Ngumi iliyookoa Maisha yangu...!

Ngumi iliyookoa Maisha yangu...!

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Posts
7,472
Reaction score
7,274
Ilikuwa mwaka 2000, mwezi wa kumi, saa moja hivi jioni..
Nilikuwa nimetoka kazini kwangu maeneo ya MIkocheni, kwenye kampuni moja hivi binafsi.

Ilikuwa kawaida yangu kila nitokapo kazini nachukua gari yangu aina ya Toyota Corolla 100 Limited, nafanya kazi za taxi bubu maeneo niliyokuwa naishi Sinza Mapambano, then saa nne tano hivi nalala kesho kazini.
Labda niweke sawa kitu hiki kwanza...nilikuwa nimenunua gari hiyo huku ofisini wakiwa hawahui na sikuwahi kwenda nayo ofisini..

Basi bwana, siku hiyo nikakodiwa na watu wawili hivi maeneo ya sinza Mori...
Kidogo nikama nilistuka hivi maana walikuwa kama wamekauka kauka hivi miili yao, na nilipowaangalia machoni nikaona kama wana kitu hivi..lkn nikapuuza nilijua watu wa mjini wanakuwa na mambo mengi...

Jamaa wakaniambia wanaenda Magomeni Usalama nyuma ya TANESCO tukakubaliana bei, wakaingia kwenye gari, mmoja mbele mwingine nyuma...

Waliniambia kuna mzigo wanapitia maeneo ya 92 Hotel (kwa sasa Mitaa ya SanSiro), nilipo fika pale wakaniambia niingie kulia kunaeneo lilikuwa wazi hivi, zamani palishawahikujengwa banda la makuti likavunjwa.

*******
Nilisimamisha gari, na nikawa nahangaika kuweka muziki mzuri kwenye radio ya gari, nikijua jamaa wanashuka..
Ghafla Yule jamaa wa mbele akatoa kitu kwenye mfuko wa plastic akanielekezea!!!! Nikastuka kuona ni bastola! Kabla sijamaliza kustuka vizuri nikapigwa ngumi nzito usoni nikapiga kelele kubwa aaaaaaagh!
Naona jamaa walistuka kwa kelele yangu, wakaanza kuniambia sogea kiti cha abiria! Nikasogea ….hukohuko ndani bila kushuka…jamaa aliekuwa amenialekezea bastola akampa ile silaha jamaa wa nyuma na jamaa akawa anatitwanga mikonzi utosini akasema tulia mbwa we! Jamaa aliekuwa mbele akakaa kiti cha dereva akaondoa gari kwa spidi kwa mtindo kuround akigeukia tulikotokea kuingia shekilango road tena!!!! Tukio hili lilichukua muda wad k kama 1 tu au chini yake…. kwa jinsi nilivochanganyikiwa hata sikujua gari ilielekea wapi baada ya kuingia tena Shekilango road..!

**********
Akili ilianza kunikaa sawa nilipoona jamaa wa nyuma yangu kaweka waya shingoni kwangu….kama kunikaba hivi huku gari inakwenda kwa kasi mno!…. nikajua leo ndio mwisho wa maisha yangu..kwa haraka na kwa namna ya ajabu nikawaza kwamba jamaa Yule wa nyuma kwa muda huu hajashika ile pisto………..nilipokuwa anawaza hivyo ule waya nikahisi unaanza kuniumiza na kuni kaba koo….
Na wakati huohuo nikirusha ngumi ya mkono wa kushoto kwa nguvu zangu zooote za kufia na kukata roho bila kujali yale maumivu ya ule waya!! Mungu mkubwa ile ngumi niilisikia ikitua kwanguvu kwenye sikio la yule jamaa aliekuwa anaendesha gari…… Ndupf!!!!

******
Ghafla kitedo kile kikaleta vurugu za ajabu kule kwenye gari, kwanza nilisikia kama breki hivi, then kishindo kikali mno kilichokuwa kinaendelea mfululizo pamoja na sauti za vyuma kama vina vunjika pamoja na vioo vyote kwa spidi ya ajabu!!!!


Hadi sasa Yule jamaa wa nyuma sikumbuki alikwenda wapi, ila nilimwona aliekuwa anaendesha gari akiusukuma mlango wa gari kwa miguu then akatoka akikimbia kwa kupepesuka…. Mimi nilijaribu kutoka nikashidwa, mkono wangu wakulia ulikuwa haujongei kufungua mlango wala kusogea nikawa siwezi, nikajitahidi tena wapi sikuweza….
Nilitupa macho nje niakona watu wengi tu sasa , wengine wanasema wamekimbia wote!! Wengine wanasema mmoja yumo kashindwa kutoka , wengine inueni gari tumwokoe jamani!!! Basi ikawa mambo kama hayo…. Nikatolewa nje ya gari kwa kunyofolewa.... wananchi wale wakanilaza chini, nilipo pepesa macho kwenye kigiza katika kadamnasi na nikamwona askari mmoja hapo kwa nje nikapata faraja sana..nikalala chali nikapumua kwa nguvu na kufumba macho…!!!!

*******
Kumbe Eneo lilipotokea tukio hili lilikuwa urafiki karibu kabisa na kituo cha polisi Urafiki pale barabarani!!(Morogoro road) Jamaa baada ya kupata ile ngumi ambayo hakuitegemea aliligonga gari nyingine kubwa hivi kwa nyuma then gari yetu ikapinduka!

******Mwisho
Kisa hiki ni cha kweli, kilinipata wakati huo..nikapelekwa hospitali,nikaja kupona. Ila polisi walishangaa sana kuhusu kisa kile, na tayari nilikuwa na alama shingoni kwangu huku nikimeza mate kwa maumivu umivu hivi.. na ule waya ukakutwa kwenye gari..pamoja na mfuko , pisto haikuonekana!
 
pole sana mkuu kwa yaliyokukuta. Hii yote ni neema ya Mungu inayotukumbusha kutubu.
 
bonge la muvi ... kama naniliu vile ....duh
 
hongera sana hapo sinza mori kuna wakati walipoonea sana,kumbukumbu zangu kuna gari kama sita zimeshaibiwa hapo kwa mtindo huo
 
Mara nyingi kwenye kesi kama hizi watu wanakufa kwa woga, hata kama wanguvu kama simba, cha muhimu ni ktuliza akili na kufikiria option ya haraka sana, majambazi wengi hawana mafunzo ya kijeshi na pia wala hawatumii akili sana, nirahisi kuwaponyoka ukitulia. Ningeweza kutoa mbinu za kiintelejensia hapa lakini ninahofu kaka jambazi atawapawenzie ili waweze kujirikebisha kwenye loose point zao.
 
Mara nyingi kwenye kesi kama hizi watu wanakufa kwa woga, hata kama wanguvu kama simba, cha muhimu ni ktuliza akili na kufikiria option ya haraka sana, majambazi wengi hawana mafunzo ya kijeshi na pia wala hawatumii akili sana, nirahisi kuwaponyoka ukitulia. Ningeweza kutoa mbinu za kiintelejensia hapa lakini ninahofu kaka jambazi atawapawenzie ili waweze kujirikebisha kwenye loose point zao.
zaidi ya hayo unaweza kuchukuliwa kwa kuhojiwa zaidi maana unaweza kuwa ndiwe uliyesaidia lile li muvi la nchi kutokutawalika
 
Mzizi wa Mbuyuumenikumbusha na mimi kuna waati nilikosa kazi nikawa nachukua gari ya bro. akitoka kazini mimi nekwenda nayo kupiga texi bubu niliziona risk nying sana kwenye hiyo kazi haswa ikizingatiwa kuwa jiji nilikuwa silijui vizuri vivyo wakati mwingine nilikuwa nalazimaka kumpa mtu gari ampeleke abiria mtu mwenyewe sikuwa namjua nilimkuta tu kijiweni, lipoona hatari zimezidi nikaamua bora kutafuta kazi nyingine
 
Last edited by a moderator:
Du jamaa yangu pole sana maana hata mm siamini ilikuweje ukapata ujasiri wa kumpiga wa mbele ukamuacha aliyekukaba kumbe wa mbele anaenda gonga lori
Je hiyo Toyota 100 Limited ilipona au uliinyoosha na kuiuza?
 
Back
Top Bottom