHA WA HALI YA JUU.

We kweli gamba la nyoka, ni sawa sawa na nyani haoni makario yake.mtu mwenye busara huwezi kutoa poit less kwa nondo hiyo hapo juu
 
Waandishi wa namna hii ni disaster kweli kweli, Hivi hajui Chama na mwanachama ni zaidi ya kuku na Yai, Chama kinachoshindwa kumtendea haki mwanachama, wala hakiwezi kufika mbali.
Chama kinachowapikia jungu wananchama wake eti kisa wasigombee uenyekiti, ni chama kinachojichinja chenyewe.
Mwandishi ameonyesha ushabiki wa hali ya juu huku akijitwika joho la falsafa, "eti kitakufa kwa sababu kila chenye mwanzo kina mwisho". SO WHAT IF MWANZO NI 1992 NA MWANZO WA MWISHO NI 2013?.
Bahati mbaya sana mwandishi hajaeleza ni kwa namna gani chama hushamiri, na ni kwa namna gani chama hufa. LABDA NIMKUMBUSHE TU KWAMBA, HAKI KWA KILA MWANANCHAMA NDIYO MSINGI WA UHAI WA CHAMA. NA WAJIBU WA KILA MWANACHAMA NDIYO HUKIFANYA CHAMA KISHAMIRI ZAIDI.
kwa kuwatungia tuhuma za kizushi, Viongozi wa juu, halafu ukawahukumu viongozi hao, HALAFU UKAANZA KUTAMBA KAMA ZUZU ETI CHAMA KIMEFANYA MAAMUZI MAGUMU NI UJUHA WA HALI YA JUU.

We kweli gamba kwelikweli unaona umeandika cha maana kumbe ujinga mtupu
 
Mtu anaye kitetea ccm anaweza kuwa shetani, jini, mchawi, jambazi, mwizi, mlafi, mzinzi,fisadi,mwovu,mfitini,mzembe, mjinga, mpumbafu,mwehu nk watu wa aina hiyo ndio wanao kitetea chama cha mpinduzi
 
Back
Top Bottom