Ngeleja: Mgawo wangu Akaunti ya Tegeta Escrow ni wa msaada

Ngeleja: Mgawo wangu Akaunti ya Tegeta Escrow ni wa msaada

idoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
3,051
Reaction score
1,423

Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja, amesema mgawo wa Sh. milioni 40 anaodaiwa kupewa kutoka kwenye fedha zilizochotwa kifisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ulikuwa msaada wa kawaida kama ambavyo wabunge wengine wamekuwa wakipewa.

Alisema hakuna mbunge anayeweza kutekeleza miradi ya maendeleo katika jimbo lake bila misaada. Ngeleja aliyasema hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kamanga kata ya Nyamatongo wilayani humo wakati akiwashukuru wapigakura wake kwa ujasiri wao wa kumkingia kifua dhidi ya kashfa ya akaunti hiyo inayomkabili.

Alisema siyo dhambi kwa wadau wa maendeleo zikiwamo kampuni, marafiki na taasisi kuchangia fedha ili kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika majimbo yao. Kutokana na hali hiyo, aliwashukuru wapigakura wake kwa kumkingia kifua dhidi ya shutuma zinazoelekezwa kwake kwa kuwa wanalitambua hilo.

CHANZO: Nipashe
 
Ni mwizi kama wengine tu,hana jinsi ya kujisafisha.
 
hii kashfa imewachanganya sana wanasiasa.

sitaki kuamini mtu kama ngeleja anatoa majibu marahisi hivyo..

ngeleja msomi wa nguvu..10 yrs with Pricewaterhouse coopers kama consultant wa sheria.

mwanasheria mkuu wa vodacom, waziri wa nishati.

tatizo la escrow, watu wanatoa majibu marahisi katika maswali magumu.

hata mtoto anaona anadanganywa
 
Huo msaada wa nn mbona anataka kudanganya watu
 
hii kashfa imewachanganya sana wanasiasa.

sitaki kuamini mtu kama ngeleja anatoa majibu marahisi hivyo..

ngeleja msomi wa nguvu..10 yrs with Pricewaterhouse coopers kama consultant wa sheria.

mwanasheria mkuu wa vodacom, waziri wa nishati.

tatizo la escrow, watu wanatoa majibu marahisi katika maswali magumu.

hata mtoto anaona anadanganywa
tatizo wanaodanganywa na wao wanaona sawa!
 
Ukijua fika kwamba wewe ni mtumishi wa umma, tusaidie ufafanuzi wa haya mawili

1. Kwa nini hukutangazia umma kabla kwamba umepata kiasi hicho cha fedha na kusudio lako ni nini.
2. Kwa nini pesa ziingie kwenye account yako binafsi
 
maswali muhimu sana hayo. ukizingatia kuna mfuko wa jimbo, pesa zingetakiwa zielekezwe humo. na angewambia wapiga kura wake tangu awali kuwa alipokea msaada! unaweza kukuta mpaka sasa hamna kitu amefanyia hizo pesa jimboni kwake, anategea azitumie kipindi cha kampeni!
 
SAKATA LA ESCROW: Tume ya Maadili yahairisha kusikiliza suala la A. Chenge kujipatia Sh1.6bn za escrow baada ya mbunge huyo kuwasilisha zuio la korti leo, Dar. Chezea sheria ww?
HAYA NGEREJA UA BRO AMEENDA MAHAKAMANI
 
Yaani baada ya kesi kutolewa hukumu ndio mtuhumiwa anakurupuka kujitetea?

Mkuu huo ndiyo utaratibu na kawaida ya siasa zetu hapa nchini. Yaani wakati wa sakata watuhumiwa walikua kimya lakini lilipoisha ndipo wanaanza kujitokeza na kujifanya kutoa utetezi, yaani bure kabisa.
 
Fisadi tu huyo, bahati mbaya sana nchi haina kiongoz alipaswa kuwa jela.

Yaana anajitapa kupokea rushwa tena hadharani
 
SAKATA LA ESCROW: Tume ya Maadili yahairisha kusikiliza suala la A. Chenge kujipatia Sh1.6bn za escrow baada ya mbunge huyo kuwasilisha zuio la korti leo, Dar. Chezea sheria ww?
HAYA NGEREJA UA BRO AMEENDA MAHAKAMANI

Yaani hii nchi bhana. . . . .jamaa anachachafya atakavyo, . .
 
Hii ni kuonyesha ni kiwango gani wanasiasa wa Tanzania wanavyowadharau uelewa wa wapiga kura wao! Hizo pesa mbona hazikwenda kwenye mfuko wa jimbo ila mahali salama ni Mkombozi Bank? Alitaarifu taasisi husika kuwa amepokea pesa za maendeleo ya jimbo?!!
 
msaada milioni 40?

Victoire ina wezekana hata zaidi ya hiyo tatizo ni kwa nini haikwenda mfuko wa jimbo siku zote mpaka imekutwa Mkombozi Bank kwenye personal account.

Nina uhakika jimbo lake kama mengine mengi lina changamoto nyingi sana zenye kuhitaji hiyo fedha kujikwamua.
 
Back
Top Bottom