PRINCEHOPE
Member
- Aug 28, 2013
- 92
- 67
Kuna dogo nilisoma naye shule ya msingi, mkoa fulani, yeye maksi hazikutosha akaenda Private School, Mimi nikachaguliwa kuendelea na elimu karibu na bure. Sasa maisha yamesonga, Dogo form four marks zikatosha akaenda kujiunga na shule moja maarufu na kongwe mkoani Tanga. Dogo akasoma term moja tu, ya pili wakati wa kwenda akakunja kuelekea Dar, akakutana na vijana wakamla hela zote, akauza na alivyokuwa navyo. Mama yake akamtumia nauli ya kurudi mkoani, na aliporudi akaulizwa kulikoni kutokwenda shule, jibu alilotoa ni kuwa walimu hawapo, akimaanisha waliopo hawafundishi. Basi mama yake, akasitisha zile jitihada za kumuendeleza kielimu. Dogo akaanza kuishi maisha aliyoyachagua, kamali, pool table n.k. akaja kuuza cheti cha Form Four, ambapo ndiyo kiini cha mada yangu. Aliyemuuzia, akakitumia kwenda kusoma nursing, akapata kazi. Mwajiri wake hiyo mnunuzi wa cheti na wangu akawa mmoja, Kimbembe kwenye jina sasa, lile jina likawa lina click kichwani kwangu, maana namjua mmiliki. Nikashindwa kuvumilia, nikamuuliza ndugu, huyu mwenye jina namfahamu, vipi, akajibu kuwa ni mtoto wa baba mkubwa, ila majina wazazi waliamua kutupa yanayofanana tu. Nikaridhika kwa sehemu, ila nikawa naendelea kufuatilia. Ohoo, si serikali ya awamu ya tano ilipoanza kufukunyua vyeti vya taaluma, yale dada kasepa, na hajulikani alipo. Jamani tusisitizane kila mtu kwa nafasi yake kama kuna ndugu, wasome na wamiliki vyeti vyao, hata kama kaxungusha, si yake Bwana. Ni bora kuwa na kisepe ukajifunga vizuri, maadamu ni chako hakuna mtu atakayekuja kukuvua, kuliko ukaazima nguo ya mtu, akaja kukuvua mbele za watu.