mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,793
- 7,165
kwani ngeleja kafa? mbona mnampa sifa za marehemu? alipokuwa madarakani mbona mlikuwa kimya au tatizo ubunge?
Nilishawai kusema ktk uzi mmojawapo uliokuwa unamzungumzi Ngeleja, kuwa mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Na haki ina sifa kuu tatu 1.Itolewe kwa mlengwa 2. Kwa wakati 3. Itolewe bila masharti. Ngeleja ni miongoni mwa Vijana ambao ni azina kubwa sana ya taifa, amelitendea haki taifa la tanzania. Mungu amjalie ktk maono yake kwa taifa hili.
Papason,Ngeleja siyo mwizi bana,kubali tu kwamba jamaa yuko vizuri ana uwezo wa kazi balaa afu anajenga hoja hakunaga! The guy is presidentaĺ material.
AWAMU YA NNE IMEINUA SEKTA YA NISHATI, MADINI
Kuanzishwa mfumo wa ununuzi mafuta kwa wingi (BPS) katika biashara ya mafuta ya petroli nchini, kwa kiwango kikubwa kumerahisisha usimamiaji wa kodi na kupunguza vikwazo vya uagizaji mafuta.
Maeneo hayo yote mawili yamepelekea kuimarisha ukusanyaji kodi utokanao na mafuta ya petroli.
Hilo limebainika baada yabutafiti uliozinduliwa na mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji (ewura) baada ya kufanywa na shule ya biashara ya chuo kikuu cha dar es salaam (UDBS: Idara ya uchumi).
BPS(Bulk procurement system) imekwenda mbali zaidi katika kudhibiti uendeshaji kwenye sekta ndogo ya mafuta nchini.
Ukipewa jina la 'hatua za udhibiti katika sekta ndogo ya mafuta nchini Tanzania, matokeo ya utafiti huo yanaonesha tangu kuanzishwa mfumo wa Bulk procurement system (BPS), kumekuwepo na upunguaji kwa kiasi kikubwa wa bei ya mafuta na kuongezeka kwa kutii mifumo ya udhibiti , na uwazi katika sekta ndogo ya mafuta kwa ujumla.
BPS ilianzishwa kwa ukamilifu januar,2012 kama njia mojawapo ya kukomesha udanganyifu uliokuwa ukifanywa zaidi na kampuni za masoko ya mafuta nchini Tanzania, ambavyo si tuu yaliinyima mapato serikali, lakini pia yalilazimisha wateja kulipa zaidi kwa bidhaa za mafuta.
Mshindi wa zabuni ya kwanza alizawadiwa tuzo Novemba-Desemba 2011 ingawa utekelezaji wake ulianza januari 2012. Utafiti huo ulijikita zaidi katika madhara na faida za wadau katika sekta ndogo kuhusu mapato ya kodi, kuhusu utupaji wa bidhaa za mafuta zipitazo Tanzania na jinsi ya kukabiliana na athari mbaya juu yake.
Pia ilijikita kuhusu uanzishwaji na ufanisi wa BPS ukichambua faida halisi na hasara kwa uchumi pamoja na upangaji bei za mafuta.
Akizungumzia matokeo ya utafiti huo, Profesa Haji Semboja anasema "kwa sasa wote tunafahamu ni mafuta kiasi gani yanaingizwa nchini na hii imesababisha ongezeko la asilimia 14 ya mapato ya kodi.
Tanzania ni mfano mmoja wapo wa nchi ambazo zimepata mafanikio makubwa katika kusimamia sekta ndogo ya mafuta.
Katika hilo baadhi ya nchi kadhaa katika kanda ya afrika zimeona ni sahihi kutembelea Tanzania kujifunza jinsi ya kutenda kazi kwa ufanisi zaidi kudhibiti sekta ndogo ya mafuta.
Utafiti huo uligundua zaidi kwamba, uwekaji alama katika mafuta kama hatua ya kupambana na utupaji imesababisha ongezeko katika mapato ya kodi ya sh. Bilioni 146.5 katika mwaka 2010/2011, sh. Bilioni 129.8 katika mwaka 2011/2012, na sh. Bilioni 192.2 katika mwaka 2012/2013. Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa BPS pia uchakachuaji mafuta ambao ulikuwa ni changamoto kubwa kwa Tanzania umepungua kwa kiasi kikubwa.
Katika mafanikio, hii imesababisha kuongezeka kwa ukusanyaji mapato ya kodi kama jambo la ukweli.
Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi, anasema tangu kuanzishwa kwa mfumo wa BPS wa bidhaa za mafuta januari 2012, kumekuwepo na maboresho na ufanisi mkubwa katika bandari kwenye ugavi wa mafuta nchini Tanzania.
Kwa kiasi kikubwa, tumeshuhudia kushuka kwa kasi kwa ada ya meli zilizokuwa zikipaki bandarini ambazo zilikuwa zikitozwa kabla ya kuanza kutumika BPS.
"Kutoka wastani wa siku 60 za chombo kusubiri kupakua mizigo hadi takribani siku 3" alisema.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu huyo, uagizaji wa bidhaa za mafuta zinazopitia nchini uliongezeka kati ya mwaka 2009/2010 na mwaka 2012/2013 kutoka lita milioni 262 hadi lita milioni 556 kwa ajili ya petroli sawa na ongezeko la asilimia 112 na kutoka lita milioni 541 hadi lita bilioni 1.28 ya dizeli, likiwa ongezeka la asilimia 136! Ufanisi wa hivi karibuni wa bidhaa za mafuta ya petroli kutoka, Januari hadi Desemba 2013, unaonesha kuwa lita bilioni 4.7 za bidhaa za mafuta ya petroli ziliingizwa nchini Tanzania kupitia Bandari ya Dar es salaam na kituo cha mpaka cha sirari," anabainisha Ngamlagosi.
Faida
Mfumo wa BPS umekuwa na ustawi wa faida wa sh. Bilioni 121.57 kuhusu uchumi wa Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2012/13 kwa njia za punguzo la tozo kwa meli zinazosubiri kupakua mizigo.
Mfumo wa BPS umepunguza idadi ya siku za kupakua mizigo kutoka 45 hadi siku 3, ambapo ni sawa na ustawi wa pato la sh. Bilioni 25.7.
Pia mfumo wa BPS umeongeza ufanisi katika uagizaji wa bidhaa za mafuta ya petroli kwa kuimarisha taratibu zinazohusika, kukuza ushindani na kuboresha matumizi ya sehemu ya upakuaji mizigo.
NANI AMEFANIKISHA KUANZISHWA MFUMO WA BPS nchini?
Ni muhimu kujua hili hasa kwa sababu mfuml huo umesaidia sana kudhibiti vitendo vichafu vilivyokuwa vimekithiri ambavyo vilikuwa vikiichafua sekta ndogo ya mafuta ya petroli.
Vitendo hivyo havikuwa na ukomo, uchakachuaji mkubwa wa mafuta, utupaji wa bidhaa za mafuta yaliyopo na kuongeza gharama za uagizaji ambao ulisababisha mfumuko wa bei za mafuta kwenye vituo vya petroli.
Yote kwa yote, hali hiyo ilisababisha soko kutokuwa na ufanisi wa juu na kwa hiyo zaidi kutokuwa na ushindani.
Mtu ambaye alikuwa nyuma ya mpango ambao sasa unatumiwa na Ewura kwa mafanikio makubwa katika kipindi kifupi si mwingine zaidi bali ni WILLIAM NGELEJA.
NGELEJA mbunge wa jimbo la sengerema kutoka mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi (CCM), ambaye alikuwa Waziri wa Niahati na madini wakati BPS ilipopokelewa kwa ajili ya utekelezaji.
NGELEJA awali alikuwa naibu waziri wa Nishati na Madini kuanzia januari 2007-Mei 2008, baadaye Raisi Kikwete alimteua kuwa waziri wa Nishati na madini, nafasi ambayo alidumu nayo hadi mwaka 2012 alipojiuzulu baada ya zengwe la kukinusuru chama kutawala.
Ni ukweli kwamba mafanikio hayo ambayo hayajawahi kufikiwa na mtu yeyote katika sekta za Nishati na Madini ya uchumi wa Tanzania ni matokeo ya mipango na maono na ubunifu kwa kiasi kikubwa wa Waziri huyo wakati huo.
Utafutaji wa gesi asilia na mafuta ulianza kushika kasi kwa nguvu wakati NGELEJA alipokuwa waziri wa sekta hiyo .
Manunuzi ya mafuta kwa wingi moja ya "zawadi" kubwa ambayo Raisi Kikwete amewahi kutoa kwa watanzania ni mfuko wa manunuzi ya mafuta kwa wingi. Kwa mujibu wa ripoti ya serikali ya wizara ya nishati na madini, mpango huo umeisaidia Tanzania kuokoa mabilioni ya shilingi katika biashara ya mafuta.
Mradi wa bomba la gesi kutoka mtwara hadi Dar es salaam ni miongoni mwa maendeleo mengine makubwa katika ustawi wa taifa chini ya serikali ya Raisi Kikwete wakati NGELEJA alipokuwa waziri wa sekta hiyo ni ujenzi wa bomba la gesi asilia lenye urefu wa km 500 linalosafirisha gesi kutoka mtwara hadi Dar es salaam.
NGELEJA kwa kushirikiana na TPDC alifanya kazi katika mradi huo kuanzia mwaka 2009 kabla ya kujiuzulu serikalini Mei 2012.
Mradi wa mchuchuma-liganga , mambo makubwa ambayo Rais Kikwete amefanya katika miaka 10 ya kipindi chake na ambayo ni kichocheo kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi ni pamoja na mradi wa makaa ya Mawe na chuma wa Mchuchuma na Liganga wilayani Ludewa,Mkoa wa Njombe.
Mradi huo ulikuwa kwenye mipango ya serikali kwa miongo kadhaa hadi mwaka 2011 wakati ulipopata mwekezaji chini ya usimamizi wa NGELEJA.
Baadhi ya faida za mradi huo wenye thamani ya dola bilioni 3 ni uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe wa megawati 600, fursa za ajira na mapato ya fedha za kigeni kutokana na mauzo ya chuma na makaa ya mawe.
Umekula maharage ya wapi wewe?
Nicholas ni ujinga tu ndo unakusumbua,yaani hata huelewi kwamba nchi hii inaongozwa na sheria. Ngeleja angekuwa mwizi au fisadi si angekuwa ameishasombwa mahakamani. Ina maana Ngeleja yuko juu ya sheria? Acha kutapika hapa,jenga hoja ndo maana mkiulizwa msaada aliopewa ngeleja unatofautianaje na misaada wanayopata wabunge wengine akiwemo kakako zzk jumla ya shs 150mil from Tanapa na Nssf (119mil) na from PAP ya singasinga Sethi (35mil)?
Yaani mnajifanya hamjui aliyofanya ngeleja?
Yaani mnajifanya hamjui aliyofanya ngeleja?
Hamjui kwamba bei ya kuungiwa umeme vijijini kwa sasa ya shs 27 elfu ilianzishwa na ngeleja kupitia wilaya za Mbozi na Kilombero? Mnasema kila alichofanya ngeleja ilikuwa utimizaji wa wajibu,basi msifieni kwa kubuni mradi wa bomba la gesi Mtwara-Dar mwaka 2009 wakati haukuwemo kwenye Ilani ya CCM ya mwaka 2005-2010. Mradi huu ulianza kutekelezwa mwaka 2011 wakati ngeleja akiwa waziri.
Watanzania tuache cheap political styles. Mtu ananunua kitu kulingana na uwezo alionao. Huwezi leta hoja nyepesi kama kununua Mercedec Benz kama hoja dhidi ya mtu. Mambo mema aliyotufanyia wananchi mpaka sasa yameacha legacy kubwa kiasi kwamba anapaswa kuwatumikia wananchi husika kwa ngazi ya juu zaidi.Huyu Ngeleja ni kikaragosi cha fisadi Rostam toka akifanya kazi Vodacom. Alipokuwa waziri wa Nishati alifisadi mikataba ya mafuta na kupata fedha nyingi zilizomuwezesha kununua gari aina ya Mercedes benz kule D.T Dobie kwa kulipa mamilioni ya shilingi kwa fedha taslimu!! Kwavile alikuwa amefisadi na kupata hizo fedha, baada ya kulipia lile gari akaogopa kwenda kulichukua na ilibidi aliache kule kwa muda mrefu sana na hata baada ya kulichukua anaogopa kulitembelea na hivyo kulifungia nyumbani kwake!!!That is Ngeleja the aspiring presidential candidate for you!!
Fedha aliyopewa Ngeleja haikuwa rushwa wala fadhila za kiuchumi isipokuwa ni msaada kwa ajili ya shughuli mbali mbali ndani na nje ya jumbo lake. Na kuthibitisha hilo baada ya kupewa shm mil 40 alilipa kodu ya shs mil 13. Na hii imeongeza mapato kwa serikali yetu. Tofautisha ufisadi na msaada wa kifedhaWewe nawe,hivi ni mafisadi wangapi wameiba na bado wapo mitaani wanapeta? Walio iba fedha za epa waliambiwa warudishe hizo pesa,huko ndio kufikishwa mahakamani?