Ng’ombe 11 wafa kwa kupigwa na radi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ng’ombe 11 wafa kwa kupigwa na radi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Jan 21, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,947
  Trophy Points: 280
  Na Shija Felician, Kahama .

  Jumla ya ng’ombe 11 zimeuawa kwa kipigwa na radi katika kijiji cha Ubagwe ,Wilayani Kahama hali ambayo imewatia hofu wananchi kwa kuwa matukio ya radi kupiga na kuuwa watu ambayo yamekuwa yakitokea safari hii imekuwa tofauti baada ya mifugo hao kuuawa.

  Tukio hilo lililotokea wiki iliyopita saa tisa mchana katika kijiji hicho baada ya mvua kunyesha ambapo radi ilipiga na kuuwa mifugo hao waliokuwa katika zizi huku kati yao 13 wakisalimika.

  Kwa mjibu wa taarifa zilizotolewa na Kaimu Mtendaji wa Kata hiyo ambaye ni Ofisa kilimo na mifugo Charles Costarten alisema kuwa siku hiyo kabla ya radi kulianza kunyesha mvua ndipo ilipopiga na kuuwa mifugo hao.

  Alisema ng’ombe hao ambao ni wa mkulima na mfugaji Nzaia Kibiliti wa Kijiji cha Ubagwe siku hiyo alikuwa anasubiri mvua ikatike aweze kuwapeleka katika malisho ndipo radi ilipopiga na kuuwa mifugo tu huku familia yake ikisalimika.

  Diwani wa Kata ya Ubangwe Robart Mdura na Mtendaji wake Costarten waliwaagiza wananchi kuwazika ng’ombe hao japo mtaalamu huyo alisema hata kama wagewala kwa vitoweo wasigepatwa na madhara yeyote.

  Matukio ya radi kuuwa yamekuwa yakijitokeza mala kwa mala hasa katika kipindi hiki cha masika ambapo yamekuwa yakiripotiwa kutokea maeneo zaidi ya vijijini na kuwa wananchi wametakiwa kuchukua tahadhali hasa wakati wa mvua zinaponyesha
  source:dullonet
   
 2. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Pole kwa mwenye ng'ombe kwa khasara kubwa aliyopata
   
Loading...