Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa Jamii Forums toka ikiitwa Jambo Forums.Kila siku lazima niingie humu ili kujua kinachoendelea hapa nchini na dunia nzima kwa ujumla kwenye nyanja mbalimbali kama siasa,uchumi,michezo, masuala ya kijamii nk.Lakini waswahili wanasema" Ukitaka kuujua uhondo wa ngoma uingie ucheze" Nami nimeona niingie ili niweze kuchangia.