Ngorongoro kunani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngorongoro kunani?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Tz Asilia, May 16, 2010.

 1. T

  Tz Asilia Member

  #1
  May 16, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Awali ya yote naomba nitumie nafasi hii kuwasalimu nyote Wanajamii Forum na Kuunga Mkono Mtazamo,itikani, Imani, na Hoja mbali mbali mnazozitoa kuhusiana na Mwelekeo wa Uchaguzi wa Tanzania October 2010.Whether I agree or against,but its freedom of speech as per Article 18 of United Republic of Tanzania Constitution and also it is prediction of what will happen to our general election.

  Baada ya utangulizi huo let me go direct to my concern,NAOMBA KUULIZA NGORONGORO KUNANI? Ni kweli kwamba kupitia vyombo vya habari wanasiasa wengi wametangaza nia zao za kuwania tena Uchaguzi ujao, wengine wakitetea nafasi zao na wengine wametangaza nia zao ya kuwania kwa mara ya kwanza au kujaribu tena kwa kushindwa uchaguzi wa 2005. Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, October ndio wasawa wa mwafaka wa Watanzania kufanya Uchaguzi mkuu hata hivyo wanasiasa waliotangaza nia ya kuwania wanatakiwa wasome alama za nyakati.
  Swali naomba kujua Waliotangaza nia ya kuwania Ubunge Wilaya ya Ngorongoro pamoja na sifa zao, ukiziondoa zile za Kikatiba ya kujua Kusoma na Kuandika.May it pleases you politics investigators
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Tz Asilia,

  Mkuu inaonekana unazijua vyema siasa za Ngorongoro, itakuwa vyema na haki ikiwa utatujuza walau kwa ufupi sana nini kinachojiri huko Ngorongoro.

  Binafsi sina data za Ngorongoro ila najua mbunge wa sasa Mheshimiwa Saning'o Ole Telele alikuwa shahidi muhimu kwenye ile kesi ya mbunge wa Simanjiro Mheshimiwa Christopher Ole Sendeka na mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha Bwana James Ole Millya.Mheshimiwa Saning'o Ole Telele alikuwa shahidi wa Bwana J Millya lakini kwa mshangao wa wengi alitoa ushahidi uliosababisha Mheshimiwa Sendeka ashinde kesi,ajabu zaidi Ole Telele alikuwepo kwenye maandamano ya kumpongeza Mheshimiwa Sendeka.

  Mkuu Tz Asilia nimeanza mbali kidogo si kwa bahati mbaya isipokuwa nilikuwa nataka kukupatia picha ya siasa za mkoa wa Arusha na Manyara ambazo zimeathiriwa zaidi na mtandao uliomungiza Muungwana magogoni.Siyo siri Mheshimiwa E Lowassa alikuwa mwenyekiti/kinara wa mtandao uliofanikisha Muungwana kuwa rais wa nne wa JMT.E Lowassa ana malengo yake ya kisiasa inasadikiwa baada ya Muungwana kumaliza kipindi chake alikuwa apokee kijiti lakini yaliyompata [kashfa ya Richmond]yanatishia adhima yake.Wapo baadhi ya wanasiasa wa mikoa ya Arusha na Manyara ambao walionekana kushabikia/kufurahia/ anguko la Mheshimiwa E Lowassa pengine kwania njema au kinyume chake.Mheshimiwa C Ole Sendeka,Lekule Laiser,Mollel ni vinara wa kundi linalompinga Lowassa kutawala siasa za mikoa ya Arusha na Manyara ambao kwa namna ya ajabu wamejikuta wakikabiliana na kesi zenye lengo la kuwaondoa kwenye ulingo wa siasa.Utakumbula Mheshimiwa Lekule alikuwa anagombea ujumbe wa halmashauri kuu lakini aliishia kubambikiwa kesi ya kutoa rushwa ambayo mwishowe jina lake liliondolewa kwenye orodha ya wagombe.Mheshimiwa Mollel mbunge wa Arumeru Magharibi nae alikuwa akigombea uenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha aliishiia kubambikiwa kesi iliyosababisha jina lake kuondolewa.

  Mheshimiwa Ole Telele mwanzoni alikuwa kwenye kundi la Lowassa lakini baada ya kumgeuka Ole Millya ambae anaandaliwa na kundi la Lowassa kuchukua ubunge wa Simanjiro amewekwa kando tayari wapo wagombea kadhaa wanaandaliwa kuchukua nafasi yake kwa dhambi kubwa ya kumtetea Ole Sendeka.
   
 3. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,405
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  hivi kweli hapo tutapata KIONGOZI BORA AMA BORA KIONGOZI.........? kama hali kwa ufupi ni hiyuo uliyotuelezea ndg NGONGO basi kuna haja wa lazima wananchi wapewe elimu ya uraia kikamilifu ili watumie vizuri kura zao.
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Du! Hivi huko kwenye CC na NEC yao wanayazungumziaje haya, maana hii trend ya Arusha na Manyara ndiyo iliyoenea nchi nzima. Ni kupigana vita na backstabbing ambayo haionyeshi kuwashtua wakubwa na yet inahatarisha amani na utulivu wa nchi.
   
 5. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Laiti Mwalimu Nyerere Angefufuka leo hakiyanani nasema watu wangecharazwa viboko wee na kusekwa ndani. Viboko 12 wakati wanaingia na 12 Wakati wanatoka wakawaonyeshe wake zao na waume zao. Maana Mwalimu alisha sema ikulu kuna nini? Kwa nini watu wakimbilie uongozi. Uongozi ni dhamana, lakini leo watu wanaukimbilia sijui utafikiria nini?
   
Loading...