Ngoma bado mbichi UWT K'njaro, wagombea walioenguliwa waanika mtandao wa rushwa

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
198
Reaction score
209
Moshi bado unaendelea kufuka ndani ya Jumuiya ya wanawake ya Chama cha mapinduzi(UWT)baada ya wanachama wake walioenguliwa katika kinyang'anyiro cha kusaka nafasi ya ubunge wa Viti maalumu kufichua mtandao uliotumika kutawanya rushwa kwa wajumbe .

Miongoni mwa wanaotajwa kutawanya rushwa kwa wajumbe katika wilaya za Mwanga,Rombo Hai na Moshi mjini n Vijijini ni mtoto wa mmoja wa walioshinda kwenye kura za maoni akishika nafasi ya pili lakini kwa sababu sijaweza kumpata kujibu tuhumu hizo pamoja na wengine nashindwa kuweka majina yao hapa.

Lakini wagombea hawa wamerusha tuhuma nyingi kwa viongozi wao wa UWT mkoa ambao ni mwenyekiti Elizabert Minde na katibu wake Jane Chatanda wanaodaiwa kuwasaidia wagombea kushinda kutokana na vishawishi vya rushwa .

Wanakitaka chama cha mapinduzi(CCM)kuchukua hatua kwa viongozi wa Jumuiya ambao wanajaribu kukichafua chama kutokana na maslahi yao binafsi .


naendelea kuwatafuta wanaodaiwa kuwa mawakala wa wagombea wanatuhumiwa kutawanya rushwa kwa wajumbe,baada ya kuwapata nitaweka hapa majina yao na kwa wale ambao hawakuweza kusoma andiko langu la jana naliweka hapa ili usome tena.


SOMA



Huko mkoani Kilimanjaro hali si shwari ndani ya Jumuiya ya Wanawake ya Chama cha mapinduzi(UWT)kutokana na kilio cha wanachama wake kulalamikia vitendo vya rushwa,kujuana,upangaji wa matokeo na upendeleo katika kwapata washindi wa kura za maoni ndani ya jumuiya hiyo.

Kinacholalamikiwa na wengi ni kwamba wanachama wenye ushawishi na wenye sifa walienguliwa katika kinyang'anyiro hicho na viongozi wa UWT mkoani humo akiwamo mwenyekiti wao Elizabert Maro Minde na katibu wake Jane Chatanda lengo ni kuwawezesha watu wao kushinda bila vikwazo.

Wanasema wilaya zote saba za mkoa wa Kilimanjaro zilitoa watia nia lakini cha kushangaza wilaya nyingi majina ya watia nia hayakurudi kabisa si kwa sababu wagombea hao hawana sifa hapana hii ni kutokana na mwenyekiti,Elizabert Minde kuwa na mtu wake aliyekuwa akimhitaji.

"Hata baada ya kumalizika kwa uchaguzi mwenyekiti alienda kwenye sherehe ya mmoja wa walioshinda ni kwa sababu ndiye alikuwa chaguo lake na huyo ndiye aliyempigania akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa UWT mkoo wa Kilimanjaro kwa hiyo alikuwa analipa fadhila",anasema mmoja wa waliokuwa sehemu ya watia nia ambaye jina lake lilienguliwa.

"Rushwa imetumika sana kwenye huu uchaguzi,sisi hatuna shida na chama chetu cha mapinduzi na kina nia njema kabisa lakini uharamia umetumika ndani ya UWT,haiwezi ingia akilini kwamba wapinzani wote wa Zuena Bushir hawana sifa hapana hii ni kwa sababu ya rushwa lakini kwa nini mwenyekiti awe na mgombea wake?",amehoji mtu mwingine.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utekelezaji UWT mkoani humo anatajwa kuwa alikuwa akimpigia kampeni mmoja wa watia nia kitendo ambacho kinadaiwa kuwa ni kinyume kabisa na taratibu za uongozi kwani mjumbe huyo ni sehemu ya viongozi wa kutoa maamuzi.

Kwa nini upangaji wa matokeo?,watia nia hawa wanasema ukiangalia aliyeongoza kwenye kura Esther Maleko aliyepata kura 1149 na wa pili Zuena Bushir (kura 964) na Regina Chonjo aliyepata kura 145 ni dhahiri kuwa kulikuwa na upangaji wa matokeo.

Kwenye mchakato huo,Caroline Lyimo alipata kura 109,huku Never Zekeya akipata kura 108 wakti Pamela Mallya akipata kura 69 ambapo mary nashenda alipata kura 19 na wa nanne alikuwa Haika Ngowi aliyepata kura 12.

Walionguliwa katika kinyang'anyiro hiki ni Rusma Ndosi kutoka wilaya ya Hai ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Kilimanjaro,Sophia Virgo,Edna Mafue na Winnie Jonas,mwingine ni Khadija Kangero kutoka wilaya ya Rombo na mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Rombo.

Wilaya ya Same aliyeenguliwa ni Namrinji Mzanza mfanyabiashara na mjumbe wa kamati ya Utekelezaji ya UWT mkoa wa Kilimanjaro,mjumbe wa Halmashauri kuu ccm wilaya na pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya,yupo pia Edith Banzi diwani aliyemaliza muda wake.

Kwenye wilaya ya Mwanga yupo Clara Mdee huyu anatajwa kuwa ni mmoja wa makada mashuhuri katika wilaya ya Mwanga .

HOJA YA UKOMO WA VITI MAALUM IKOJE?

Chama cha mapinduzi kimeweka ukomo kwa wabunge wa viti maalumu waliokaa muda mrefu kwenye nafasi hiyio na kanuni hizo zitaanza kutekelezwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2030 lakini katika mkoa wa Kilimanjaro kanuni hiyo imeanza kutekelezwa kabla ambako Shally Raymond alienguliwa kwa kigezo hicho.

Lakini mkoani Simiyu miongoni mwa watia nia alikuwemo Esther Mdimu ambaye amekuwepo kwenye nafasi hiyo tangu mwaka 2005 na katika uchguzi huu jina lake lilirudi na amekuwa sehemu ya washindi,yupo Catherine Magige wa Arusha,yupo Liziki Rulida wa Lindi naye ni moja wabunge wa muda mrefu hawa majina yao yalirudi lakini wameangushwa kwenye sanduku la kura.

Hapa unaweza kuona wanaokichafua chama cha mapinduzi ni hawa viongozi wa hizi jumuiya ambao wamekuja na agenda zao za kuwa na wagombea kwenye mifuko yao,una maoni gani kuhusiana na hizi tuhuma za upangaji matokeo,kubebana na matumizi ya rushwa?
 

Attachments

  • Mama Minde.jpg
    18.8 KB · Views: 19
Hakuna uchaguzi wa ndani wa chama changu CCM usiokuwa na rushwa! Kama ulikuw hulijui sikiliza clip ya yule mbunge wa CCM.
 
Rushwa na sisiem ni kama ibada walah tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…