Ngeleja chaguo la Watanzania, Lowassa chaguo la CHADEMA

Ngeleja chaguo la Watanzania, Lowassa chaguo la CHADEMA

Richcountrytz

Member
Joined
Dec 17, 2014
Posts
9
Reaction score
2
Aminini maneno yangu: Katika siasa za Tanzania, siasa za kuchafuana... binafsi sijawahi kuona Viongozi wa Chadema wakipanda majukwaani kusema mabaya au mabaya ya kutunga ya Mhe. Lowasa kama wafanyavyo kwa watu wengine vigogo wanaotajwa katika kuwania Urais kupitia tiketi ya CCM. Naamini kama ninyi mmeona basi itakuwa mara chache mno.

Point iloyopo hapo si kama wanamwamini na kumsifu sana Lowasa au ni kiongozi msafi sana bali hiyo ni strategy yao ya kwenda ikulu 2015. Wanamsifia na kutomsema vibaya ili CCM tujichanganye kulipitisha jina lake then wapate mteremko tu kumgaragaza wakati wa uchaguzi coz wanajua namna alivyochafuka na kuwa yeye si chaguo la watanzania kwa sasa.

My take: Tulale na tuamke tuhakikishe jina safi na hitaji la watamzania ndilo tunalohakikisha linapita kwa tiketi ya CCM badala ya lowasa ambaye tayari watu washamuwekea mipango ya ushindi ili tuwashangaze.

Tusiwaze sana tumpate nani maana Jina thabiti na chaguo la watanzania kwa sasa ni William Ngeleja. Twende na Ngeleja 2015.
 
  • Thanks
Reactions: Gor
Ni kweli Ngeleja Ni kijana mwenye uwezo wa kudeliver vitu vikaonekana. Ni huyu huyu Ngeleja alianzisha mchakato wa ReA ambao kwa sasa umeme vijijini Ni zaidi 36% kutoka 12% ya awali.
Kunaambo mengi ambayo kijana huyu ameyafanya kwa hakika anastahili kuongoza nchi 2015.
 
Ni kweli Ngeleja anafaa hata migao ya kifisadi haiachi mfano ni mgao wa ESCROW alilamba million 40
 
Janja ya CHADEMA ya kumkumbatia LOWASSA inajulikana, ni kutafuta urahisi wa kwenda Ikulu, kwa taarifa yao hakuna atakayempitisha LOWASSA kugombea urais. Watu wanakula pesa anazogawa kwa vile wanajua ni kodi za watanzania mwisho wa siku anapigwa chini.
 
Kwendeni zenu mnakuja kupiga debe hapa jf.huyo ngeleja labda akawe rais wa wasukuma pale ccm sijaona lowa sa ndio huyo kakamatwa anagawa rushwa zanzibar huyo ngeleja ndio nae kapokea fedha za escrow bado mnakuja kuleta ujinga wenu hapa.
 
Kwendeni zenu mnakuja kupiga debe hapa jf.huyo ngeleja labda akawe rais wa wasukuma pale ccm sijaona lowa sa ndio huyo kakamatwa anagawa rushwa zanzibar huyo ngeleja ndio nae kapokea fedha za escrow bado mnakuja kuleta ujinga wenu hapa.
LOWASSA, NGELEJA kwa KiZANAKI wote tunawaita MAKANJANJA.
 
Ngeleja zile pesa za escrow ndo ameshaanza kuhonga wahuni wenzake waje kumpigia debe humu DR.Slaa ndo raisi mtarajiwa wa watanzania chaguo la wananchi
 
Kwendaaaa,,, hako kajamaa kila kashfa kapo,, nilikaona bungeni kashfa ya escrow kamekunjamana kama sangara wa kukausha,,
Ngeleja ni mtoto wa LOWASSA, refer urafiki wa LOWASSA na Rostam Aziz. Wote ni mafisadi.
 
anafaa huko dar labda sababu sisi tuko jimboni kwake hakubaliki huku au ndiyo ile nabii hakubaliki kwao?
 
​Huo ndio ukweli, hatutaki mwizi mwingine Ikulu baada ya mwizi huyu aliyekuwemo Ikulu kumaliza muda wake.
ni kweli mkuu hatuwezi kukubali kuendelea kuongozwa na wezi wa pesa za umma ccm
 
  • Thanks
Reactions: BAK
​ndo shida ya kupiga viroba tangu asubuhi ona sasa zinakuja thread za mazingaombwe kama hizi
Hawa team LOWASSA wana uswahiba wa kinafiki na team SLAA, wamewaambukiza viroba. Naona wanamvuta na kijana wa rafiki yake na ROSTAM AZIZ naye wanamdanganya kuwa anaweza kuwa rais wa nchi hii, japo ana kashfa kibao.
 
Back
Top Bottom