Nguo kutoka UK

Kuku wa Kabanga

JF-Expert Member
Oct 28, 2009
807
366
wadau habari zenu

Nina suala nahitaji msaada wa mawazo,nina jamaa yangu yupo UK anataka kutuma nguo tuuze hapa bongo,nafikiria kufungua duka kabisa,vp hii biashara ya nguo kutoka UK italipa kweli hapa bongo?naomba maoni na ushauri wenu wakuu.
 
Biashara ya nguo inalipa sana tu, we huoni kuna maduka ya nguo kila kona na wote wanauza
 
Inaweza ikakulipa ila itategemea na location ya duka lenyewe,kwa bei za nguo UK nijuavyo ukiongeza na usafirishaji nguo inaweza kuwa high quality ila ikifika Tz itabidi uiuze bei kubwa ili upate faida.Chukulia mfano jeans...cheapest jeans 10 pounds sawa na Tsh 25000 ukiweka usafirishaji na faida yako labda uiuze Tsh 30000.Ili uweze kuuza kwa bei hii inabidi uwe maeneo ya kisure TZ,ni watu wachache watanunua jeans ya Tsh 30000 wakati wanajua Kariakoo kuna jeans ya 10000 regardless quality.In short nakushauri weka duka lako maeneo ya kisure.Mungu abariki malengo yako.
 
wadau habari zenu

Nina suala nahitaji msaada wa mawazo,nina jamaa yangu yupo UK anataka kutuma nguo tuuze hapa bongo,nafikiria kufungua duka kabisa,vp hii biashara ya nguo kutoka UK italipa kweli hapa bongo?naomba maoni na ushauri wenu wakuu.

huenda ina lipa!!!jaribu lakini sijui kama itakulipa sana,wengi wanauza nguo ambazo wanazinunua toka china kupitia nchi kama uganda na kenya!kwa vile hawasafiri umbali mrefu kuzichukua hata bei inakuwa reasonable kwa wateja wao!!kuna mtu alichukua nguo moja kwa moja toka china, bei ilibidi iwe juu matokeo yake haikumlipa!!
 
Hii biashara ni ya msimu sana. Kumbuka UK kuna misimu minne tofauti ya hali ya hewa na maduka yao huwa yanabadilika kama hali ya hewa inavyobadilika...
Sasa kwa kwetu na hali yetu ya joto ikifika winter UK na mzigo umekuishia dukani, huyu ndugu yako ataenda wapi kununuia nguo zinazoendana na mazingira ya huku?
Mi nimeshaifanya hii biashara... Nilikuwa nanunuia nguo kwenye clearance stores kama matalan clearance, littlewood clearance, nk... Lakini ilipokuwa inafika winter ikabidi niwe nastick na viatu vya kike tu. Kwani nguo haziendani na mazingira ya tz...
Kuhusu bei sasa, inabidi uwe na mtandao mkubwa wa wanaojua na kupenda kuvaa quality products, kwani kama alivyosema mdaui hapo juu... Jeans ya bei rahisi kabisa uk ni kama £10 tena ikiwa on sale, sasa ukishaisafirisha, ukailipia kodi, ukaweka dukani kwako, ili uendelee kusustain inabidi uiuze elf 50 na kuendelea... Je location ya bei hizo unayo? Hapo ndio mi nilishindwa biashara, kwani rent tu ya maeneo ambayo wanunuzi wa nguo za maelfu ni kwa dola kwa sqmtr... Nikapiga mahesabu nikaona sitoweza kwa mtaji niliokuwa nao.

All the best and good luck.
 
Ndo uzuri wa kuuliza kabla hujafanya kitu,asante sana mkuu kwa ushauri.
 
wadau habari zenu

Nina suala nahitaji msaada wa mawazo,nina jamaa yangu yupo UK anataka kutuma nguo tuuze hapa bongo,nafikiria kufungua duka kabisa,vp hii biashara ya nguo kutoka UK italipa kweli hapa bongo?naomba maoni na ushauri wenu wakuu.
Mkuu hujajieleza vizuri nguo gani unazo zungumzia: Mpya au mitumba. Ukieleza vizuri tutakupa ushauri
 
mitumba mkuu.

Kama mitumba hiyo ni rahisi sana kupatikana kwa bei ya sawa sawa na bure, na nyingi ya nguo hizo ni of high quality. Bahati nzuri maduka hayo ya Charity yanayo huza nguo hizo haina mambo ya nguo za msimu; zipo nguo za misimu yote muda wote chaguo lako tu. We sema labda gharama za kuzisafirisha kuja bongo, labda na mambo ya ushuru - we fanya utafiti hapa kuhusu mambo ya ushuru, huna haja ya kuleta container zima, we anza na bales kidogo kidogo mambo yakiwa mazuri ongeza idadi. Goodluck.
 
Asante mkuu.
 
Back
Top Bottom